Sweetbert Lukonge na Nassor Gallu
SIMBA ipo
katika hatua za mwisho kuwasainisha mikataba mifupi viungo wakongwe
nchini, Haruna Moshi ‘Boban’ na Shabani Kisiga ‘Maron’.
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema anataka viungo wawili
wazoefu na si wale ambao wanataka kujifunza.Loga, raia wa Croatia,
amesisitiza anataka wachezaji wa kazi ambao watamsaidia huku akiwa na
wachache ambao wanakuzwa.
“Kutokana na hilo, Simba imeona iwarudishe Boban na Kisiga kwa kuwa
wao walikuwa tayari na walipitisha maombi kwa baadhi ya viongozi wa
kamati ya usajili.
“Waliwaambia kwamba wanataka kurejea Simba kwa
kuwa wanaamini kuna watu ambao watafanya nao kazi vizuri kwa kuwa wako
makini,” kilieleza chanzo.
Taarifa zinasema, Boban na Kisiga watapewa mikataba mifupi ya miezi
sita ili kuangalia utendaji wao kwanza na iwapo watafanya vizuri,
itaongezwa.
Boban aliyekuwa Coastal na Kisiga Mtibwa Sugar, wote waliitumikia Simba kabla ya kuondoka na kuendelea kutafuta maisha kwingine.
No comments:
Post a Comment