Saturday, February 1, 2014

USALITI HAUNA NGUVU, SHETANI WA USALITI NI AKILI ILIYOKOSA MALENGO-10

Tunaendelea na mada yetu ambayo tumeianza wiki kadhaa zilizopita, inahusu fundisho la usaliti. Endelea...
Sikumtaka mume wangu wala Paul, wote niliwaona wana matatizo, yaani hawajakamilika. Saa 4 usiku ndiyo nilikwenda kulala.
“Niliamka saa 3 asubuhi, muda huo mume wangu alikuwa ameshakwenda kazini. Mtoto wangu mkubwa naye alishakwenda shuleni, maana huondoka asubuhi pamoja na baba take. Nilikwenda chumba cha watoto na kumkuta mtoto wangu akiwa bado kalala, kama kuhakikisha nilikwenda chumbani kwa Paul nikamkuta amekaa kitandani kwake anasoma kitabu cha mapenzi.
“Baada ya salamu, nilimuuliza sababu ya kutokwenda kazini mpaka muda huo, akanijibu alikuwa ananisubiri mimi niamke. Aliniambia asingeweza kufanya kazi zake ipasavyo kama hatatimiza lengo la kucheza ‘kikwetukwetu’ faragha na mimi. Nilicheka, kisha nikamuuliza kama anaweza.
“Akaniambia anaweza. Kusema ule ukweli pale nilikuwa nimeshamuona Paul kama mgonjwa asiye na jeuri yoyote kitandani. Nilicheka kama kumsanifu halafu nikaenda bafuni kuoga. Nilimuamsha mtoto wangu, nikamuogesha halafu nikampa chai anywe, alipomaliza kunywa chai nilimpeleka kwa mama mdogo.
“Nilirudi nyumbani nikiwa najiuliza mengi lakini kubwa ni kama Paul ataweza. Nilijua ni mbovu tu, anayetaka kunichezea lakini nilimpa nafasi ya mwisho, ndiyo maana nilihakikisha pale nyumbani tunakuwa wawili tu ili akishindwa asiwe na kisingizio kingine.
“Nilipofika nyumbani nilifunga mlango mkubwa, nikaenda moja kwa moja chumbani kwa Paul. Nilimkuta amelala anasoma kitabu, nilikaa jirani yake, nilimwambia awe na uhakika kama ataweza, siyo nasaula halafu hakitokei chochote.
“Kweli ni aibu, maana mimi kwa umri namzidi Paul miaka sita, ukichangia na umbile langu, halafu nisaule nguo zote naye anione kama nilivyozaliwa nikiwa na matarajio ya kupata penzi ambalo silipati, ni aibu iliyoje? Paul alionekana kujiamini sana, akanihakikishia kwamba hataniangusha.
“Paul aliachana na kitabu chake, akanifuata pale nilipokaa. Nilikuwa nimevaa kanga na blauzi, kwa ndani ni kufuli kama kawaida, juu ni ‘brazia’. Alinitoa kanga nilimkubalia, vilevile kabati langu aliliondoa, alipotaka kuhusika na blauzi nilimgomea, nilimwambia ingewezekana vilevile.
“Kiukweli nilikuwa simuamini ndiyo maana sikutaka aguse blauzi yangu. Siku hiyo sikuwa mfuatiliaji sana kwa sababu nilihofia kwamba atashindwa. Mwanzoni kama alihangaika, yaani gari lake lilianza kuleta mgogoro kwenye kuwaka lakini baadaye stata ilikubali, mambo yakawa safi kabisa.
“Ni dereva mzuri, anaendesha vizuri gari lake, nilimkubali. Nilimuuliza mbona usiku alishindwa, akanijibu hata yeye anashangaa. Ubora wake anaposhika usukani, ndiyo uliofanya nisichoshwe naye, ilipoisha safari moja, iliendelea nyingine. Paul alinifikisha nilipotaka, alinikata kiu yote.
“Kuanzia siku hiyo nilichanganyikiwa kabisa kwa Paul. Nikawa namdharau mume wangu, kwani hata alipotaka huduma chumbani sikumpa. Mume wangu aliposafiri nililala na Paul. Hatukujali matumizi ya kinga wala kujali mzunguko wa siku, basi ikawa napata mimba natoa.
“Penzi la Paul lilinitia wazimu, kila alichoniambia nilikisikiliza bila kuhoji. Neno lake likawa sheria. Tukadanganyana tutaoana, nami nikavimba kichwa. Mgogoro na mume wangu ukawa mkubwa, kila siku vikao kwa wazazi, nikawa nasisitiza nipewe talaka.
“Nilipoona anakuwa mgumu kunipa talaka, ikabidi nimwambie kwamba nina uhusiano na Paul, nilifanya vile achukie anipe talaka yangu. Kumbe nikawa nimechokoza moto, ulitokea ugomvi mkubwa kati ya mume wangu na Paul, waligombana mpaka kufikishana polisi.
“Huwezi kuamini, pamoja na ugomvi huo lakini hatukuacha. Mimi na Paul tuliendelea na mapenzi yetu. Hata nilipogombana na mume wangu, nami kurudi kwetu, niliwasiliana na Paul akiwa nyumbani, nami nilikwenda, tukajifungia chumbani kwake na kufanya ya kwetu. Tulipomaliza nilirudi kwetu, yaani kwa mama mdogo.
“Baada ya wazazi kuona mgogoro ni mkubwa ndani ya ndoa, huku ikiwa wazi kwamba tatizo ni Paul, waliamua kunisafirisha kwenda kwa shangazi yangu Dodoma ili nikae huko, angalau niwe mbali na Paul. Hiyo safari ndiyo iliyonisaidia kujitambua.
“Nikiwa Dodoma, kwanza hisia zangu kwa Paul zikapungua, halafu nikaja kusikia sifa zake za kubadili wanawake kama nguo, halafu analala nao chumbani kwake, niliona amenidhalilisha sana. Nikaanza kukumbuka mazuri ya mume wangu, nikajuta kwa kila kitu.
“Uzuri ni kuwa mume wangu hakunipa talaka, kwa hiyo nilimuomba msamaha. Tulimaliza mgogoro wetu, tulihama ile nyumba ili kuwa mbali na Paul. Kwa hiyo kumbukumbu kuhusu Paul ikawa historia tu. Itaendelea wiki ijayo.
Sioni nguvu kubwa iliyonituma kusaliti ndoa yangu, isipokuwa yale mazoea na ukaribu ndiye Shetani wa usaliti.
“Kilichonifanya nijione siwezi kuishi bila Paul hayakuwa mapenzi makubwa, isipokuwa ni yale mazoea. Nawaasa wanawake wenzangu waheshimu ndoa zao, maana kama mume wangu angekuwa siyo mvumilivu, leo ningekuwa sina ndoa.”
HITIMISHO
Siku zote, uaminifu ni nguzo. Mtu mwenye malengo yake hawezi kuteleza kwa kiwango kikubwa mpaka kutoka nje ya ndoa. Shikilia hapo ulipo, vishawishi vya hapa na pale visikuyumbishe.
Lauryn ametufundisha kwa mfano. Jambo lenye faida kwako ni kutambua thamani ya mwenzi wako kisha umlinde kwa hali yoyote ile. Kumsaliti ni kumaanisha hujitambui, hujielewi, akili yako haina malengo.
Mantiki ni kuwa unaposaliti, maana yake unaliweka rehani penzi lako. Mtu mwenye malengo hawezi kufanya hivyo. Nikutakie kila la heri katika maisha yako ya sasa na yajayo. Daima penzi lenu liwe imara.

No comments:

Post a Comment