Saturday, February 1, 2014

USALITI HAUNA NGUVU, SHETANI WA USALITI NI AKILI ILIYOKOSA MALENGO-10

Tunaendelea na mada yetu ambayo tumeianza wiki kadhaa zilizopita, inahusu fundisho la usaliti. Endelea...
Sikumtaka mume wangu wala Paul, wote niliwaona wana matatizo, yaani hawajakamilika. Saa 4 usiku ndiyo nilikwenda kulala.
“Niliamka saa 3 asubuhi, muda huo mume wangu alikuwa ameshakwenda kazini. Mtoto wangu mkubwa naye alishakwenda shuleni, maana huondoka asubuhi pamoja na baba take. Nilikwenda chumba cha watoto na kumkuta mtoto wangu akiwa bado kalala, kama kuhakikisha nilikwenda chumbani kwa Paul nikamkuta amekaa kitandani kwake anasoma kitabu cha mapenzi.
“Baada ya salamu, nilimuuliza sababu ya kutokwenda kazini mpaka muda huo, akanijibu alikuwa ananisubiri mimi niamke. Aliniambia asingeweza kufanya kazi zake ipasavyo kama hatatimiza lengo la kucheza ‘kikwetukwetu’ faragha na mimi. Nilicheka, kisha nikamuuliza kama anaweza.
“Akaniambia anaweza. Kusema ule ukweli pale nilikuwa nimeshamuona Paul kama mgonjwa asiye na jeuri yoyote kitandani. Nilicheka kama kumsanifu halafu nikaenda bafuni kuoga. Nilimuamsha mtoto wangu, nikamuogesha halafu nikampa chai anywe, alipomaliza kunywa chai nilimpeleka kwa mama mdogo.
“Nilirudi nyumbani nikiwa najiuliza mengi lakini kubwa ni kama Paul ataweza. Nilijua ni mbovu tu, anayetaka kunichezea lakini nilimpa nafasi ya mwisho, ndiyo maana nilihakikisha pale nyumbani tunakuwa wawili tu ili akishindwa asiwe na kisingizio kingine.
“Nilipofika nyumbani nilifunga mlango mkubwa, nikaenda moja kwa moja chumbani kwa Paul. Nilimkuta amelala anasoma kitabu, nilikaa jirani yake, nilimwambia awe na uhakika kama ataweza, siyo nasaula halafu hakitokei chochote.
“Kweli ni aibu, maana mimi kwa umri namzidi Paul miaka sita, ukichangia na umbile langu, halafu nisaule nguo zote naye anione kama nilivyozaliwa nikiwa na matarajio ya kupata penzi ambalo silipati, ni aibu iliyoje? Paul alionekana kujiamini sana, akanihakikishia kwamba hataniangusha.
“Paul aliachana na kitabu chake, akanifuata pale nilipokaa. Nilikuwa nimevaa kanga na blauzi, kwa ndani ni kufuli kama kawaida, juu ni ‘brazia’. Alinitoa kanga nilimkubalia, vilevile kabati langu aliliondoa, alipotaka kuhusika na blauzi nilimgomea, nilimwambia ingewezekana vilevile.
“Kiukweli nilikuwa simuamini ndiyo maana sikutaka aguse blauzi yangu. Siku hiyo sikuwa mfuatiliaji sana kwa sababu nilihofia kwamba atashindwa. Mwanzoni kama alihangaika, yaani gari lake lilianza kuleta mgogoro kwenye kuwaka lakini baadaye stata ilikubali, mambo yakawa safi kabisa.
“Ni dereva mzuri, anaendesha vizuri gari lake, nilimkubali. Nilimuuliza mbona usiku alishindwa, akanijibu hata yeye anashangaa. Ubora wake anaposhika usukani, ndiyo uliofanya nisichoshwe naye, ilipoisha safari moja, iliendelea nyingine. Paul alinifikisha nilipotaka, alinikata kiu yote.
“Kuanzia siku hiyo nilichanganyikiwa kabisa kwa Paul. Nikawa namdharau mume wangu, kwani hata alipotaka huduma chumbani sikumpa. Mume wangu aliposafiri nililala na Paul. Hatukujali matumizi ya kinga wala kujali mzunguko wa siku, basi ikawa napata mimba natoa.
“Penzi la Paul lilinitia wazimu, kila alichoniambia nilikisikiliza bila kuhoji. Neno lake likawa sheria. Tukadanganyana tutaoana, nami nikavimba kichwa. Mgogoro na mume wangu ukawa mkubwa, kila siku vikao kwa wazazi, nikawa nasisitiza nipewe talaka.
“Nilipoona anakuwa mgumu kunipa talaka, ikabidi nimwambie kwamba nina uhusiano na Paul, nilifanya vile achukie anipe talaka yangu. Kumbe nikawa nimechokoza moto, ulitokea ugomvi mkubwa kati ya mume wangu na Paul, waligombana mpaka kufikishana polisi.
“Huwezi kuamini, pamoja na ugomvi huo lakini hatukuacha. Mimi na Paul tuliendelea na mapenzi yetu. Hata nilipogombana na mume wangu, nami kurudi kwetu, niliwasiliana na Paul akiwa nyumbani, nami nilikwenda, tukajifungia chumbani kwake na kufanya ya kwetu. Tulipomaliza nilirudi kwetu, yaani kwa mama mdogo.
“Baada ya wazazi kuona mgogoro ni mkubwa ndani ya ndoa, huku ikiwa wazi kwamba tatizo ni Paul, waliamua kunisafirisha kwenda kwa shangazi yangu Dodoma ili nikae huko, angalau niwe mbali na Paul. Hiyo safari ndiyo iliyonisaidia kujitambua.
“Nikiwa Dodoma, kwanza hisia zangu kwa Paul zikapungua, halafu nikaja kusikia sifa zake za kubadili wanawake kama nguo, halafu analala nao chumbani kwake, niliona amenidhalilisha sana. Nikaanza kukumbuka mazuri ya mume wangu, nikajuta kwa kila kitu.
“Uzuri ni kuwa mume wangu hakunipa talaka, kwa hiyo nilimuomba msamaha. Tulimaliza mgogoro wetu, tulihama ile nyumba ili kuwa mbali na Paul. Kwa hiyo kumbukumbu kuhusu Paul ikawa historia tu. Itaendelea wiki ijayo.
Sioni nguvu kubwa iliyonituma kusaliti ndoa yangu, isipokuwa yale mazoea na ukaribu ndiye Shetani wa usaliti.
“Kilichonifanya nijione siwezi kuishi bila Paul hayakuwa mapenzi makubwa, isipokuwa ni yale mazoea. Nawaasa wanawake wenzangu waheshimu ndoa zao, maana kama mume wangu angekuwa siyo mvumilivu, leo ningekuwa sina ndoa.”
HITIMISHO
Siku zote, uaminifu ni nguzo. Mtu mwenye malengo yake hawezi kuteleza kwa kiwango kikubwa mpaka kutoka nje ya ndoa. Shikilia hapo ulipo, vishawishi vya hapa na pale visikuyumbishe.
Lauryn ametufundisha kwa mfano. Jambo lenye faida kwako ni kutambua thamani ya mwenzi wako kisha umlinde kwa hali yoyote ile. Kumsaliti ni kumaanisha hujitambui, hujielewi, akili yako haina malengo.
Mantiki ni kuwa unaposaliti, maana yake unaliweka rehani penzi lako. Mtu mwenye malengo hawezi kufanya hivyo. Nikutakie kila la heri katika maisha yako ya sasa na yajayo. Daima penzi lenu liwe imara.

SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE MZEE!

Stori: Imelda Mtema na Ojuku Abraham
YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.
Michael Christian‘hendsam’boi’ aliyevunja ndoa na ndoa hiyo na mheshimiwa huyo ndani ya Ofisi za Global.
SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.

SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.

SIRI YA NNE
Siri zilizidi kubanjuliwa, Michael alisema sababu ya nne ambayo pia ilimsukuma kuamua kubatilisha ndoa yake na mama Kasikila ni baada ya kubaini kwamba, hataweza kupata uzao kwa mke huyo kwa sababu ana watoto wakubwa kiumri kuliko yeye.
“Nilijua sitapata watoto, hakukubali kuzaa na mimi kwa sababu tayari ana watoto wakubwa, mimi mdogo, ingekuwa vigumu. Kifupi haikuwa ndoa halali kwangu,” alisema kijana huyo.

SIRI YA TANO
Michael: “Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima ndoa ivunjike.”
SIRI YA SITA
Kijana huyo hakuona sababu ya kubakiza siri hata moja, akaendelea kuzianika:
“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu.
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi.
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael. 

SIRI YA SABA
Michael alisema sababu ya saba ambayo pia ilimshinikiza kuivunja ndoa hiyo ni kupwaya ndani ya nyumba.
Alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.

SIKU ALIPOIVUNJA NDOA
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani.
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.

ANATAKA KILIO CHAKE KIFIKE KWA JK
Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.
“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.

MSIKIE MBUNGE SASA
Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”
AWAWEWESEKEA WANASIASA
Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo.

MAMA RWAKATARE BWANA
Kwa upande wake, Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kwa lengo la kumsikia chochote kuhusu ishu hiyo, alianza kulalamikia habari iliyoandikwa miezi miwili nyuma na kukata simu.  

ROMANI KATOLIKI WAWASHUKIA BONGO MOVIE

Stori: Jelard Lucas
KANISA la Romani Katoliki limeishukia tasnia ya filamu Bongo (Bongo Movies) kutokana na matendo maovu yanayofanywa na wasanii katika sinema zao hususan suala zima la kuheshimu imani za watu.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Thadeus Ruwa’ichi amewaonya wasanii kuwa maigizo yao yasilenge kuchafua umma ama kikundi chochote kwani wanaweza kuleta mgawanyiko katika taifa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Akizungumzia msimamo wa kanisa kuhusiana na filamu ya Sister Maria ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ ambayo kanisa hilo liliipinga kutokana na madai ya kukiuka maadili, Askofu Ruwa’ichi alisema hawakubalini nayo kwani mavazi ya masista yaliyotumiwa na wasanii hao, yalitumika vibaya hivyo hawakubaliani nayo.
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
Akifafanua zaidi kuhusiana na filamu hiyo, kiongozi huyo wa kiroho alisema alisononeshwa na kazi hiyo ambayo ilikuwa na dosari za kuingilia imani ya kikatoliki kwani mavazi ya kanisa yalitumika kuvaliwa bila staha.
“Ile filamu ilikuwa na lengo la kuhatarisha jamii, kamwe isiendelee kwani ni hatari kwa watu ama mtu binafsi anayechukizwa na tatizo hilo,
“Maigizo yanayofanywa yanaweza kuwa na lengo la kutumbuiza, lakini kutumbuiza kokote kule, hakupaswi kuhatarisha lengo la kulea ama kuvuruga mambo ya watu fulani, kulinda heshima ya watu binafsi ama taasisi, nidhamu inahitajika kwa kila jambo wanalolifanya,” alisema.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Askofu huyo alisema taifa lina mambo mengi na linajivunia kwa amani ya muda mrefu, hivyo waigizaji hao wanapoigiza maigizo ambayo yanagusa imani au jamii ya watu wengine linaweza kuwa tatizo kubwa huko mbele.
“Hakuna haja ya maigizo kuchafua watu wengine, heshima kwa wote ni jambo jema ambalo linaweza kuongeza upendo kwa kila jambo ufanyalo kwa jamii nyingine.
“Wakifanya kazi zao kwa ufasaha bado taifa litawaheshimu, hakuna mtu ama kundi ambao wangependelea kutokee vurugu eti kwa sababu ya maigizo ya mtu fulani, haiwezi kuungwa mkono,” alisema askofu huyo.

PENNY; CHAGUA BEGA, CHAPA ILALE!

Stori: Anko Nangale
LEO nabonga naye mwanadashosti anayeuza nyago kwenye kichupa cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Nianze kwa kukupa gwala kiroho safi. Juzikati umefunguka kuwa umepiga chini kiaina malovee na Diamond, mzuka mwingi. Umetisha sana.
Mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Unajua laifu la malavidavi ndivyo lilivyo siku hizi. Mizinguo inakuwa mingi na wengi huwa wanatambua kuna taimu inafika unalazimika kupiga chini ili michongo mingine iendelee.
Nikiwa katika mingo zangu za kusaka chambi, nilipata bahati ya kuchonga na masela f’lani hivi ambao walikuwa wakizimikia penzi lenu, walipenda kuliona linakimbiza kitaa deile lakini wakasema umechagua bega sahihi, kubwaga manyanga kwa pisi.
“Ni uamuzi mzuri sababu mchizi akiwa hasomeki huna haja kufosi kingi wakati unaona hivihivi chombo kishaenda mrama, halafu mbona mtoto mwenyewe full mauzo, shepu anayo na ameumbika kinoma?” alifunguka mwana mmko.
Kwa wale ambao hatuko pamoko, msiogope. Ishu ilikuwa hivi, mapema wiki hii Penny alibonga na midia na akafunguka kuwa hamchukii ex wake huyo lakini wameamua kupeana spesi kiaina ili kila mmko wao aweze kufanya yake bila kupeana bugdha.
Penzi lao lilikuwa na tensheni ya kufa mtu, mingo zao za kimahaba zilikuwa zinasanuka kila kukicha. Baadhi ya wana walikuwa hawazimiki na skendo zako, ziliwaboa kinoma lakini hawakuwa na sehemu ya kufikisha meseji zao, waliamua kupiga kimya kimtindo.
Kwenye midia ulifunguka kuwa kama ikitokea umepata doni mpya, hutamaindi awe mtu maarufu, hicho ndicho wana wengi walichokitolea saluti. Wameona mafahari wawili hamuwezi kuishi kwenye zizi moko.
Kabla sijamaliza, nikupe salamu za watoto wa kishua kule kipande cha Oysterbay, Masaki na Mikocheni. Nao walizimika sana na yai lako, walipenda unavyodondosha ung’eng’e katika mahojiano yako ya mtandaoni.
Kimsingi ulienda nao sawa, walikuelewa kinoma. Ulipokuwa ukitema yai, wengi walikuwa wakiwatonya matha zao, si unajua zile za; “dadi, yu noo, shi izi andastendi…!” walifunguka kwa matha zao.
Walizimikia msimamo wako na kutamani wakupe tano hata la mbali.
Siyo kesi, chapa ilale umeshachagua bega. Spesi mmepeana, kamata kiburudisho kipya na muvi jipya liendelee.

MUUNGANO WA UTEPE MWEUPE WAKUTANA WAZIRI MKUU PINDA, KUJADILI NAMNA YA KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO

Wajumbe wa Mkutano kati ya Utepe Mweupe na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Ikulu.
Mkutano wa Waziri Mkuu na wajumbe kutoka Muungano wa Utepe Mweupe ukiendelea. Mkutano wa Waziri Mkuu na wajumbe kutoka Muungano wa Utepe Mweupe ukiendelea.
David Lyamuya kutoka Muungano wa Utepe Mweupe akimvisha utepe Mweupe Waziri Mkuu, Pinda.
*Ni kujadili namna ya kupunguza vifo vya wajawazito

FORBES MAGAZINE REVEALS MO AND MAKAMBA JR AMONG 10 POWERFUL MEN IN AFRICA 2014‏

Mohammed Dewji, Tanzania, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited
Dewji is the Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) and at 39 is the youngest member of the Forbes’ Africa’s 50 Richest list with an estimated net worth of USD $500 million.
The MeTL Group began as a family business, a small trading company which Mohammed transformed into one of the largest industrial conglomerates in East Africa, with interests ranging from real estate, agriculture, finance, distribution and manufacturing.
The company employs more than 24,000 people across Tanzania and according to Dewji, generates annual revenues of USD$1.3 billion.
Dewji has been a Member of Parliament in the National Assembly of Tanzania since 2005. Dewji graduated from Georgetown University with a degree in International Business and Finance with a minor in Theology.
January-Makamba1
January Makamba Tanzania, Deputy Minister of Communication, Science & Technology.
January Makamba Tanzania, Deputy Minister of Communication, Science & Technology and Member of ParliamentMakamba is one of Tanzania‘s rising stars in government. He is currently the Deputy Minister of Communication, Science and Technology and is rumored to run for President in 2015.
Makamba is a Member of Parliament for Bumbuli constituency in the National Assembly of Tanzania. Before running for the Bumbuli parliamentary seat, Makamba was aide to Tanzanian President Jakaya Kikwete for 5 years.
Named Young Global Leader class of 2012 by the World Economic Forum, Makamba comes from a political family; his father, Yusuf Makamba was Secretary General of the ruling CCM party under Julius Nyerere.

Wednesday, January 22, 2014

B ENKI KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA SH 50,000....ANGALIA HAPA



Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.


Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.
Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’. 
Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.
-Tanzania daima

Zile mali za mastaa, mwimbaji Barnaba nae katuonyesha hii ndio nyumba aliyojenga.

Screen Shot 2014-01-22 at 1.38.10 AMSio kwamba mastaa wa zamani wa bongofleva hawakuwa wanapata chochote kwenye malipo kutokana na kazi zao bali  imefahamika kwamba mipangilio na matumizi mazuri ya fedha havikuzingatiwa sana kwa baadhi ya Wasanii wachache ambao walibahatika kuzipata pesa nyingi zilizotokana na mauzo ya kanda na show.
Wasanii wengi wa bongoflevani sasa hivi wameshtukia mchezo ndio maana wengi wao wanaingia kwenye headlines za kuonyesha mali zao kama nyumba na magari siku kadhaa tu baada ya kusikika kwenye chati za bongofleva ambapo hii kwa kiasi kikubwa ni kutokana na malipo ya show zao, wengine mauzo ya nyimbo kwenye miito ya simu, dili za makampuni na ishu nyingine.
Barnaba ni miongoni tu mwa waimbaji wenye talent zao na amekua akifanya showz mbalimbali hata nje ya Tanzania pamoja na kupata dili za mashirika/taasisi mbalimbali na kufanya nao kazi zikiwemo za ubalozi mfano Pepsi, Barclays Bank na wengine kama unavyoweza kuona moja ya stori zake za mwaka 2013.

Picha mpya za Rihanna zinazo-make headline kwenye internet hivi sasa

0Rihanna ame-share picha zake akiwa kwenye mapumziko huko Brazil ambazo zinasambaa sana hivi sasa kwenye mtandao.
Rihanna akiwa Brazil ametumia muda huo pia kupiga picha kwa ajili ya cover ya Vogue Magazine.
Hizi picha amezipiga akila good time kwenye yatch.
6
5
4
3
2
1

Ajali nyingine yatokea asubuhi hii Mtwara.


lattestTaarifa iliyotufikia hivi punde ni kuhusu ajali ambayo imetokea asubuhi hii ya leo majira ya sa 12 huko Mtwara ambayo imehusisha wanafunzi wa Shule ya Secondary ya Mustapha Sabodo ambao walikua wanakimbia mchaka mchaka.
Chanzo cha ajali hiyo kinasema kuwa kuna Gari ndogo aina ya Benzi ilimgonga mwanafunzi mmoja aliyekuepo kwenye mchamchaka huo baada ya wanafunzi kuona hali hiyo katika hali ya taharuki ndipo bila kuangalia nyuma lori lingine likaja kuwagonga wengine.
Taarifa mpaka sasa ni kwamba mwanafunzi mmoja amefariki pale pale na wengine watatu wamefariki hospitali,idadi ya majeruhi mpaka sasa ni zaidi ya 20,Dereva wa Benzi amejisalimisha kwenye kituo cha polisi Mtwara,ingawa dereva wa lori amekimbia.
Millardayo.com inaendelea kufatilia taarifa hizi.

Ya huyu Mwanamke wa Russia kukalia hiki kiti chenye umbo la Mwanamke wa Kiafrika umeiona?


Screen Shot 2014-01-22 at 9.57.10 AM
Russian Socialite ambae ni muhariri wa jarida la Garage magazine, Dasha Zhukova akiwa pia ni patner wa mmiliki wa club ya Chelsea Roman Abramovich, ameingia kwenye maporomoko ya matusi na maoni mengine mazito ya watu mbalimbali mtandaoni baada ya kusambaa kwa picha inayomuonyesha akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mfano wa Mwanamke wa Kiafrika.
Mwanamke huyu ambae anasema ana mapenzi na fashion pamoja na usanii wa vitu kama hivi amekosolewa na wengi ambapo baadhi ya Wanawake hata wenye ngozi kama ya Dasha, wamemkosoa huku wengine wakiuliza ‘bado tunafanya vitu hivi mpaka huu mwaka wa 2014?’
Screen Shot 2014-01-22 at 9.38.20 AMKiti hiki kimedizainiwa na msanii raia wa Norway Bjarne Melgaard ambapo baada ya kupostiwa kwa picha hii kwenye mitandao akiwa anafanyiwa interview na tovuti ya Buro 24/7 , muda mfupi baadae waliitoa hii picha na kuomba radhi kwa kitendo hicho.
Sehemu ya maelezo yao ilisema ‘sio nia yetu kuendeleza au kufanya ubaguzi kwa binadamu yeyote’

Unataka kuwaona wanaotuhumiwa kushambulia Westgate? tazama walipokwenda eneo la tukio chini ya ulinzi

2Ripota wangu wa nguvu Julius Chemitei kutoka Nairobi anaripoti kwamba Hakimu na pande husika dhidi ya washukiwa wa shambulio la Westgate wametembelea eneo la tukio kutekeleza amri iliyotolewa na hakimu mkuu Daniel Ojenja wiki iliyopita kabla ya kesi hiyo kuahirishwa.
Hakimu Daniel Ochenje alizungumza na waandishi kwenye hii ziara na kusema umuhimu wa ziara hiyo ni kuwezesha pande husika kupata taswira ya eneo hilo wakati Mashahidi wanapolihusisha eneo la tukio kwenye ushahidi wao Mahakamani.
Mawakili wa washukiwa wanaendelea kusimamia kwamba wateja wao hawana hatia yoyote na baada ya ziara hiyo walikua tayari kuendelea na kushirikiana na Mahakama wakati wakisubiri uamuzi kutolewa.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 27 & 28 January 2014 wakati upande wa mashtaka ukitarajiwa kuwasilisha mashahidi wengine 28 ambapo hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa mawakili wa upande wa Washukiwa kwamba viongozi wa mashtaka hawajawapa taarifa za polisi zilizoandikishwa na mashahidi.
3
1
6Hawa ni baadhi wa washukiwa wenyewe wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la Westgate.
5
4

Loga akesha, kisa Yanga SC



 

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic.
Na Hans Mloli
POINTI tatu katika mechi nne za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, zimemfanya Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, akose usingizi.
Logarusic, raia wa Croatia, maarufu kama Loga, amesema kati ya pointi hizo 12, tatu ni zile dhidi ya Yanga na amekuwa akipiga hesabu atazipata vipi kwa kuwa wakikutana anatambua ‘patachimbika’.
Akizungumza na Championi Jumatano, Logarusic amesema anajua mechi dhidi ya Yanga itakuwa ngumu sana lakini anazihitaji pointi zao tatu.
“Ndiyo pointi za Yanga ni muhimu sana, lakini jumla pointi 12 za mzunguko wa pili ndiyo zinaninyima usingizi.
“Mechi dhidi ya Yanga, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Azam FC. Najua itakuwa kazi ngumu kuzipata, lakini nazitaka, ni muhimu sana kwetu kimahesabu,” alisema Loga.
Katika timu nne anazozihofia, mbili kati ya hizo, Loga ameishacheza nazo katika mechi ambazo si za mashindano.
Loga alikutana na Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe na kuifunga mabao 3-1 wakati alipocheza na Mtibwa Sugar katika mechi ya kirafiki, kikosi chake kililala bao 1-0.
Tangu aanze kuifundisha Simba, haijawahi kucheza na Azam FC wala Coastal Union ambayo imefunga safari hadi nchini Oman kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Iwapo Logarusic atafanikiwa kukusanya pointi hizo 12 za timu hizo vigogo, maana yake atakuwa katika nafasi ya kutwaa ubingwa.
Simba inafungua dimba la mzunguko wa pili Jumapili, wakati watani wao Yanga na vinara wa ligi hiyo watatangulia dimbani Jumamosi.
Kuhusiana na mechi ya Jumamosi, Loga ametabiri kwamba wapinzani wao Yanga watashinda kirahisi.

ANGALIA ALAMA HIZI, ANZA MWAKA NA FIKRA MPYA!-4

KUTAMBUA alama za nyakati na kuangalia maisha yako ni jambo la msingi sana rafiki zangu. Kwa majuma matatu mfululizo yaliyopita, tumeona alama nyingi za wenzi ambao siyo sahihi kutokana na tabia zao.
Tulianza kwa kuwaangalia wanawake, tukaingia kwa wanaume ambapo tunaendelea pale tulipoishia kabla ya kugeukia katika ushauri kwa wote. Wiki iliyopita tuliishia pale ambapo mwanamke humshusha mwanaume waziwazi kwa matendo yake.
Mfano kusifia wanaume wengine mbele ya mwenzi wake au kufanya jambo lolote linaloashiria kuwa yupo naye lakini si kwa malengo ya muda mrefu.
Hebu sasa tuendelee kujifunza...
HATAOLEWA NA WEWE!
Mwanamke huyu anaweza kuzungumzia kuhusu kuolewa lakini siyo na wewe. Mathalani, anaweza kusema: “Duh! Mwanaume atakayenioa atakuwa na kazi sana.”
Kauli hiyo ni tata na mara zote haina maelezo mengine yoyote mbele yake.
Ni kweli anajua kwamba ataolewa siku moja, lakini wewe huna chako. Anamuwaza mwanaume mwingine kabisa. Hata hivyo, hawezi kukuambia mojamoja, atatumia tenzi, ngano na methali katika kufikisha ujumbe huu kwako.
MASHARTI KIBAO
Mwanamke huyu ni mjanja sana, anaonekana ana mambo mengi, ni kama hataki mapenzi yajulikane, lakini mbaya zaidi kwa kuwa anajua wazi kwamba hana mapenzi na wewe hataki umharibie!
Ana masharti kibao ambayo hayaeleweki. Hapendi muongozane, hasa kwenye sehemu zenye watu wengi. Hata kama ikilazimika kufanya hivyo, hukuchagulia mahali pa kupita.
HANA WIVU...
Hafikirii sana kuhusu kusalitiwa, hana muda na simu yako na wala haonyeshi dalili zozote za kujali sana penzi lako. Hafikirii kwamba siku moja unaweza kumsaliti. Hana muda huo.
Anaweza kukudhihirishia hili moja kwa moja, hata pale utakapokuwa umepanga kutoka naye, halafu ghafla akakuambia amepata dharura lakini atakupa rafiki yake uende naye kwenye pati. Hili ni tatizo na ni lazima uwe nalo makini kwa kiwango cha mwisho.
Mwanamke ambaye hana wivu, kuna mapenzi kweli hapo? Hana shida na wewe ndiyo maana basi hafikirii sana kuibiwa. Iache akili yako itafakari hili kwa makini, mwisho wa siku utajua cha kufanya.
RATIBA ZISIZOELEWEKA
Ana mambo mengi sana ambayo hayaeleweki, pengine ana ratiba zake kabisa, lakini hakuweki! Yeye anawaza mipango yake kama yeye na inawezekana kabisa hujui ratiba zake na hajakuambia.
Hata kama alikuambia, siyo ratiba yake kamili. Kimsingi hataki ufahamu kabisa juu ya mambo yake. Hii nayo ni alama tosha ambayo itakufanya uelewe kwamba upo katika penzi la wizi. Hakuna anayekupenda hapo.
USHAURI KWA WOTE
Mapenzi siyo kitu cha mchezo, umakini ni jambo la kwanza kabisa ambalo unatakiwa kuwa nalo katika uhusiano. Siku zinazidi kwenda mbele, sasa hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda kwa mtu ambaye umeshagundua kuwa hakupendi.
Hana ‘future’ na wewe, hawazi kwamba unaweza kuwa wake wa maisha siku moja, wakati wewe ukiwaza hayo, mwenzako anawaza mambo mengine. Upo naye kwa ajili ya mapenzi ya dhati, mwenzio yupo kwa sababu ya kustarehe tu.
Tafakari kwa makini, lakini kuna sifa zaidi za kuziangalia ili kuona kama mwenzi uliyenaye ni kweli anafaa kuwa wako wa maisha au unapoteza muda wako. Hata kama anakupenda lazima uwe na sababu zako za kumfanya awe wako wa maisha.
Mambo yafuatayo ni muhimu zaidi kuzingatia wakati ukiwa katika uhusiano ambao unahitaji uwe wenye malengo. Tuendelee kujifunza...
NI WA NDOTO ZAKO?
Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu ni kama mwenzi huyo ni wa ndoto zako. Je, yukoje? Siku zote kabla ya kuamua kufanya chochote lazima ujiulize kama ndicho ulichokuwa ukikifikiria.
Hata kwa upande wa mwenzi wako, lazima ujiridhishe, ni kweli ni yule uliyekuwa unamtarajia? Ana sifa unazohitaji? Acha tabia ya kujifariji kwamba utampenda taratibu ndani ya ndoa, hicho kitu hakipo.
Hakuna kujifunza kupenda katika ndoa, lazima ujihakikishie mwenyewe kuwa mwenzi wako ni yule mwenye sifa ulizokuwa ukizitarajia. Hili ni la msingi, maana unaweza kuwa naye siku mbili, ukatamani mwingine nje. Kwa  nini? Kwa sababu si yule mwenye sifa ulizotarajia.

MMILIKI WA YANGA AIBUKA, ATAKA KWENDA KWA KIKWETE


Juma Mwambelo.
Na John Joseph
ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.
“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.
“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),” alisema.
Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.
“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema.
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.
“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku akitabasamu.

WAZIRI JOHN MAGUFULI, NOMA

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, John Pombe Magufuli, wikiendi iliyopita alidhihirisha yeye si mtu wa kubabaika, badala yake anachapa kazi kulingana na kauli mbiu ya ari, nguvu na kasi zaidi.
John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Jumapili iliyopita, wakati Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, akitangaza mabadiliko ya nafasi za mawaziri na manaibu wao kama Rais Jakaya Kikwete alivyoteua, Magufuli alikuwa ‘bize’ akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Magufuli akiendelea na ukaguzi wa daraja hilo.
Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya waliomshuhudia walisema: “Huyu ndiye kamanda, aisee ni noma sana!”
Kauli hiyo, ilitokana na ukweli kwamba Magufuli hakuwa na wasiwasi wala mchecheto kuhusu nafasi za mawaziri na kuonesha kwamba anajiamini na yupo kikazi zaidi, ndiyo maana aliamua kuzipa kisogo taarifa kutoka ikulu na badala yake kusimamia ujenzi wa daraja hilo ambalo linatajwa kuwa la kihistoria.

Daraja la Kigamboni.
“Muda ambao Magufuli alikuwa anakagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni, mawaziri na manaibu wengi walikuwa wakifuatilia taarifa ya Balozi Sefue kwenye vyombo vya habari kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete.
“Magufuli hakujali kabisa hilo, ndiyo maana alichokifanya ni kwenda kukagua daraja hilo ambalo likikamilika, litaacha heshima kubwa kwa Rais Kikwete,” alisema Mwisege Kimbati katika maoni kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Rebecca Mwizarubi katika maoni yake Facebook, alisema: “Ni Jumapili, ni wikiendi, watu wapo kwenye mapumziko, wengine wanastarehe kama siyo na familia basi katika viwanja mbalimbali lakini Magufuli yupo kazini anachapa kazi. Tunahitaji viongozi wa aina yake. Magufuli ni hazina ya nchi hii.”

Daraja la Kigamboni linaloendelea kujengwa.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mitandao mingi ‘iliposti’ picha hizo za Magufuli na wachangiaji wake walimsifu Magufuli kwa kupiga kazi bila kujali kwamba ilikuwa Jumapili, vilevile kwa kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na taarifa ya mabadiliko ya mawaziri.