Stori: SHAKOOR JONGO NA IMELDA MTEMAKATIKA
staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji
Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’
alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
Peniela Mungilwa ‘Penny’.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake
Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu
wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na
‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.

Mmoja
wa wapangaji wa nyumba anayoishi Penny, aliliambia gazeti hili kuwa
msafara wa magari matatu ulifika hapo na kugonga mlango wakimuulizia
mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha Channel Ten.

“Walivyofika
sisi tulijua labda leo ni bethidei ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na
maua, keki, shampeni na kadi, walipomuulizia tukawaambia ametoka,
wakaacha mzigo huo wakisema apewe atakaporudi,” alisema shuhuda huyo.

Juu
ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi
yaliyomsuta na kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua mabwana wa rafiki
zake pamoja na dada zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea ujumbe
huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mtamboni.
No comments:
Post a Comment