JCB AFUNGUKA KUHUSIANA NA HABARI ZINAZOANDIKWA KWENYE MITANDAO
Siku za hivi karibu baada ya kutokea kifo cha Lexa huko Arusha sasa mitandano mbalimbali inasema kwamba JCB amehusika katika kifo hicho lakini yeye mwenyewe anafunguka na kusema kwamba kuna baadhi ya mitandano ya hapa Tzee inapenda sana kuandika habari ambazo sio za kweli kwani yeye ndiye alikuwa ni mtu wa mwisho wa kuongea na Lexa lakini angependa kuwajulisha kwamba yeye sio muhusika katika kifo hicho wahusika wa kifo hicho wapo chini ya Usalama wa Polisi na uchunguzi unaendelea huko Arusha.Hayo ndiyo maneno ya JCB baada ya kufunguka kuhusiana na baadhi ya mitandano kuandika kwamba yeye anahusika katika kifo cha Lexa kilichotokea siku za hivi karibuni huko Arusha.
No comments:
Post a Comment