Saturday, January 4, 2014

PENNY ABWAGIWA KEKI YA KUSUTWA

Stori: SHAKOOR JONGO NA IMELDA MTEMA
KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
Peniela Mungilwa ‘Penny’.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.
Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Penny, aliliambia gazeti hili kuwa msafara wa magari matatu ulifika hapo na kugonga mlango wakimuulizia mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha Channel Ten.
“Walivyofika sisi tulijua labda leo ni bethidei ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na maua, keki, shampeni na kadi, walipomuulizia tukawaambia ametoka, wakaacha mzigo huo wakisema apewe atakaporudi,” alisema shuhuda huyo.
Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsuta na kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua mabwana wa rafiki zake pamoja na dada zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea ujumbe huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mtamboni.

MKWASA, PONDAMALI WAANZA KAZI RASMI YANGA

Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akiwaongoza wachezaji wake katika mazoezi leo.
Yanga wakiendelea na mazoezi chini ya Mkwasa katika Uwanja wa Bora uliopo Mabatini-Kijitonyama jijini Dar leo.
Kocha wa makipa Juma Pondamali akitaniana na kipa wake Juma Kaseja.
KOCHA msaidizi wa Yanga aliyechukua mikoba ya Fredy Felix Minziro, Charles Boniface Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Juma Pondamali leo wameanza rasmi kukinoa kikosi cha Jangwani katika Uwanja wa Bora uliopo Mabatini-Kijitonyama jijini Dar.

MASHABIKI WAMPONGEZA SCHUMACHER HOSPITALINI BIRTHDAY YAKE YA MIAKA 45

Michael Schumacher.
MASHABIKI wa Michael Schumacher leo walimtumia salamu za kuadhimisha kutimiza mwaka wa 45 tangu kuzaliwa kwake wakati akiwa amelazwa hospitalini kutokana na kujeruhiwa vibaya kichwani wakati alipokuwa akishiriki mchezo wa kuteleza kwenye barafu maeneo ya Alps nchini Ufaransa.
Schumacher ambaye ni mshindi wa mara kadhaa wa mbio za kuendesha magari  za Formula One (F1) hivi sasa anapata matibabu akiwa hajitambui baada ya kufanyiwa operesheni ya kichwa ambapo alikipigiza kwa bahati mbaya kwenye jiwe.
Schumacher ambaye mashabiki wake humwita Schumi, ndiye dereva mwenye  mafanikio zaidi katika mashindano ya  F1 akiwa ameshinda mara 91 kabla ya kustaafu mwaka 2012.

CHADEMA WAFANYA KIKAO CHA KAMATI KUU JANA JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed wakati wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu.

SIYO VIBAYA ‘KUIGILIZIA’

NIANZE kwa kumshukuru sana Mungu kwa kuweza kunijaalia kuwa mmoja wa waliofika salama salimini mwaka mpya wa 2014. Nimshukuru pia kwa niaba yenu, kwa sababu bila yeye tusingeweza kuwa hai leo.
Mwaka uliopita ulikuwa na changamoto nyingi sana kwetu, nyinyi mlio shule na sisi tulio mtaani. Naweza kusema kuwa ni bora yenu nyie, maana bado tunawaita kula kulala, kazi kubwa ilikuwa kwetu, mwenyewe unahitaji kula, kuvaa na kulipa kodi ya nyumba ya watu na nyumbani watu wengine watano wanakusubiri!
Katika maisha, kitu kikubwa ambacho binadamu anatakiwa kuwa nacho ni malengo. Yaani ni lazima ajue anachokitaka, iwe kwa muda mfupi, wa kati au mrefu. Kwa kawaida, huwa tuna ndoto nyingi za mafanikio, lakini ni wachache ambao huzigeuza kuwa kweli.
Lakini siyo lazima kila mara kwamba utimize ndoto zako kwa asilimia zote kile unachokilenga. Kufikia hata robo ya matarajio yako ni hatua katika maisha. Hivyo usikate tamaa, kama muhula uliopita kwa mfano ulipata daraja D, ni wazi kwamba umepanda sana kama hapo kabla ulikuwa katika lile daraja ambalo sisi zamani tulikuwa tunasema Fantastic (F), sijui nyie maanko mnaliitaje siku hizi.
Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza. Ninaposema kuigilizia, simaanishi ile tabia ya baadhi ya wanafunzi kupiga chabo kilichoandikwa na mwenzake ili na yeye aweze kukiandika katika karatasi yake wakati wa mtihani. Ninachomaanisha, ni kuiga tabia ya kujisomea ya mwenzako ili na wewe uweze kuwa bora, ikibidi zaidi yake.
Unajua, tukiwa shule kila mmoja ana usongo tofauti wa kusoma. Wapo ambao siku za nyuma niliwahi kusema, wanasoma utafikiri wametumwa na kijiji. Yaani wao wakiwa darasani, muda wote ni wao na daftari au kitabu. Wakati wengine hutumia nafasi ya kutokuwepo kwa mwalimu kwa ajili ya kupiga soga, wenyewe wapo bize na kusoma.
Utafikiri labda wako hivyo kwa sababu wapo darasani, la hasha, hata wakitoka, wakiwa nje ya darasa, mwendo ni huo huo na wakifika nyumbani ndiyo usiseme, muda wote wao ni kusoma!
Lakini kuna wengine sasa, kusoma ni mpaka awepo mwalimu karibu na anapotoka, na yeye anatoka.
Niseme kitu kimoja, kibiolojia, binadamu tunafanana kila kitu, ambacho mimi naweza kufanya hata wewe unaweza, kinachoweza kukutokea wewe, hata mimi kinaweza nitokea pia. Kwa maana hiyo, hakuna mtu mwenye akili kuliko mwenzake, isipokuwa tofauti ni jinsi gani wewe unavyoitumia akili yako kurahisisha mambo yako.
Tunawaona wenzetu na kusema, “Anko Oj ana akili sana darasani, huwezi kushindana naye”! Siyo kweli, hana akili kuliko sisi, isipokuwa  yeye anatumia muda mwingi kuifikirisha akili yake, ndiyo maana muda wote inakuwa iko active. Wewe huna muda huo ndiyo maana swali au research ndogo tu inakupa taabu kweli kweli!

Ni kweli kwamba wapo baadhi yetu tunawaita genius, hawa wana vipaji maalum walivyobarikiwa na Mungu, lakini kwa jumla, kama tungetaka kujihangaisha, wote tungeweza kuwa wanazuoni wazuri sana.
Nichukue fursa hii basi kuwaasa maanko kujaribu kwa kadiri tunavyoweza, tuwe bora zaidi kitaaluma mwaka huu kuliko ilivyokuwa mwaka jana. Kama hakuna budi, siyo vibaya kama nilivyosema, kuiga baadhi ya mbinu zinazotumiwa na wenzetu ambao wanafanya vizuri darasani kuliko sisi.
Angalizo langu kwenu ni lile lile, elimu ni mkombozi wako wa uhakika kabisa. Nadhani mnawaona vijana wenzenu wanavyohangaika kutafuta maisha ya juu kwa njia za mkato, wanajikuta wanatumiwa na matajiri kusafirisha madawa ya kulevya.
Haya ni matokeo ya kushindwa kwao kuzingatia shule. Huwezi kuwa PHD Holder halafu mjinga mjinga mwenye hela zake akufuate na kukubebesha unga. Na kusoma haimaanishi hadi uwe daktari au profesa, kusoma ni kuelimika na kuelimika ni ile hali ya kujitambua, wewe ni nani, unataka nini na kwa nini!
Pigeni kitabu kwa malengo, maisha mazuri yanatusubiri!

USALITI HAUNA NGUVU, SHETANI WA USALITI NI AKILI ILIYOKOSA MALENGO-6

Kuna hoja nzito kimantiki katika mada hii. Uchambuzi na ufafanuzi wa kina, vilishajitosheleza lakini nikaona kuna maana kubwa katika kufundisha kwa mifano.
Msomaji wangu Lauryn ameamua kuiweka wazi stori yake, jinsi alivyotoka kimapenzi nje ya ndoa na kijana Paul ambaye alikuwa mpangaji mwenzake.
Alishaeleza mengi huko nyuma, lakini wiki iliyopita aliishia hapa: “Sisemi uongo, siku hiyo ndiyo nilikuwa napokea kwa mara ya kwanza kiss la nje ya ndoa, tangu nilipoolewa na mume wangu. Sijui kama alibahatisha au ni ufundi aliojaliwa, maana aliufyonza kitaalamu ule mdomo wangu wa chini, mpaka nikapatwa na mchecheto. Kama ingekuwa chumbani, pengine ningemsukuma na kuchojoa viwalo vyote ili tuikamilishe mechi.”
Endelea kusoma: “Nilishindwa kufanya hivyo kwa sababu pale tulikuwa sebuleni halafu mume wangu alikuwa chumbani, kwa hiyo hakuwa na kizuizi chochote cha kutoka na kutufumania. Uoga huo ndiyo ulionifanya niidhibiti mizimu yangu ambayo kwa hakika, ilikuwa inaninyevuanyevua ile mbaya.
“Kweli sikuchojoa nguo kama ambavyo nilipenda iwe kama tungekuwa chumbani lakini hata hivyo sikubaki nyuma. Nami niliushughulikia mdomo wake wa juu ambao awali nilikuwa naung’ata. Hapo haikuwa habari nyingine, tulikuwa
tunatenda kitu ambacho wengi huanza nacho kabla ya tendo lenyewe la faragha.
“Yaani tulikuwa tunapeana busu la ndani kabisa, wenzetu wanaita deep kiss, kamusi ya kisasa inalitafsiri tendo hilo kama denda. Kilikuwa kipindi kizuri sana kwa wakati huo, maana kama kujuta, nilifanya hivyo baadaye baada ya kunikuta makubwa yaliyofanya ndoa yangu iwe chungu. Hakika usaliti ni mbaya.
“Tukiwa tunaendelea na kiss, mara nikamuona Paul amepoa, nilipomuona akiwa katika hali hiyo, sikutaka ionekane yeye ndiye ameamua kusitisha mchezo, niliinuka pale kwenye sofa kama mtu aliyekurupuliwa, nilikwenda msalani kujiosha kisha nikaenda zangu chumbani kwangu kulala na mume wangu bila kumuaga Paul.
“Siku iliyofuata asubuhi sikukoma, nilimkuta amesimama mlangoni akiwa ameelekea nje, nilimfuata nikamgusa kwa nyuma, yaani kifua changu nilikiegemeza mgongoni mwake. Nilifanya hivyo nikijua lazima ataweza kuakisi joto langu na kupata msisimko fulani wa ndani.
“Ni kweli nilikuwa na joto kali, mimi mwenyewe nilikuwa nalisikilizia. Lile joto lilisababishwa na mambo mawili, kwanza ndiyo nilikuwa natoka kitandani, pili nilikuwa na siku nyingi sijakutana na mume wangu. Tunalala na kuamka utadhani mtu na dada yake.
“Hili pia ni kosa la mume wangu, alikuwa mvivu sana kwenye kipengele cha faragha. Bila kujisikia vibaya, aliweza kukaa hata miezi mitatu na hatujakutana. Haombi huduma wala nini, sijui alikuwa na maana gani kufanya hivyo. Hali hiyo ilinifanya niwe nakaa na ‘ganzi’ zangu kwa muda mrefu mpaka kuingiwa na mawazo mabaya.
“Ni mawazo mabaya ndiyo, fikiria mimi kumtamani mpangaji mwenzangu ambaye kiumri namzidi kama miaka sita. Mbaya zaidi hata kimaumbile mimi ni mnene wakati Paul ni mwembamba, kwa hiyo hata bila kutafuta umri, kila aliyetuona, alipata jawabu kuwa mimi ni mkubwa sana kwa Paul.
“Basi pale nilipomuegemea Paul, naye alipata msisimko, nilimuangalia vinyweleo vyake vilikuwa vimesimama. Baada ya kuona hivyo, nilimuwekea mapozi, nilimsalimia na kurudi chumbani kwangu. Huko nikaendelea kupanga na kupangua jinsi ya kumteka Paul. Nilimhitaji sana kwa wakati huo.
“Kama dakika 20 zilizofuata, Paul aliaga anakwenda kazini kwake saluni (kazi yake ni kinyozi, nilishasimulia huko nyuma). Nilitamani kumwambia asiende lakini nikajisikia aibu kusema hivyo. Nilimuitikia kwa sauti iliyokosa unyoofu. Nilikuwa katika kipindi kibaya sana cha matamanio.
“Mchana nilipika chakula, nikamtumia SMS Paul aje kula, akanijibu kazi ni nyingi saluni. Nilijisikia vibaya lakini usiku tulipata muda mwingine mzuri. Maana baada ya chakula cha jioni (dinner), mimi na Paul tulibaki sebuleni tukizungumza lile na hili. Alitaka kuanza ule mchezo wa kuzomea, sikumpa ushirikiano.
“Aligusisha paji lake la uso kwenye la kwangu, bado sikumpa ushirikiano wowote. Sikutaka michezo, nilitaka tufanye kweli. Ndiyo maana nilipoona analeta yale mazoea ya kuzomeana sikumpa ushirikiano. Naye alipoona simpi ushirikiano, ikabidi ajiongeze na kutimiza kile nilichotaka.
“Kwa kutumia kinywa chake, aliitumbukiza midomo yangu ndani yake, kwa hatua hiyo nilimpa ushirikiano wa kutosha. Tulibadilishana kila ambacho iliwezekana kupitia vinywa vyetu. Nilisikia burudani hasa ila niliendelea na tabia yangu ya kumtegea Paul ndiye atangulie mbele nifuate.
“Kwa maana hiyo nilitamani tusiishie kwenye kiss peke yake, nilitaka mikono yangu ifanye utalii kwenye maeneo yote muhimu ya Paul, vilevile na yeye apitishe mkono wake katika kona tofauti za mwili wangu. Nilitamani anishike maeneo mengi lakini sikuthubutu kumuomba afanye hivyo na nilijizuia kumshika popote.
“Hatimaye Paul alifika pale nilipopataka, aliuruhusu mkono wake wa kushoto kufanya utundu kwenye mwili wangu. Wakati huohuo midomo yote iliendelea kung’ang’aniana. Ulimi wangu ulikuwa ukigeuzwageuzwa kinywani kwa Paul. Ni mfyonzaji mzuri. Nilifurahia kila kitu.

KIGOGO WA WEMA ATANGAZA VITA NA DIAMOND

Stori: Shakoor Jongo
Yule kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na Wema Isaac Sepetu katika pozi.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.
Wema Isaac Sepetu.
“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.
Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.
“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.
“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni arobaini na nane ziliteketea.
Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.
“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.
“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota  Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.
“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwa
Kajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.
Baada ya kujazwa data, Risasi Jumamosi lilijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond:
 “Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One.

LOWASSA AANGUSHA BONGE LA PATI NYUMBANI KWAKE

Stori: Mwandishi Wetu, Arusha
WAZIRI  Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Ngoyai Lowassa ameangusha bonge la pati la kuukaribisha mwaka 2014.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza katika sherehe ya mwaka mpya nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.
Tukio hilo lililojaa furaha ya aina yake lilifanyika Januari 1, mwaka huu nyumbani kwake Ngarashi- Monduli, mkoani hapa ambapo mamia ya watu walijumuika pamoja na mbunge huyo kuukaribisha mwaka.
Lowassa aliyeonekana na sura ya furaha, alishika kifaa chenye mkia wa ng’ombe ambacho ni cha asili na kuwasalimia waalikwa kwa kukichezesha kuashiria sherehe imeanza na watu waukaribishe mwaka mpya.
Mbali na wageni waalikwa, Lowasa alijumuika na familia yake akiwemo mkewe, Regina Lowassa ambaye pia alionekana akiambatana na mumewe kwa kuwasalimia ndugu wageni waalikwa.
Katika pati hiyo ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya, watu walikunywa, walikula hadi kusaza.
Waalikwa walimuomba Mh Lowassa kujenga utaratibu huo kila mwaka, ili kudumisha umoja na mshikamano.                   
Waalikwa katika shughuli hiyo, walikuwa ni pamoja na maaskofu na viongozi wengine wa dini wa ndani na nje ya nchi.
Waalikwa hao walimpongeza Mh Lowassa kwa kitendo cha kuamua kujumuika pamoja na ndugu zake na viongozi mbalimbali kwani kimeonesha ishara ya upendo.
“Ni jambo zuri sana Mh Lowassa amefanya kwa ndugu zake. Mwaka mpya ndiyo huu unaanza hivyo si vibaya akikutana na kufurahi pamoja na wadau mbalimbali,” alisema mmoja wa waalikwa.

MASOGANGE ANASWA AKIKATA MAUNO


Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’akikata mauno.
Stori: Imelda Mtema
BAADA ya kujificha muda mrefu tangu atoke mahabusu nchini Afrika Kusini kwa msala wa madawa ya kulevya, Video Queen Agnes Jerald ‘Masogange’ amenaswa ‘live’ akikata mauno huku akipewa kampani na mtoto mdogo nyuma yake.

Agnes Jerald ‘Masogange’ akiwa nyumbani kwa Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar
Weekly Star Exclusive  ilimbamba mrembo huyo juzikati nyumbani kwa mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’, Kijitonyama jijini Dar ambapo Nisha alikuwa akipiga makofi na kushangilia wakati Masogange alipokuwa akikata mauno.
“Sijacheza siku nyingi jamani ndiyo maana leo nimejikumbushia mambo yangu ya mjini, kuna vitu vingi sana nilivimisi kama kukutana na watu hivi na kucheka pamoja kwa uhuru,” alisema Masogange.
Wakati akiendelea kukatika, mtoto mdogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja mwenye umri uliokadiriwa kama miaka 7, alishangilia na kucheza naye pamoja.
Tangu arejee kutoka Bondeni, Masogange amekuwa shosti mkubwa wa Nisha ambapo mbali na urafiki, wanafanya filamu pamoja iitwayo Betina na Zena.
Kwenye msala wa madawa ya kulevya, Masogange aliachiwa kwa kulipa faini baada ya kuthibitika kuwa mzigo aliokutwa nao haukuwa madawa ya kulevya bali ni ‘material’ ya kutengenezea madawa tofauti.

ROHO WA KIFO BADO KWA MASTAA

Stori: Hamida Hassan na  Haroun Sanchawa
MTOTO wa  aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, Maalim Hussein Yahya ametoa utabiri wake wa mwaka na kusema kwamba vifo zaidi vitaendelea kutokea kwa mastaa wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na wanasiasa, Risasi Jumamosi linaweka bayana.
Aliyekuwa mtabiri  maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein.
Akifafanua kuhusu utabiri wake huo, Maalim Hussein alisema kwamba pamoja na vifo hivyo lakini mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio kwa baadhi ya mastaa na wanahabari.
Marehemu Ngwea.
“Pamoja na kwamba vifo vitatokea kwa mastaa na wanahabari lakini wapo kati yao watakaopata neema ya uongozi na kuwa watu wakubwa  kwa kushika nyadhifa mbalimbali,” alisema Maalim Hussein.
Akizungumzia kwa upande wa siasa, Maalim Hussein alisema nyota zinaonesha kwamba kuna kiongozi mmoja  kwenye vyama vikubwa vya siasa atavuliwa uongozi ghafla na kutokana na sakata hilo ataanguka na kufariki dunia.
Kama vile haitoshi, Maalim Hussein alisema baadhi ya  viongozi wa dini watapata kashfa ambazo zitawasababishia umauti pamoja kuvuliwa uongozi katika nyadhifa walizonazo.
Maalim huyo ameongeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mwaka huu kutatokea vuguvugu kubwa litakalosababisha mapigano ya jamii kwa jamii na jambo hilo huenda likasababisha vifo.
Mbali na misiba hiyo, Maalim Husseina alisema kwamba mwaka huu kutakuwa na msiba utakaoligusa taifa moja kwa moja na kuongeza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi ambalo litaleta neema kubwa kwa jamii.
“Huu ni utabiri wangu kwa mwaka, natarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mengi kwani haya ni baadhi ya  mambo machache kati  ya mengi,” alisema Maalim Hussein.
Mwaka jana, Maalim Hussein alitabiri kutokea vifo vya baadhi ya  mastaa ambavyo vilitokea na kuufanya utabiri wake kutimia.

SIRI NZITO YAVUJA: RAIS HAVUNJI BALAZA LA MAWAZIRI

Stori: mwadishi wetu
SIRI nzito imevuja! Ni dhahiri kwamba, Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ hatavunja baraza la mawaziri kufuatia kusitisha kwake uteuzi wa mawaziri wanne na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi,  Dk. William Augustao Mgimwa kama wengi wanavyoamini bali atabadilisha tu, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Rais Jakaya Kikwete ‘JK’.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa ni Emmanuel John Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Balozi Khamis Juma Kagasheki (Maliasili na Utalii) aliyejiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili na haki za binadamu katika Oparesheni Tokomeza Ujangili.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
KWA NINI HAVUNJI BARAZA?
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani serikalini, JK hana mpango huo kwa sababu kuu mbili. Kwanza kuvunja baraza la mawaziri ni kumuweka kando waziri mkuu wa sasa, Mizengo Kayanza Peter Pinda na kuteua waziri mkuu mwingine.
Pili, atakuwa  anaongeza mzigo kwa serikali kwa kuwa waziri mkuu akiondoka madarakani huendelea kulindwa na serikali na kupokea stahiki zake mbalimbali.
                                                                     Mhe.Nchimbi.
NI NYERERE
Tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni Baba wa Taifa tu, hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiye aliyewahi kuwa na mawaziri wakuu wanne.
Alianza na Rashid Mfaume Kawawa, akafuata Edward Moringe Sokoine, Salim Ahmed Salim (baada ya kifo cha Sokoine) na Cleopa David Msuya.
                                                                 Shukuru Kawambwa.

AWAMU YA MWINYI
Katika awamu ya pili, Rais Ally Hassan Mwinyi, mawaziri wakuu walikuwa Joseph Warioba, John Malecela na David Msuya.
Katika awamu ya tatu ya Rais Benjamin William Mkapa kulikuwa na waziri wakuu mmoja tu, Frederick Tuluwayi Sumaye.

WAZIRI MKUU HADI 2015
Kwa sababu hiyo, chanzo kikasema kuwa Pinda ataendelea ‘kuula’ kwenye nafasi yake ya kuwa waziri mkuu wa Tanzania hadi mwisho wa muhula wa awamu ya nne, mwaka 2015.

WATAENDELEA KUPANGUA
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo hicho, JK na rais ajaye wataendelea kukumbwa na shinikizo la kupangua baraza la mawaziri kila wakati kutokana na mfumo wa madaraka uliopo sasa.
“Unajua mfumo wa sasa uko hivi; waziri anateuliwa na rais, katibu mkuu wa wizara pia anateuliwa na rais. Katibu mkuu wa wizara ana uwezo wa kumfukuza kazi mkurugenzi wa halmashauri bila waziri kujua, lakini waziri hana uwezo huo.
“Nguvu kubwa ya kazi ipo kwa makatibu wakuu ambao ndiyo watendaji wakubwa wa wizara. Kinachotokea ni kwamba kama wizara itampata waziri mwenye kusimamia sawa majukumu yake kiasi cha kutishia ulaji wa makatibu wakuu, atawekewa zengwe mpaka ang’oke.
“Ndiyo maana utakuta mawaziri kwenye wizara kila siku wanawajibika kisiasa lakini makatibu wakuu wapo tu. Ni mfumo mbaya wa kimadaraka hivyo JK atabadili kila siku, hata rais ajaye naye atakuwa katika harakati hizo,” kilisema chanzo hicho.

MAWAZIRI ZAIDI
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kunyetisha kwamba, wapo mawaziri ambao wanakalia kuti kavu na huenda wakang’olewa kabisa kutokana na utendaji kazi wao usioridhisha.

SHUKURU KAWAMBWA
Huyu anadaiwa kung’oka wakati wowote kutokana na madai ya walimu.
Chanzo kilisema kuwa Kawambwa pia anaponzwa na mfumo kwani kwa kawaida mwalimu anaajiriwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi lakini usimamizi wake unakuwa chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Ikadaiwa kuwa mwalimu anapandishwa cheo na Wizara ya Utumishi, lakini mshahara analipwa na Wizara ya Fedha, Mipango na Uchumi (hazina).
“Sasa mwalimu akipandishwa cheo na utumishi, nyongeza ya mshahara inatakiwa itoke hazina. Hazina nao wanakuwa hawana habari kwa sababu ya mawasiliano duni, matokeo yake mwalimu analia na mwajiri wake ambaye ni Wizara ya Elimu. Hili la walimu litamng’oa Kawamba,” kilisema chanzo.
                       Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo Tibaijuka.
ANNA TIBAIJUKA
Chanzo kilidai kwamba Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, mama Anne Kajumulo Tibaijuka naye yupo mguu pande, sawa kwa sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.
Mfano: “Wakulima wanaopakana na Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu, Manyara, wamekuwa wakilalamikia kitendo cha mazao yao kuunguzwa na mbolea hiyo, waziri ameshaambiwa akajibu atafuatilia, sasa atafuatilia mpaka lini?
“Kuna kamati iliundwa kufuatilia suala hili. Pia inadaiwa kuwa vigogo mbalimbali wa serikali wamejimegea maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro hivyo kusababisha migogoro isiyoisha kati ya wakulima na wafugaji wanaogombea ardhi kiduchu iliyobaki, huenda ikawa miongoni mwa mambo yatakayomng’oa madarakani Mheshimiwa Tibaijuka,” kilisema chanzo.
                                Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
CHRISTOPHER CHIZA
Huyu ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Wizara yake inakabiliwa na tuhuma ya kuzembea kwenye eneo la mashamba ya mpunga katika Kijiji cha Kapunga, Mbarali, Mbeya.
“Kuna kaburu mwekezaji alinunua shamba hilo lililokuwa la Nafco, hajalilima matokeo yake  analikodisha kwa wanakijiji vipandevipande. Sasa mtu ataitwaje mwekezaji wakati ni mbangaizaji tu, hii ni kashfa, wizara ipo na haisemi lolote.
“Naamini ripoti ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Peter Msolwa itaanika madudu yote haya,” kilisema chanzo.

WANAVYOTAKA WANANCHI
Risasi Jumamosi wiki iliyopita liliingia mitaani kusikiliza maoni ya wananchi juu ya watu wanaotakiwa kuwa mawaziri kushika nafasi zilizoachwa wazi.
Katika kila wananchi kumi, nane walitaka mawaziri na wizara zao wawe hivi:
Benard Membe, Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi. Asha-Rose Mtengeti Migiro (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Lazaro Samuel Nyalandu (Waziri wa Maliasili na Utalii) na Anne Kilango Malecela (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Wananchi hao walisema, Harrison George Mwakyembe na John Pombe Magufuli waendelee kwenye wizara zao  kwa vile utendaji kazi wao ni mzuri, hauna shaka huku wakitaka George Huruma Mkuchika awe Waziri wa Ulinzi.
“Ila Amos (Gabriel) Makalla awe waziri kamili wa habari, yule mama (Fenella Mukangala) apelekwe wizara nyingine. Waziri wa Mambo ya Ndani sisi wananchi tunamwona. Halafu yule mama anaitwa Joanista (Joackim) Mhagama aingizwe kwenye Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,” alisema mkazi wa Kijitonyama, Dar aliyejitambulisha kwa jina la Kadoda, fundi wa magari, Bamaga, Mwenge.

MOTO MKUBWA WAZUKA JANCO MOTEL JIJINI MBEYA USIKU WA KUAMKIA LEO

Moto mkubwa umezuka katika Hoteli ya Janco iliyopo Forest Mpya jijini Mbeya usiku wa kuakia leo. Chanzo cha moto huo hakijajulikana.