Saturday, July 19, 2014
SPIKA ANNE MAKINDA AWASILI ARUSHA, AKAGUA UKUMBI UTAOTUMIKA KATIKA MKUTANO WA 45 WA MABUNGE WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA
Jaja aanza kazi Yanga, afanya balaa mazoezini
Na Sweetbert Lukonge
STRAIKA mpya Yanga, Mbrazili, Genilson Santana Santos ‘Jaja’, tayari ameanza kuonyesha makeke yake baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu katika mazoezi ya timu hiyo yaliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sokondari Loyola, Mabibo, jijini Dar es Salaam, jana.
Jaja, tangu atue hapa nchini Jumanne iliyopita akitokea Brazil, alikuwa hajawahi kufanya mazoezi ya kucheza mpira, siku zote alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia ili kujiweka fiti tayari kwa kuungana na wachezaji wenzake wanaoendelea na programu za kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo kwa ajili ya michuano ya ligi kuu msimu ujao na ile ya kimataifa.
Hata hivyo, katika mazoezi ya jana ambayo Jaja alijumuika na wachezaji wenzake katika kuuchezea mpira ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo, alionyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu.
Katika mazoezi hayo ambayo wachezaji wa timu hiyo walikuwa wakifundishwa na Maximo jinsi ya kufunga pindi wanapokuwa katika eneo la hatari, Jaja alipiga mashuti nane na matano kati ya hayo yalitinga wavuni.
Mashuti matatu alimfunga Juma Kaseja na mawili alimfunga Ally Mustapha ‘Barthez’, jambo ambalo liliwafanya mashabiki wengi waliokuwa wakiangalia mazoezi hayo kumpigia makofi mchezaji huyo.
Mchezaji mwingine aliyefanya vizuri katika mazoezi hayo alikuwa ni Hamis Thabiti ambaye alizifumania nyavu mara sita na kukosa mashuti miwili.

Azam, Mtibwa kunogesha Tamasha la Matumaini
Na Khadija Mngwai
TIMU za Azam FC na Mtibwa Sugar, zinatarajiwa kunogesha Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Agosti 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kushuka dimbani siku hiyo kuonyeshana ubabe.
Tamasha hilo litahusishwa na burudani kibao ikiwa ni pamoja na mechi za Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Simba na Yanga ambao wataonyeshana ubabe kwa kujua nani mkali.
Mwaka jana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alipuliza kipenga kuashiria mtanange huo kuanza kati ya wabunge ambapo safari hii wataonyeshana uwezo wa hali ya juu kufuatia kila upande kutaka kuibuka na ushindi.
Mechi hiyo ya Azam na Mtibwa itaanza mapema kabla ya mechi ya waheshimiwa. Mtanange wa timu hizo za ligi kuu, utachezwa kwa dakika 90 na kutoa fursa kwa timu hizo mbili kuonyesha vikosi vyao vipya kwa ajili ya msimu ujao.

Loga awarudisha Boban, Kisiga Simba
Sweetbert Lukonge na Nassor Gallu
SIMBA ipo katika hatua za mwisho kuwasainisha mikataba mifupi viungo wakongwe nchini, Haruna Moshi ‘Boban’ na Shabani Kisiga ‘Maron’.
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema anataka viungo wawili wazoefu na si wale ambao wanataka kujifunza.Loga, raia wa Croatia, amesisitiza anataka wachezaji wa kazi ambao watamsaidia huku akiwa na wachache ambao wanakuzwa.
“Kutokana na hilo, Simba imeona iwarudishe Boban na Kisiga kwa kuwa wao walikuwa tayari na walipitisha maombi kwa baadhi ya viongozi wa kamati ya usajili.
“Waliwaambia kwamba wanataka kurejea Simba kwa kuwa wanaamini kuna watu ambao watafanya nao kazi vizuri kwa kuwa wako makini,” kilieleza chanzo.
Taarifa zinasema, Boban na Kisiga watapewa mikataba mifupi ya miezi sita ili kuangalia utendaji wao kwanza na iwapo watafanya vizuri, itaongezwa.
Boban aliyekuwa Coastal na Kisiga Mtibwa Sugar, wote waliitumikia Simba kabla ya kuondoka na kuendelea kutafuta maisha kwingine.

Maximo aleta fomesheni nne Yanga
Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, amepanga kuthibitisha kuwa yeye ni bora kwa kutumia mifumo minne katika mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kauli hiyo ameitoa kocha huyo akiwa na wiki tatu tangu aanze kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na ligi na michuano ya kimataifa watakayoshiriki mwakani.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Maximo alisema katika mifumo hiyo atakayoitumia, itategemea na aina ya timu atakayocheza nayo ndani ya uwanja.
Maximo alisema wakati mechi inaendelea, anaweza kubadili mfumo baada ya kuona ule anaoutumia haumpi matokeo mazuri ya ushindi.
Mbrazili huyo aliitaja mifumo atakayoitumia katika mechi zake kuwa ni 4-4-2, 4-3-3, 4-5-1 na 4-3-2-1 ambayo kati ya hiyo itategemeana na timu anayocheza nayo.
“Ni ngumu kutaja mfumo mmoja ninaoutumia katika mechi zangu, kikubwa unachotakiwa kufahamu ni kuwa, mimi nina mifumo ya aina nne na yote huenda nikaitumia katika mechi moja.
“Hiyo inategemeana na aina ya timu ninayocheza nayo, mechi nyingine ni ngumu ambazo zinahitaji kulinda goli lenu na nyingine inayohitaji viungo wengi, hivyo unahitaji kubadili mfumo haraka.
“Mifumo yote hiyo ninawafundisha wachezaji wangu katika mazoezi, lengo ni kuishika na kuitumia wakiwa ndani ya uwanja,” alisema Maximo.
Aidha, kocha huyo anaendelea kukiimarisha kikosi chake ambapo tangu atue kuifundisha Yanga, anaiboresha safu ya ushambuliaji kwa kuwapa mbinu mbalimbali za ufungaji mabao washambuliaji wake.
“Tatizo la ushambuliaji ni kubwa nchini, ndiyo maana tangu nimeanza kuifundisha Yanga, ninawapa washambuliaji wangu mbinu za ufungaji.”
Katika hatua nyingine, Maximo amemtema kiungo mshambuliaji, Reliants Lusajo na beki wa pembeni, Abuu Ubwa kwenye kikosi chake.
Maximo aliwarejesha wachezaji hao ili aangalie viwango vyao baada ya hivi karibuni uongozi wa timu hiyo kutangaza kuwatema pamoja na mwezao Hamis Thabiti aliyebakizwa.
Maximo alisema kuwa amewaondoa nyota hao rasmi katika kikosi chake atakachokitumia kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Maximo alisema, amefikia hatua ya kuwatema wachezaji hao kutokana na kutoridhishwa na viwango vyao katika mazoezi.
Aliongeza kuwa, amemrejesha kiungo Thabiti katika kikosi chake kutokana na kuridhishwa na kiwango chake alichokionyesha kwa muda wa wiki mbili alizompa.
“Ujue nilivyoondoka nchini na kurudi nyumbani kwetu Brazil, niliondoka na faili la wachezaji niliokuwa nawafundisha, kati ya hao alikuwepo Ubwa na Thabiti wakiwa na umri mdogo wanaichezea timu ya taifa ya U20.
“Hivyo nilivyorudi niliwaulizia wachezaji nikaambiwa walisajiliwa na Yanga na kutemwa kabla ya kuwaita kwenye mazoezi yangu kuona viwango vyao kabla ya kuwarejesha, pia nikatajiwa Lusajo kuwa ana umri mdogo ambaye nilimuita naye.”
Wakati huo huo, Maximo amekuja na mpya katika timu hiyo kwa kutaka kila mchezaji kucheza nafasi zaidi ya moja ndani ya uwanja.
Maximo alisema, hataki kikosini kwake amtegemee mchezaji mmoja, hivyo amepanga kuwafundisha wachezaji wake katika mazoezi ili wacheze namba tofauti.
“Ukifuatilia katika mazoezi yangu, utaona ninawafundisha wacheze nafasi zaidi ya moja ndani ya uwanja kwenye mechi zetu.
“Mchezaji kama Twite (Mbuyu) nimemkuta anacheza namba mbili, lakini tangu nimekuja ninamtumia katika mazoezi yangu kucheza kiungo mkabaji, namba mbili na tatu.
“Pia Javu (Hussein), Bahanuzi (Said) na wengine wengi wakiwemo wachezaji wa U20 niliowapandisha katika kikosi cha wakubwa nahakikisha wanacheza nafasi nyingi ili siku ikitokea mmoja akapata majeraha au kadi, basi nitatumia mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake,” alisema Maximo.

MASWALI 10 YA KUJIULIZA KABLA YA KUACHANA(TALAKA)-4
Grisi hufanya chuma kuwa laini, swali hilo nalo ni grisi inayoweza kuulaini moyo wako na fikra zako kisha kukufanya kujirudi na kuutetea uhusiano wako usiende na maji. Tafiti zinaonesha kuwa bila kuangalia aina ya makosa ambayo wapenzi wametendeana, asilimia 90 ya waliojirudi na kila mmoja kujisahihisha, walivuka wakiwa imara.
Ushauri kwako ni kwamba jaribu kujishusha kwenye mgogoro wako na mwenzi wako. Usiangalie nani katenda, kwani muhimu kwako ni penzi lako kuwa endelevu. Ukiona wewe huwezi kujishusha basi hiyo itakujengea tabia ya kujiona bora sana, hata mbele ya safari utakutana na mwingine na mambo yatakuwa yaleyale. Jitazame, jikosoea!
SAPOTI YAKO KWA MPENZI WAKO IPOJE?
Usisahau kujiuliza swali hili! Inawezekana mwenzi wako mnatofautiana kwa sababu humuoneshi sapoti yoyote. Haya maisha yana changamoto nyingi sana, hakuna kitu kizuri kama pale mwenzio anapokuona upo naye bega kwa bega katika kuzikabili na kuzishinda mkiwa pamoja.
Hakuna jambo linaloumiza kama pale ambapo mwenzi wako anakutana na vipindi vigumu lakini kila anapotafuta uwepo wako inakuwa shida. Hakuoni na kumfanya ajihisi yupo peke yake. Wakati wa kuelekea kuachana na mwenzio, unapojiangalia na kugundua hujampa sapoti, jirekebishe.
Si ajabu wewe ukawa karibu na mtu ambaye ana uhasama na mwenzi wako. Jiulize hapo unakuwa unamsaidia mwenzi wako au unamuumiza? Hakuna kosa kubwa ambalo unaweza kulifanya kama la kukubali kuachana na mwenzi wako bila kufanya tathmini ya mchango wako kwake. Je, ni chanya au hasi?
Jiulize hata wewe mwenyewe, ghafla tu umejikuta unagombana na mtu, ukiwa unatarajia kuwa mpenzi wako atakuwa nawe bega kwa bega, inakuwa tofauti kabisa. Mpenzi wako yupo mbali na hata hajishughulishi angalau kukutia moyo au kukupa ushauri unaoweza kukufanya ujione haupo peke yako.
Si hivyo tu, unajikuta mwenzi wako anakuwa karibu na mtu ambaye anakupiga vita.
Kwa hayo mawili, mwenzio kuwa mbali nawe au kuwa karibu na adui, unajisikiaje? Jawabu hilo likuongoze kutambua kuwa naye anapokukosa nyakati ambazo anahitaji kampani yako, ni maumivu makubwa kwake.
Sapoti haipo kwenye mapambano tu, inahusu harakati mbalimbali. Anapokuwa kwenye uhitaji mkubwa, nafasi yako ipoje? Anapokuwa anaumwa, wewe unakuwa wapi? Kuna jambo analitaka sana na endapo atalifanikisha furaha yake itakuwa imekamilika, je, unamsadiaje kufikia hayo malengo?
Kabla hujaachana naye, hakikisha umeangalia maeneo yote na kugundua kwamba sapoti unayompa ni kubwa lakini yeye ameshindikana. Jitahidi kujisahihisha pale unapogundua kuwa hukuwa ukimpa sapoti ya kutosha. Pengine hiyo inaweza kuwa chanzo cha mgogoro, kwa hiyo ukijirudi unaweza kufanya uhusiano wenu uwe imara sana.
MUME WA DIDA ATAJA SIFA ZA MKEWE MTARAJIWA
BAADA ya kuachana na mkewe ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida,’ mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha TV1, Ezden Jumanne ametaja sifa za mwanamke atakayekuja kumuoa kama akitaka kufanya hivyo.
Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar, Ezden alisema kuwa kutokana na kupitia kipindi kigumu cha kuachana na aliyekuwa mkewe amedai kuwa hafikirii kuoa kwa sasa lakini kama akija kuoa tena atamhitaji mwanamke mcha-Mungu, mwenye heshima, asiyemlevi na atakayejitambua kama ni mke wa mtu.
“Sidhani kama nitaoa hivi karibuni, lakini kama nitaoa tena mwanamke ninayemtaka ningependa awe mwenye heshima, anayefuata dini, asiyependa ulevi na atakayejitambua kama mke wa mtu,” alisema Ezden.
AUNTY ATAMANI KUZAA
Mkali wa sinema za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema anatamani iwe leo au kesho apate mtoto kwani umri wake unaruhusu.Akipiga stori mbili-tatu na paparazi wetu, Aunty alisema kuwa anatamani kuwa mama si kwa kufuata mkumbo bali anataka kuwa mama kwani sasa ni muda muafaka kwake.
“Natamani kwelikweli na mimi siku moja niwe mama wa mtoto sema tu sijabahatika kupata ila naendelea kumuomba Mungu ili ndoto zangu ziweze kutimia,” alisema Aunty Ezekiel.
UCHAWI KABURINI KWA RECHO
AMA kweli duniani imani imekwisha! Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo, Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
Baada ya mpashaji huyo naye kushuhudia mauzauza hayo alipiga simu kwenye Ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa na kupokelewa na kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambapo alimweleza mkuu wa zamu hali ilivyo juu ya kaburi hilo.
toa habari: “Jamani hapo ni Global?”
OFM: “Ndiyo. Tukusaidie?”
Mtoa habari: “Kama mnaweza, njooni kwenye Makaburi ya Kinondoni haraka sana. Juu ya kaburi la Recho kumewekwa vitu kama vya ushirikina.”
OFM: “Tupe dakika sifuri tu.”
OFM WATINGA NA PIKIPIKI
Kama kawaida mkuu wa zamu aliwatuma mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walikwenda mpaka eneo la tukio na kukuta vitu hivyo ambavyo ni tunguri moja iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja (huenda likawa viza) na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
WALINZI WATAFUTWA
Baada ya kujionea vitu hivyo, mapaparazi wetu walikwenda kuwauliza walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:
“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa aliwaona walioviweka. Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo kaburi.”
NDUGU WA MAREHEMU WENGINE
Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini watu waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye alikataa kutaja jina lake.
Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema havina tena mamlaka ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.
BABU ASEMA NI NDUMBA
Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu kuivuta nyota ya marehemu.
Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao walichelewa kwani kwa kawaida kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada ya mwili wa marehemu kuzikwa.
“Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.
SAGUDA WA RECHO SASA
Baada ya hapo, mapaparazi wetu walimsaka aliyekuwa mchumba wa marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina.
Saguda akaenda mbele zaidi kwa kusema: ”Nitakwenda kukutana na walinzi wa makaburi wanieleze kinagaubaga kulikoni kaburi la mchumba angu kuchezewa hivyo.”
ODAMA: SIKWENDA NJE KUJIUZA
Leo tunamalizia makala haya kwa kutazama majibu ya maswali mbalimbali ambayo nilimuuliza na kuyatolea ufafanuzi. UNGANA NAYE…
Mwandishi: Wasanii mnatajwa sana kwenye masuala ya ushirikina ili mng’ae kisanii, kwa nini msimtegemee Mungu?
Odama: Uchawi upo, huwezi kuukwepa lakini inategemea na mtu anaundekeza kiasi gani. Binafsi siamini katika hayo mambo. Namtegemea Mungu zaidi.
Mwandishi: Malengo yenu kama kampuni ni nini katika gemu la filamu za Kibongo?
Odama: Kama kampuni malengo yetu makubwa ni kuvuka mipaka ya Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya Wanigeria ambao wanaonekana kututangulia kimaendeleo.
Mwandishi: Kila mtu kwenye sanaa huwa anakuwa na mtu aliyemvutia hadi kuingia, kwa upande wako, ni nani alikufanya uingie kwenye sanaa?
Odama: Msanii ambaye alikuwa akinivutia kabla sijaanza uigizaji ni Monalisa (Yvonne-Chery Ngatwika). Uhalisia wake katika uigizaji ndiyo kitu kilichokuwa kikinivutia kwake ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye sanaa.
Mwandishi: Wasanii wengi mnatajwa kuwa mnakwenda nchi za nje kujiuza, hili unalizungumziaje?
Odama: Kila mtu ana uhuru wa kusema kile anachojisikia lakini kwa upande wangu sina ‘comment’ (maoni) kwa sababu mimi huwa nikienda nje ya nchi nafuata ishu maalum.
Mwandishi: Ishu maalum ndiyo ipi maana hata wewe uliwahi kutajwa katika sakata hili.
Odama: Weee, uniache kabisa. Mimi mara nyingi nakwenda kwa kazi maalum. Kwa mfano safari yangu ya mwisho kwenda (China) nilifuata vifaa vya ofisi kama kamera na vitu vingine.
Mwandishi: Tunafahamu huna muda mrefu tangu ujifungue, lini sasa utaanza kuingia mzigoni au utabaki kama mkurugenzi na hutaigiza tena?
Odama: Hobi yangu ni kuigiza, siwezi kuacha fani hii kwa sababu naipenda. Nasubiri tu mtoto atimize miezi mitatu, nitaanza kazi kama kawaida. Sasa hivi ana miezi miwili.
Mwandishi: Naona umekuwa bongenyanya, huoni kama inaweza kukuharibia ukapoteza mvuto wa kimwonekano utakapoanza kuigiza?
Mwandishi: Kwa nini usianze sasa mazoezi, huoni kadiri muda unavyozidi kwenda na wewe unazidi kunenepa?
Odama: Siwezi kuanza mazoezi kwa sasa kwa sababu nilijifungua kwa oparesheni hivyo lazima nikae kama miezi sita hivi ndiyo nipige mazoezi ya nguvu kuepuka kufumua mshono bure.
Mwandishi: Wasanii kwa sasa mna makundi katika mitandao ya kijamii, utakuta timu flani imemdiss flani, hivi unaona kuna umuhimu wowote kwa msanii kuwa na hizo timu?
Odama: Mimi sioni ubaya wa kuwa na hizi timu kwa sababu zinamfanya msanii azungumze kwa ukaribu na mashabiki wake ila tatizo linakuja kwa wale ambao wanazitumia kwa kurushiana matusi, hapo ndipo tatizo linapokuja. Tukizitumia vizuri, hazina madhara.
Mwandishi: Katika maisha yako ya sanaa, ulishawahi kukwazwa na jambo au msanii mwenzako ukateseka kila wakati.
Odama: Huwa napenda kufurahi na kusahau kila wakati, siwezi kukaa na dukuduku moyoni hivyo kama yalitokea nimeshayasahau. Sikumbuki.
Mwandishi: Msanii gani wa kiume anakuvutia jinsi anavyoigiza kwa sasa?
Odama: Walikuwepo wengi huko nyuma ila kama ulivyosema kwa sasa namkubali zaidi Gabo, ni msanii mzuri sana sema kama watu wengi hawajamshtukia.
Mwandishi: Mashabiki wako wangependa kumjua baba wa mtoto huyo na pengine mna mipango gani?
Odama: Mtoto wangu anaitwa Jason kuhusu baba yake watamjua siku si nyingi, wasikonde! Mipango inakuja wakae mkao wa kula.Mwandishi: Asante kwa ushirikiano wako tangu mwanzo hadi mwisho.
Odama: Karibu sana, nawapenda wote.
WEMA AMLIPUA KAJALA, KISA UNAFIKI!
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.
TAMASHA LA MATUMAINI 2014: WABUNGE KUTWANGANA ‘LIVE’
Miongoni mwa matukio hayo ni ndondi za waheshimiwa wabunge ambapo mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala atakazichapa ‘kavukavu’ na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mratibu wa tamasha hilo lenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya sekondari nchini, Luqman Maloto alitaja burudani kibao zitakazolipamba tamasha hilo ikiwemo mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na wenzao wa Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie.
Yemi alade wa Nigeria kulitikisa jukwaa
Maloto alisema kwa upande wa burudani ya muziki, atadondoka mkali kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade ambaye ameahidi kumtafuta Johnny wake katikati ya maelfu ya mashabiki watakaojitokeza uwanjani siku hiyo.
Hapatoshi kwenye soka
Kama hiyo haitoshi, Maloto alisema katika upande wa mpira wa miguu, mwaka jana kwenye tamasha hilo mechi kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva, Bongo Fleva waliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 safari hii mambo yatakuwaje?
“Tayari Bongo Movie wameshataja kikosi kamili kitakachoongozwa na kipa wao mahiri Mzee Majuto ‘King’ huku wakiwa kambini chini ya kamati ya ufundi inayoongozwa na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ wakiahidi kuwateketeza kabisa Bongo Fleva,” alisema Maloto.
Kwenye kipengele cha ndondi, Maloto alisema pia kutakuwa na kipute kikali kati ya bondia anayeshikilia mkanda wa UBO (Universal Boxing Organization), Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’ atakayezipiga na mpinzani wake wa siku nyingi, Mada Maugo ‘Mbunge Mtarajiwa’ huku mwanamuziki Khalid Chokoraa akipimana ubavu na Said Memba, Jacob Steven ‘JB’ atamaliza ubishi unaoendelea kwa sasa kwa kuchapana na Cloud 112 pambano hilo likiwa na raundi nne tu.
Maloto alisema, burudani haitaishia hapo, anga la muziki litashambuliwa na Ally Saleh ‘Ali Kiba’ ambapo atapanda jukwaani na kupiga nyimbo zake zote kali sambamba na kutoa sapraizi ya ukimya wake kwa mara ya kwanza.
Mastaa wengine watakaopokezana kipaza sauti ni pamoja na Meninah, R.O.M.A Mkatoliki, Madee, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Wema Sepetu ambaye ataimba nyimbo za bebi wake ‘Diamond’ pamoja na wengine kibao.
“Listi ya waburudishaji ni ndefu, wasomaji waendelee kufuatilia magazeti ya Global Publishers watajuzwa kadri siku zinavyosogea,” alisema Maloto.
TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LIVE: YEMI ALADE, SHILOLE KUONYESHANA KAZI AGOSTI 8, 2014
ZIARA YA RAIS KUFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKUZO, SONGEA
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za
makazi Mkuzo na kukaribishwa na wenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe (mwenye tisheti ya
pundamilia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la tukio ambako alizindua mradi huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe
la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani
Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia),
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za
mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la
Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya
Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili
kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na
mafunzo . Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka na
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za
kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya
zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi
vya vijana kuendelea na mafunzo .
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza
katika hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe
Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia
tukio hilo.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo
aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma
zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga
miji vizuri na kuboresha madhari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
Msafara
wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo
wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa
Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine
zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF,
LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo
hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na
zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa
nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya "Nyumba
yangu, Maisha yangu" ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14.
Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi
ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa
zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT
lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea
ukubwa wa nyumba - kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais
Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18
zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za
msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za
shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa
watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za
miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo
kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho
ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina
mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za
vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje
na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na
mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.
Subscribe to:
Posts (Atom)