SPIKA ANNE MAKINDA AWASILI ARUSHA, AKAGUA UKUMBI UTAOTUMIKA KATIKA MKUTANO WA 45 WA MABUNGE WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA
Spika
wa Bunge, Mhe Anne Makinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe
Magese Mulongo (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Arusha, jana tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 45 wa Mabunge wa Nchi
wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika utakaoanza
tarehe 20 hadi 27 Julai Mjini Arusha .
Spika
wa Bunge, Mhe Anne Makinda akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Habari,
Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka alipokwenda
kukaguwa Ukumbi wa Ngurudoto, Arusha , jana, patakapofanyika Mkutano wa
45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara
la Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa kongamano hilo.
Spika
wa Bunge, Mhe Anne Makinda akitowa maelekezo kwa kamati ya maandalizi
ya Mkutano wa 45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa
Kanda ya Bara la Afrika alipotembelea Ukumbi wa Ngurudoto, mkoani
Arusha patakapofanyika kongamano hilo ambapo Tanzania ndio mwenyeji
No comments:
Post a Comment