Tanzania Yachaguliwa Kuwa Mjumbe wa Baraza la Utawala la
Umoja wa Posta Duniani
Na Innocent Mungy
Katika uchaguzi wenye
ushindani mkubwa na diplomasia ya hali ya juu, nchi nyingi zilikusudia kuingia
kwenye Baraza hilo .
Tanzania imekuwa moja ya
nchi mbili za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda kushinda nafasi hizo. Nchi
nyingi e za Africa zilizofanikiwa kuingia katika Baraza hilo
ni Burkinafaso, Jamhuri ya Congo Brazaville, Ivory
Coast , Misri , Gabon , Malawi ,
Morocco , Sudan na South Africa .
Mapema leo asubuhi,
Balozi Hussein A. Bishar wa Kenya
alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UPU akimshinda mwanamama Serrana Casco
kutoka Uruguy. Nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu iliyokuwa na ushindani mkubwa
kati ya Mmarekani Denis Delehantty na Mswiss Pascal-Thienry Clivaz ambapo
Clivaz alishinda nafasi hiyo
Pichani juu ujumbe wa
Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa
wakifurahia ushindi wa Tanzania
kuchaguliwa katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani leo. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 40 zinazounda
Baraza hilo ,
Kati ya nchi wanachama 192.
No comments:
Post a Comment