Na Khadija Mngwai
TIMU za Azam
FC na Mtibwa Sugar, zinatarajiwa kunogesha Tamasha la Usiku wa Matumaini
litakalofanyika Agosti 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kushuka
dimbani siku hiyo kuonyeshana ubabe.
Tamasha hilo litahusishwa na burudani kibao ikiwa ni pamoja na mechi
za Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Simba na
Yanga ambao wataonyeshana ubabe kwa kujua nani mkali.
Mwaka jana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alipuliza kipenga kuashiria
mtanange huo kuanza kati ya wabunge ambapo safari hii wataonyeshana
uwezo wa hali ya juu kufuatia kila upande kutaka kuibuka na ushindi.
Mechi hiyo ya Azam na Mtibwa itaanza mapema kabla ya mechi ya
waheshimiwa. Mtanange wa timu hizo za ligi kuu, utachezwa kwa dakika 90
na kutoa fursa kwa timu hizo mbili kuonyesha vikosi vyao vipya kwa ajili
ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment