Wednesday, October 10, 2012

TAARIFA HII IKUFIKIE KUHUSU ALIEPIGWA CHINI KWENYE SEKTA YA AFYA TZ.

TAARIFA HII IKUFIKIE KUHUSU ALIEPIGWA CHINI KWENYE SEKTA YA AFYA TZ.
Serikali imemsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa Tanzania Joseph Mgaya pamoja na mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na afisa udhibiti ubora wa MSD kutokana na kuidhinisha matumizi ya dawa bandia ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi(ARV) yenye jina la kibiashara TT-VIR 30 toleo namba OC.O1.85

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Hussein Mwinyi amesema nyaraka zinaonyesha kuwa kiwanda cha Tanzania pharmacetical Industrial Limited kiliiuzia MSD hizo dawa na kuzisambaza lakini walijua ni kinyume cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219.

Dr Mwinyi amesema hizo dawa bandia zilikua na kiambata cha EFAVERENZ badala ya kuwa na viambata aina ya NIVERAPINE, LAMIVUDINE na STAVUDINE.

Kwenye line nyingine Dr Mwinyi ameamplfy kwamba licha ya kusimamisha matumizi ya dawa hizo bandia na kuagiza kuondolewa mara moja kwenye vituo vya afya, serikali pia imesitisha uzalishaji wa dawa zote katika kiwanja cha TPI hadi uchunguzi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment