Thursday, October 11, 2012

KAULI YA PROFESA J KUHUSU KILICHOMPELEKA CANADA NA KUKUTANA NA J.K

KAULI YA PROFESA J KUHUSU KILICHOMPELEKA CANADA NA KUKUTANA NA J.K

Staa wa hit single ya ‘Kamiligado’ Profesa Jay ambae alishindwa kuperform kwenye Fiesta 2012 kama ilivyopangwa, amesema sababu ni mwaliko aliopewa wa kupeform nchini Canada.

Namkariri akisema “tulialikwa mimi na Mzee Yusuf kuperform na kushiriki katika mkutano wa Diaspora huku Canada unaohusisha wafanyabiashara wa Tanzania na nje ya Tanzania ili kuja kuwekeza na kuikwamua Tanzania kiuchumi ambapo mkutano huu ulifunguliwa na rais Mtukufu Jakaya Kikwete na wadau wengi na viongozi wengi, mabalozi na watu wengine walihusika”


Kwenye line nyingine Prof ambae single yake ya mwisho kuitoa inaitwa ‘Hallow’ kasema waliohudhuria sio walio Canada peke yake, hata kutoka Marekani na sehemu nyingine walikuepo.

Kuhusu kurudi bongo, J amesema anarudi wekeend hii kwa sababu bondia wake Thomas Macharia anacheza hivyo atarudi kwa ajili ya kuja kumsupport kwa sababu pia yeye Prof ni meneja wa Macharia.

No comments:

Post a Comment