Wednesday, October 31, 2012

JCB AFUNGUKA KUHUSIANA NA HABARI ZINAZOANDIKWA KWENYE MITANDAO

JCB AFUNGUKA KUHUSIANA NA HABARI ZINAZOANDIKWA KWENYE MITANDAO

Siku za hivi karibu baada ya kutokea kifo cha Lexa huko Arusha sasa mitandano mbalimbali inasema kwamba JCB amehusika katika kifo hicho lakini yeye mwenyewe anafunguka na kusema kwamba kuna baadhi ya mitandano ya hapa Tzee inapenda sana kuandika habari ambazo sio za kweli kwani yeye ndiye alikuwa ni mtu wa mwisho wa kuongea na Lexa lakini angependa kuwajulisha kwamba yeye sio muhusika katika kifo hicho wahusika wa kifo hicho wapo chini ya Usalama wa Polisi na uchunguzi unaendelea huko Arusha.Hayo ndiyo maneno ya JCB baada ya kufunguka kuhusiana na baadhi ya mitandano kuandika kwamba yeye anahusika katika kifo cha Lexa kilichotokea siku za hivi karibuni huko Arusha.

LINA AFUNGUKA BAADA YA KUFANYA COLLABO NA AMINI



LINA AFUNGUKA BAADA YA KUFANYA COLLABO NA AMINI
Baada ya kusikia habari katika mitandao mbalimbali kwamba mwana dada Lina amefanya collabo na Amini niliamua kumpigia simu Lina na anielezea ilikuwaje mpaka wakapiga collabo hiyo alieleza kwamba japokuwa Amini alikuwa ni Ex boyfriend wake sasa jana Amini baada ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa alimuomba wakafanye kitu ambacho ni suprise kwa mashabiki wao na ndiyo maana wakafanya ngoma yao mpya chini ya Producer C9 lakini Lina alifunguka na kusema kwamba jina la hiyo ngoma bado hawajaipa ila ndiyo wapo katika mchakato wa kuipa jina na wanatarajia kuiachia siku za hivi karibuni info by Lina Sanga.


MWANAMKE AMSHTAKI CEE LO GREEN KUZISHIKA SEHEM ZAKE NYETI BILA RUHUSA

MWANAMKE AMSHTAKI CEE LO GREEN KUZISHIKA SEHEM ZAKE NYETI BILA RUHUSA

kwenye mtandao kuna taarifa ya kusikitisha kuwa singer-songwriter, rapper, actor and record producer, maarufu kama cee lo green anachunguzwa na polisi nchini marekani kwa kile kilichoelezwa na mwanamke mmoja akidai kuwa cee lo green alimshika sehem nyeti bila ruhusa yake na tukio hilo eti lilitokea kwenye restaurant moja jijini los angeles, na polisi walifika mpaka kwenye mgahawa huo na kufanya mahojiano na wafanyakazi wake pamoja na manager lakini wote walijibu kuwa hawaja shuhudia kitendo hiko kikitokea
akiongea na mtandao wa tmz cee lo green ametiririka kuwa hajafika katika mgahawa huo kwa miezi mitatu sasa, na akasisitiza kuwa hakuna kitu kama hicho.
cee lo green sasa hivi ni judge wa shindano la kusaka vipaji la the voice nchini marekani
polisi wanaendelea na uchunguzi na bado kesi haijafika mahakamani

TAHADHARI KWA WATUMIAJI SIMU ZA MKONONI:

TAHADHARI KWA WATUMIAJI SIMU ZA MKONONI:

Simu zinatumia Mionzi ya
 MICROWAVE ambayo huwezesha
 kuunganisha simu yako kwenda
 kwenye Mnara na mnara
 ... huunganisha Simu yako na Mitambo
 ya Mtandao wako ambapo pia
 Hurudishwa kwenye mnara hadi kwa
 mtu Unaye mpigia. Microwave ndio
 njia kuu ya muunganisho huo. Lakini
 kunamdhara mengi mtu huyapata
 kutokana na kuwa karibu na Mionzi
 hiyo ambayo hadi sasa bado
 haijafahamika ni kwa kiasi Gani.
 Uchunguzi umeonyesha kuwa kuna
 madhara mengi ya kiafya tunayapata
 kutokana na Matumizi ya simu.
 mfano wa magonjwa hayo ni
 1. KUUMWA KICHWA MARA KWA
 MARA
 2. PRESSURE YA KUPANDA NA
 KUSHUKA
 3. UVIMBE KWENYE UBONGO
 4. KANSA
 5. ALZHEIMER
 6. NA MENGINE MENGI
 Hatuwezi kujizuia kutumia simu na
 Hatuwezi kuzuia hiyo mionzi ya
 MICROWAVE sababu ni sehemu ya
 shughuri zetu za kila siku ila
 tunaweza KUPUNGUZA. hapa
 nawaletea Njia chache za kupunguza
 Mionzi ya MICROWAVE isituletee
 matatizo makubwa zaidi.
 1. Punguza matumizi yasio lazima
 ya simu.Mfano Ongea mda mfupi
 kwa kutumia simu sio muda
 mrefu uweunaongea, Uchunguzi
 umeonyesha kuwa ukiongea kwa
 DAKIKA mbili haileti madhara,
 (Alter natural electricity of the
 Brain)
 2. Watoto wasiruhusiwe kutumia
 Simu bali pale tu inapobidi.
 3. Tumia Earphone za wireless mfano za bluetooth. ni nzuri zaid kuliko za
 wire,Earphones za wire zinaongeza wingi wa mionzi
 sababu pia zinatumika kama
 antena ya simu,
 4. Usiweke simu kwenye Mfuko wa
 suruari au shati au
 kiunoni,sehemu za mwili
 zinapitisha mionzi vizuri zaidi
 sababu pia ni njia ya neva za
 ubongo na chini ya mwili.
 5.Usitumie simu kwenye chumba
 kidogo au lift au gari. Sababu
 Simu itatumia nguvu nyingi
 kuvuta mionzi ili kuwezesha
 mawasiliano.
 6. Ukipiga simu subiri hadi mtu
 apokee ndipo uweke sikioni
 kusikiliza na sio wakati ina
 connect.
 7. Usipige simu kama network ipo
 chini au signal inaonyesha bar
 moja au ndogo, simu itavuta
 mionzi zaidi ili kufanya
 mawasiliano
 8. Ukinunua simu hakikisha
 unasoma kama ina LOW SAR
 (Specific Absorbtion Rate) Ni
 kipimo cha kupokea mionzi ya
 simu.Za nokia zinazo ila za
 Kichina HAZINA.
 9. Tumia vifaa vya kupunguza
 Mionzi vinapatikana madukani
 (vinawakawaka taa hivi)
 10.Weka simu atleast 3.4 inches kutoka kwenye sikio
 11. Jitahidi kutumia Earphones muda
 wote unapotumia simu
 12. Tumia speaker phone."Loudspeaker "
 13. Text zaidi kuliko kupiga simu .
 14. Jitahidi usitumie muda mwingi
 kwenye simu kama umeiweka kwenye
 sikio
 15. Jitahid kuiweka mbali na reproduction
 organs zako hasa kwa wanaume
 ambao hatujapata watoto.
 16. La mwisho kula vizuri ilikuongeza
 Via

picha ya siku

picha ya siku
Maajabu

Friday, October 26, 2012

DIAMOND ADAI KUOA NI BAADAYE SANA

 
 
Msanii wa Bongo fleva, Naseeb Abdul, a.k.a Diamond wa wasafi siku za hivi karibuni alifunguka na kusema kwamba hana mpango wa kuoa siku za karibuni kwa kuwa bado anahitaji sana mapenzi ya karibu na mama yake.
Akihojiwa na vyombo vya habari hapa Tzee, Diamond alisema kumekuwa na maneno mengi sana yanayozagaa kuwa hivi karibuni atamuanika mchumba wake anayetaka kufunga naye ndoa, jambo ambalo si la kweli.
Diamond, ambaye unaweza kusema ndiye mwanamuziki anayefunika kwa sasa katika miondoko ya Bongo fleva, kutokana na ngoma zake kupendwa na mashabiki wengi hapa Tzee hata nje ya Tzee, alisema kwamba mbali na kuhitaji mapenzi kwa mama yake, pia ushauri wake ni jambo la muhimu katika kila jambo analotaka kulifanya.
“Unajua mimi ninampenda sana mama yangu na ndiye kila kitu kwangu, hivyo najikuta hakuna kitu ninachoweza kufanya bila kumjulisha, hivyo kuwa naye mbali kwa sasa itakuwa ngumu,” alisema.
Akizungumzia kuhusu uhusiano wake na aliyewahi kuwa na mahusiano na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, alisema kwa sasa ni rafiki yake wa kawaida tu, si mpenzi na wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali.
Kwa mujibu wa Diamond, matatizo yote yaliyotokea huko nyuma, wameshasameheana na sasa hivi wanaiva vilivyo.
Diamond na Wema walishawahi kuwa wapenzi na kujikuta wakimwagana mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo habari zao ziliteka vyombo mbalimbali vya habari, hasa pale mwanamuziki huyo alipofanya onesho lake Mlimani City na kuzikataa fedha alizokuwa akipewa na mwanadada huyo.Lakini kwasasa Diamond anatuhumiwa kwamba anamahusiano na mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Najma sema msanii aliendelea tu kusema kwamba Najma si mpenzi wake ila ni rafiki tu Duuuuhh!!!!! baada ya hayo ndipo akaamua kusma kwamba suala la kuoa sio wakati huu ni baadaye sanaa .

STUDIO ANAYOREKODIA NEY WA MITEGO YAPINGWA ZENGWE

 
tiiiiiiili tili ntiliti, siiiiri imefichuka...inasemekana baada ya kutoa ngoma kadhaa ya kuwaponda watu kwa kuwaambia ukweli ulio na maneno makali kiaina, studio anayorekodia Ney wa mitego inayoitwa Shyne Rcords imeandikiwa barua na Basata ya onyo na kupewa siku tano kuonana na basata huku ikituhumiwa kutengeneza ngoma zenye kutukana watu

Mnager wa studio hiyo amesema kuwa michongo hiyo yote itakua imefanywa na maadui wakubwa wa Ney kwenye ngoma zake ambao ni wasanii wa Bongo Movie wametia ndio wamesababisha yote hayo na kuwatuhumu kwa matunguli " yaani sasa hivi unakuta mauza uza tu mara mixer inazima mara amplifaya bila sababu yoyote ila watashindwa tu kwa jina la Yesu." amesema manager huyo..
zaidi msikilize Gossip Cop hapo chini

DIDDY APATA AJALI

 
Mitandao kadhaa ukiwemo wa TMZ imeripoti kutokea kwa ajali ya gari ikimhusisha Bad Boy Diddy maeneo ya Bevery Hills
 
maaskari waliofika eneo la tukio walisema kuwa kila mmoja aliehusika katika ajali alionekana kulalamika kuumia akiwemo Diddy, dereva wake na dereva wa gari lingine, na kudai kuwa bado haijajulikana wameumia kiasi gani lakini hakuna hata mmoja aliepelekwa hospitali licha ya ambulance kufika eneo la tukio

BLOG YENU YA JAMII YA WATAKIA SIKUKUUB NJEMA YA IDD AL HAJJ

BLOG YENU YA JAMII YA WATAKIA SIKUKUUB NJEMA YA IDD AL HAJJ

WTF: NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATANGAZA TANZANIA NI MUUNGANIKO WA VISIWA VYA PEMBA NA ZIMBABWE

 WTF: NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATANGAZA TANZANIA NI MUUNGANIKO WA VISIWA VYA PEMBA NA ZIMBABWE
 
HUYU NDIO NAIBU WAZIRI WETU WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TANZANIA
 
HON: PHILIPO AGUSTINO MULUGO AMBAE AMETANGAZA HUKO SOUTH AFRICA KUWA TANZANIA ILIANZISHWA MWAKA 11964 IKIUNGANISHWA NA VISIWA VYA ZIMBABWE NA PEMBA....LAKINI UKIANGALIA VIZURI SCRIPT ANAYOISOMA INAYOONYESHWA PEMBENEI MKONO WA KUSHOTO INAONYESHA KUANDIKWA ZANZIBAR NA SIO ZIMBABWE NA IMEANDIKWA 1964 NA SIO 11964 KAMA ALIVYOITAMKA........................HAPA NANI WA KULAUMIWA????????/ TATIZO LIKO WAPI??????

Monday, October 22, 2012

HIZI PICHA NDIO KABISA ZIMEWAPA WATU USHAHIDI KWAMBA CHRIS BROWN NA RIHANNA WAMERUDIANA.

HIZI PICHA  NDIO KABISA ZIMEWAPA WATU USHAHIDI KWAMBA CHRIS BROWN NA RIHANNA WAMERUDIANA.

Hii ilikua ni kwenye party ya uzinduzi wa brand new channel ya Chris Brown on Qubeey, a software site kwa ajili ya mashabiki wa Chris ambapo watu kadhaa walialikwa na kupita kwenye redcarpet lakini Rihanna hakupita redcarpet alafu baadae akaonekana ndani V.I.P akiwa karibu na CB pamoja na kukiss pia….. hii imewafanya wengi waamini kwamba wapenzi hawa wa zamani wamerudiana.

Wednesday, October 17, 2012

HAWA NDIO WAUAJI WA WALE WANACHUO WANNE NIGERIA, WALIWACHOMA MOTO KWA TUHUMA ZA WIZI WAKATI SIO KWELI.

HAWA NDIO WAUAJI WA WALE WANACHUO WANNE NIGERIA, WALIWACHOMA MOTO KWA TUHUMA ZA WIZI WAKATI SIO KWELI.
Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.

Ni wiki mbili zimepita lakini hii taarifa bado inaongoza kwenye headlines za Nigeria, ni kuhusu wanachuo wanne ambao walipigwa, waliteswa, walitembezwa uchi barabarani na baadae kuchomwa moto hadharani wakidaiwa kuwa ni wezi.

Imefahamika ni watuhumiwa 13 akiwemo chief wa hicho kijiji cha Aluu ambae alihusika pia kuwachoma moto hao wanachuo.

Watuhumiwa hao wamesema kulikua na askari polisi mmoja ambae aliwaaambia wawachome moto hao wanachuo wakati huohuo kulikua na askari mwingine aliesema wasichomwe moto.

Chanzo cha kuchomwa moto kilitokana na mmoja kati yao kuwaomba wenzake kumsindikiza kwa jamaa mmoja aliekua akimdai hapohapo kijijini lakini kibao kikawageukia baada ya jirani wa mdaiwa kuanza kupiga kelele kwamba wamevamiwa na wezi, vivyo hivyo kwa mdaiwa pia ambae alimuunga mkono jirani kwa kusema kweli wanachuo hao walikua wezi, wananchi wakakusanyika na kuanza kuwapiga.

Kilichopelekea wananchi kutotoa nafasi ya kuwasikiliza wanachuo walipojitetea ni pamoja na mfululizo wa matukio ya uhalifu ambayo yamekua yakitokea kwenye hicho kijiji kwa siku za karibuni kwa wanakijiji mbalimbali kuibiwa.


JK aongoza mkutano wa Wafanyabishara wa Oman na Tanzania jijini Muscat

JK aongoza mkutano wa Wafanyabishara wa Oman na Tanzania jijini Muscat


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabiashara wa Oman na Tanzania wakati wa mkutano malum wa uwekezaji aliouandaa kwaajili ya kuelezea fursa za uwekezaji nchini.Mkutano huo wa uwekezaji ulofanyika jijini Muscat Oman ulihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe,Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Abdallah Kigoda ,Wziri wa Kazi,Ushirika na Uwezeshaji kiuchumi wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wafanyabishara wa Oman na Tanzania waliohudhuria mkutano maalum wa uwekezaji Tanzania ulifanyika jijini Muscat Oman leo .Mkutano huo wa uwekezaji ulofanyika jijini Muscat Oman ulihudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe,Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Abdallah Kigoda ,Wziri wa Kazi,Ushirika na Uwezeshaji kiuchumi wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene.Pamoja na viongozi waandamizi  wa serikali zote mbili.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na maofika wangazi za juu wa Oman na Tanzania waliohudhuria mkutano maalum wa uwekezaji uliofanyika katika Hoteli ya Al Bustan jijini Muscat Oman leo. Picha na Freddy Maro


WAISLAM WAKASILISHWA KWA KITENDO CHA KUKOJOLEWA KITABU KITAKATIFU CHA ALLAH

WAISLAM WAKASILISHWA KWA KITENDO CHA KUKOJOLEWA KITABU KITAKATIFU CHA ALLAH




ENEO la Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana liligeuka uwanja wa mapambano kati ya makundi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu na polisi baada ya watu hao kuvamia Kituo cha Polisi Kidogo cha Maturubai kilichopo eneo hilo.
Watu hao walivamia kituo hicho wakitaka wakabidhiwe mtoto anayedaiwa kukojolea kitabu kitakatifu cha Quran ili wamwadhibu.
Vurugu hizo zilizoanza tangu saa nne asubuhi, zilisababisha makanisa matano kuchomwa moto, magari kadhaa kuvunjwa vioo na watu hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo... “Siwezi kutaja idadi ya waliokamatwa, lakini kuna watu tunawashikilia kutokana na kufanya fujo, kwa sasa niko katika operesheni, nitazungumza kwa kirefu baadaye.”
Hata hivyo, Misime alisema hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi.
“Pamoja na kwamba bado tupo katika eneo la tukio bado hatujashuhudia vifo wala majeruhi na tunaomba Mungu mambo hayo yasitokee.
Aliyataja makanisa hayo kuwa ni la TAG Kizuiani, Wasabato Kizuiani, TAG la Shimo la Mchanga na KKKT Mbagala Zakheim.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchomaji wa makanisa hayo ni kosa la jinai na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao.
Alisema katika vurugu hizo gari la Mkuu wa Polisi Wilaya ya Temeke (OCD) limevunjwa vioo.
Kamanda Kova alisema Jeshi hilo litaimarisha ulinzi katika makanisa hayo ili kuhakikisha kunakuwa na usalama.
Miongoni mwa magari hayo matano yaliyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo zilisababisha Barabara ya Kilwa kufungwa kwa muda ni gari la Kituo cha Televisheni cha Clouds ambalo lilivunjwa vyoo.
Akizungumzia suala hilo, mkazi wa Mbagala Mission, Nassor Mohamed alisema vurugu hizo zilitokea baada ya mtoto mmoja kukojolea Quran.
Alisema mtoto huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo na ubishi na mtoto mwenzake ambaye wanasoma wote katika Shule ya Sekondari Chamazi.
Mohamed alisema mtoto huyo mwenye miaka 14, alikuwa akibishana na mwenzake mwenye umri kama huo kwamba mtu akikojolea kitabu hicho hugeuka kuwa nyoka.
Alisema kuwa mtoto huyo aliamua kufanya kitendo hicho ili kuona kama atageuka nyoka na wakati akifanya kitendo hicho mzee mmoja alimuona na kumhoji kisha kumpeleka kwa mama yake na kumshtaki.
“Yule mama aliwajibu kuwa kama ni hilo tu, basi awape hela wakanunue kingine. Aliposema hivyo wale watu wakakasirika wakamwambia, sisi tulikuja kukuambia kwa uzuri ili umwadhibu mwanao, lakini kutokana na majibu yako hatukuachii tena huyu mtoto,” alisema.
Alisema baada hapo, watu hao walimpeleka mtoto huyo katika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Chamazi ambako waliandikiwa barua na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo katika eneo hilo.
Jumatano jioni, watu hao walifika katika kituo hicho wakitaka wapewe tena mtoto huyo na ndipo walipoambiwa kuwa amehamishiwa katika Kituo cha Maturubai.
Alisema baada ya kumkosa mtoto huyo walihamasishana na kukubaliana kuwa baada ya kutoka msikitini kesho yake (jana), wakavamie kituo hicho na kumtoa mtoto huyo.
Wakati ghasia hizo zikiendelea, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Temeke, Farid Salehe aliwasihi waumini wa dini hiyo kuwa watulivu.
Katibu wa Vijana wa Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkarim Kulao aliwataka Waislamu waliokuwa wamekusanyika katika eneo la kituo hicho cha polisi kurejea majumbani kwao kwani mtuhumiwa huyo alikuwa ameshahamishwa.
Baadaye Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha baadhi ya watu waliokuwa wamekiendelea kubaki katika eneo hilo.
Askari waliokuwa na mabomu ya machozi walitawala eneo hilo kuweka ulinzi na hatimaye kufanikiwa kuwatawanya watu hao.
Baada ya kutimuliwa katika mkusanyiko huo, kundi moja la watu hao lilifika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mbagala na kulichoma moto.
Mzee wa Kanisa hilo, Siaga Kiboko alisema mali kadhaa zimeharibika na kwamba walishatoa taarifa polisi.



SAMAHANI SANA KWA KUWEKA PICHA HII MBAYA,,ILA KWELI ILIKUWA BAHATI MBAYA KUPIGA PICHA HII KAMA ANAVYOSEMA RECHO AU ILIKUSUDIWA

RECHO ATOA UFAFANUZI JUU YA PICHA HII

SAMAHANI SANA KWA KUWEKA PICHA HII MBAYA,,ILA KWELI ILIKUWA BAHATI MBAYA KUPIGA PICHA HII KAMA ANAVYOSEMA RECHO AU ILIKUSUDIWA

RECHO:ni bahati mbaya tu diamond kutushika sisi vile alikua anajiweka sawa tu sema mpiga picha ndo aliwahi kupiga,
Jana kupitia mitandao ya jamii, kulikua na mzunguko wa picha hii kila kona ya mitandao hiyo, huku ikiwaacha mashabiki kujiuliza maswali mengi na wengine kudai kuwa inawezekana kuna watu tu wameamua ku edit picha kwa madhumuni ya kuwachafu wasanii hawao ambae ni Lina kushoto, Recho kulia na Diamond.
kupitia simu tumefanikiwa kumpata Recho ambae yupo mkoani Iringa kwa ajili ya show ya leo na haya ndio aliyoyasema.

"hiyo picha ni hali tu ya kawaida, na wala hatukua peke yetu tulikuwa na wasanii wenzetu na presenter wengine tulikuwa tunaogelea,na tulikua tunapiga picha ndio, so ni bahati mbaya tu diamond kutushika sisi vile alikua anajiweka sawa tu sema mpiga picha ndo aliwahi kupiga, bahati mbaya tu ndio mtu akaziweka kwenye bbm ndio ikafika huko.
 tulikua sehem to have fan tu, tunaogelea so nikitu ambacho hata mwenyewe sijakipenda kwasababu si tumefanya vile kwa sababu yetu wenyewe ila mwingine anachukua na kuanza kusambaza sio vizuri

NAY WA MITEGO FT CHIBWAY"WAMENICHOKOZA"

 NAY WA MITEGO FT CHIBWAY"WAMENICHOKOZA"

Najua kuna ile time utakuwa unajiuliza daaah!!!! hivi Nay wa mitego kwanini anapenda sana kuponda wasanii wenzake katika ngoma zake.Sasa basi Nay alifunguka na kusema kwamba sio kama anaponda wasanii wenzake ila nyimbo zake zinasema ukweli na uwazi jinsi wasanii wa hapa Tzee wanavyojihusisha na vitu ambavyo sio vizuri katika jamii.Baada ya kutoa sababu hiyo msanii huyu alifunguka na kusema kwamba amefanya ngoma mpya ambayo hiyo sasa ndiyo amewaka uwazi na ukweli na jina la ngoma ni "Wamenichokoza"ebu fanya kama una click hapo chini uone jinsi alivyofanya yake dzain ametisha daaaahh!!!!! ni nomaaa.

Artist; Nay wa mitego ft chibwa
Song; wamenichokoza
Studio; shine record
Prod; mr T touchez

Tuesday, October 16, 2012

DK. NDUGULILE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA HUKO MBAGALA

DK. NDUGULILE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA HUKO MBAGALA

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugulile akisalimiana na Makamu Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies Of Gog Askofu Magnus Muiche wakati alipokwenda kutembelea pamoja na kutoa pole kwa Makanisa yaliyoharibiwa na Mgogoro wa Kidini ambapo Mbunge alibaini Makanisa kumi yaliyoharibiwa na Sakata hilo ambapo aliweza kutembelea makanisa yote kumi.



Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani Mtaa wa Mbagala Mch, Frank Kimambo akimwenyesha Mh Mbunge baadhi ya Sehemu iliyoharibiwa katika Kanisa hilo ambapo alisema kuwa Ofisi yake ilichomewa kila kiti na hawakuweza kuokoa kitu chochote, na kuongeza kuwa sehemu nyingine iliyoharibiwa ni Madhabau.

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk Faustine Ndugulile (kulia) akiangalia gari liliochomwa katika hekaheka hizo.

Kinanda cha Kanisa la KKKT kilichoharibiwa.


Thursday, October 11, 2012

LINEX AKANUSHA KUMMWAGA DEM WAKE WA KIZUNGU

LINEX AKANUSHA KUMMWAGA DEM WAKE WA KIZUNGU


Baada ya gazeti moja la udaku kumwaga wino na kudai kuwa msanii Linex amemmwaga dem wake wa kizungu na kumtambulisha mpya kwenye viwanja vya Liders siku ya fiesta, Linex amekanusha madai hayo kwa nguvu zote

"mwenyewe nashanagaa kuona hii story kwenye blog na magazeti lakini sijui imetoka wapi, mimi mwenyewe nakanusha sijaachana nae, niko nae na tuko fresh, na next month kama mishe itapungua nitaenda Finland na nitarudi nae, ila sitaki kuzungumza kuwa nini kitafata kwasababu ni mapema sana, basi kama ndio hivyo tutashindwa hata kukaa na madada zetu sehem za starehe ...,hivo yani"


BE UPDATED


Kwa habari za kijanja kutoka kwenye SIASA,MUSIC,FILAMU,FASHION,UDAKU ndani na nje ya Tanzania usikose kutembelea blog yako daily ili uzidi kuwa mjanja,na pia usisahau kuacha comment,,"KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI

kichekesho cha leo


Wizi mtupuuuuuuuuuu!

 Girl: Hellow

 Boy: Sweety mambo vip?

 Girl: poa

 Boy: Utakua free weekend hii? Nilikua nataka uje home.

 Girl: Ooh Sorry, sitoweza kuja coz kuna harusi ya Aunt yangu na kesho yake kutakua na wageni nyumbani.

 Boy: kama ni hivo sawa just nilikua nataka nikufanyie surprise, nimekununulia Blackberry Torch

 Girl: ooh!! Usijali mpenz wangu ntakuja, hata ukitaka nilale uko uko nitalala

 Boy: vipi kuhusu harusi??

 Girl: harusi ipi?? Nilikua nakutani honey.

 Boy: ok, na mimi pia nilikua nakutania tu.....

KAULI YA PROFESA J KUHUSU KILICHOMPELEKA CANADA NA KUKUTANA NA J.K

KAULI YA PROFESA J KUHUSU KILICHOMPELEKA CANADA NA KUKUTANA NA J.K

Staa wa hit single ya ‘Kamiligado’ Profesa Jay ambae alishindwa kuperform kwenye Fiesta 2012 kama ilivyopangwa, amesema sababu ni mwaliko aliopewa wa kupeform nchini Canada.

Namkariri akisema “tulialikwa mimi na Mzee Yusuf kuperform na kushiriki katika mkutano wa Diaspora huku Canada unaohusisha wafanyabiashara wa Tanzania na nje ya Tanzania ili kuja kuwekeza na kuikwamua Tanzania kiuchumi ambapo mkutano huu ulifunguliwa na rais Mtukufu Jakaya Kikwete na wadau wengi na viongozi wengi, mabalozi na watu wengine walihusika”


Kwenye line nyingine Prof ambae single yake ya mwisho kuitoa inaitwa ‘Hallow’ kasema waliohudhuria sio walio Canada peke yake, hata kutoka Marekani na sehemu nyingine walikuepo.

Kuhusu kurudi bongo, J amesema anarudi wekeend hii kwa sababu bondia wake Thomas Macharia anacheza hivyo atarudi kwa ajili ya kuja kumsupport kwa sababu pia yeye Prof ni meneja wa Macharia.

Wednesday, October 10, 2012


Kwa habari za kijanja kutoka kwenye SIASA,MUSIC,FILAMU,FASHION,UDAKU ndani na nje ya Tanzania usikose kutembelea blog yako daily ili uzidi kuwa mjanja,na pia usisahau kuacha comment,,"KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI

TANZANIAN MP ZITTO ZUBERI KABWE MEETS MYSORE CHAMBER OF COMMERCE AND INDUSTRY (MCCI) IN INDIA

TANZANIAN MP ZITTO ZUBERI KABWE MEETS MYSORE CHAMBER OF COMMERCE AND INDUSTRY (MCCI) IN INDIA



MCCI President Sudhakar S. Shetty and other members seen with Tanzanian MP Zitto Zuberi Kabwe during an interaction in  Mysore  City, India,  yesterday.

Mysore, Oct. 10- The Mysore Chamber of Commerce and Industry (MCCI) had organise d an interaction meeting with Zitto Zuberi Kabwe, Member of Parliament of Tanzania yesterday at the Chamber premises.
Interacting with the members, he requested all the business communities to set up industrial enterprises at Tanzania which gives job opportunities to Tanzanian locals as well taxes to the Government and the Indian enterprisers too can expand their business overseas.
The units established under Special Economic Zones are exempted from taxes for 10 years and will get other incentives too, he said adding that they have ample land to set up industrial units, ample natural resources for power generation, for mining in coal and copper and plenty of virgin lands for cultivation of sugar. There is also scope for sugar industries at Tanzania, he said and urged them to invest in these areas. The meeting also discussed about the MoU between MCCI and Tanzanian government for better business. HERE



Tanzania Yachaguliwa Kuwa Mjumbe wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani

Tanzania Yachaguliwa Kuwa Mjumbe wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani



Na Innocent Mungy
Tanzania imechaguliwa tena kuingia katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU), kipindi kingine cha miaka minne baada ya kuwa miongoni mwa nchi 40 kati ya nchi 192 wanachama wa umoja huo.
 Katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa na diplomasia ya hali ya juu, nchi nyingi zilikusudia kuingia kwenye Baraza hilo. Tanzania imekuwa moja ya nchi mbili za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda kushinda nafasi hizo. Nchi nyingi e za Africa zilizofanikiwa kuingia katika Baraza hilo ni Burkinafaso, Jamhuri ya Congo Brazaville, Ivory Coast, Misri, Gabon, Malawi, Morocco, Sudan na South Africa.
 Mapema leo asubuhi, Balozi Hussein A. Bishar wa Kenya alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UPU akimshinda mwanamama Serrana Casco kutoka Uruguy. Nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu iliyokuwa na ushindani mkubwa kati ya Mmarekani Denis Delehantty na Mswiss Pascal-Thienry Clivaz ambapo Clivaz alishinda nafasi hiyo
 Pichani juu ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa wakifurahia ushindi wa Tanzania kuchaguliwa katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani leo. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 40 zinazounda Baraza hilo, Kati ya nchi wanachama 192.




TAARIFA HII IKUFIKIE KUHUSU ALIEPIGWA CHINI KWENYE SEKTA YA AFYA TZ.

TAARIFA HII IKUFIKIE KUHUSU ALIEPIGWA CHINI KWENYE SEKTA YA AFYA TZ.
Serikali imemsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa Tanzania Joseph Mgaya pamoja na mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na afisa udhibiti ubora wa MSD kutokana na kuidhinisha matumizi ya dawa bandia ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi(ARV) yenye jina la kibiashara TT-VIR 30 toleo namba OC.O1.85

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Hussein Mwinyi amesema nyaraka zinaonyesha kuwa kiwanda cha Tanzania pharmacetical Industrial Limited kiliiuzia MSD hizo dawa na kuzisambaza lakini walijua ni kinyume cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219.

Dr Mwinyi amesema hizo dawa bandia zilikua na kiambata cha EFAVERENZ badala ya kuwa na viambata aina ya NIVERAPINE, LAMIVUDINE na STAVUDINE.

Kwenye line nyingine Dr Mwinyi ameamplfy kwamba licha ya kusimamisha matumizi ya dawa hizo bandia na kuagiza kuondolewa mara moja kwenye vituo vya afya, serikali pia imesitisha uzalishaji wa dawa zote katika kiwanja cha TPI hadi uchunguzi utakapokamilika.

picha ya leo

Yale yaleeeeeee....barabara ya morogoro road leo





Miyeyusho na Ramadhani kuzichapa Desemba 9 jijini Dar

Miyeyusho na Ramadhani kuzichapa Desemba 9 jijini Dar


Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links, Mohammed Bawazir akiwatambulisha kwa waandishi wa habari mabondia Francis Miyeyusho (kushoto) na Nassib Ramadhani watakaopambana Desemba 9 kwenye Ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam kugombea mkanda wa Ubingwa wa Mabara wa WB Forum, pambano hilo la uzito wa kilo 53.


 Bondia Francis Miyeyusho akisaini mkataba wa kupambana na Nassib Ramadhani (wa pili kulia). Anayeshuhudia kulia ni Mwanasheria Nyasebwa Berious wa Kampuni ya Member Law Attorneys (MLA). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Darworld Links inayoandaa pambano hilo, Mohammed Bawazir.



Headlines kutoka kwenye magazeti ya Udaku na Michezo