Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za
makazi Mkuzo na kukaribishwa na wenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe (mwenye tisheti ya
pundamilia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la tukio ambako alizindua mradi huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe
la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani
Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia),
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za
mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la
Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya
Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili
kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na
mafunzo . Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka na
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za
kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya
zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi
vya vijana kuendelea na mafunzo .
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza
katika hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe
Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia
tukio hilo.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo
aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma
zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga
miji vizuri na kuboresha madhari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
Msafara
wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo
wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa
Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine
zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF,
LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo
hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na
zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa
nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya "Nyumba
yangu, Maisha yangu" ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14.
Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi
ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa
zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT
lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea
ukubwa wa nyumba - kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais
Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18
zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za
msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za
shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa
watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za
miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo
kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho
ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina
mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za
vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje
na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na
mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.
No comments:
Post a Comment