Friday, September 13, 2013

Unaambiwa huyu ni mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani

4yearold_mayorb.jpgWRobert ‘Bobby’ Tufts hajaanza hata shule ya  Nursery ambayo huku Tanzania tunaifahamu kama chekechea au vidudu lakini tayari ameshajiwekea historia ya kuwa mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani .
Dogo huyo ameweza kuwa meya wa mji mmoja huko Minesotta akiwa na umri wa miaka mitatu pekee, unaambiwa ni Meya wa mji mdogo wa Dorset ulioko huko Minesotta Marekani na hii ni mara yake ya pili kuchaguliwa kuwa meya wa mji huo baada ya kupigiwa kura siku ya jumapili ambapo aliweza kushinda kipindi chake cha pili cha uongozi .
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert 'Bobby' Tufts.
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert ‘Bobby’ Tufts.
Mji huo una serikali ndogo inayoongozwa na meya huyo mdogo ambaye anaongoza idadi ya watu 220 ambao ni wakazi wa mji huo ambapo kama ilivyo kwenye manispaa yoyote, meya Bobby anaongoza serikali ambapo hufanya maamuzi yanayohusu bajeti ya matumizi ya mji wa Dorsett pamoja na masuala mengine nyeti kama ya kodi na makusanyo mengine ya mapato.
Mama mzazi wa Meya Robert Tufts, Emma Tufts anasema kuwa moja ya agenda za uongozi wa mwanaye ni kukusanya fedha kwa ajili ya taasisi ya misaada ya Ronald McDonald iliyoko Dorset eneo la Red River Valley Fargo Dakota ya Kaskazini pamoja na ujenzi wa kibao kipya cha kuwakaribisha wageni huko Dorset kwenye barabara zinazopakana na miji mingine.
4yearold_mayorc.jpgWTaarifa za Meya huyo mdogo kuliko wote duniani zimefika mpaka ikulu kwa Barack Obama ambae amempa Robert Tufts mwaliko maalum kwenye ikulu yake na ana mpango wa kumfanya kuwa mshauri wake maalum kwenye mfuko wake unaofahamika kama ObamaCare Foundation.

Mama amnyonga mwanae wa miezi 9


111111111111111111111111 Mara nyingi huwa tunasikia mama kamtupa mwanae baada ya kumzaa, lakini hii imekua mbaya zaidi baada ya mama kumyonga mwanae wa miezi tisa. Habari kutoka KTN inaeleza zaidi kuhusu hiki kisa.




Ratiba nzima ya movie kuanzia 13 hadi 19 September kwenye theater za Dar na Arusha ipo hapa


687883034_2108327899001_pain-and-gain-trailer-still
Wiki hii movie mpya inayoonyeshwa wiki hii kwenye theaters za hapa Tanzania ni Pain and Gain. Movie hii ni true story ambayo ilitokea huko Miami, angalia hapa trailer yake na ukaangalie kwenye theater uipendayo


1185935_10151699887733842_997317895_n
1239831_505685009505787_531302041_n
1208707_576530562408211_53189326_n 1229971_10151699879423842_134378913_n 1230027_10151699885198842_554494605_n


SERIKALI YAANDAA MAPENDEKEZO YA KUTUNGA SHERIA MPYA YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi akiwaeleza wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mapendekezo ya serikali kutunga sheria mpya ya kudhibiti dawa za kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Serikali imeandaa mapendezo ya kutunga sheria mpya ya kudhibiti dawa za kulevya nchini. Tatizo la matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya limekuwa kero nchini hasa kumaliza nguvu kazi ya taifa.
Hayo yamesemwa  na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za tume ya kuratibu dawa za kulevya jijini Dar Salaam.
Aidha amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na tatizo la matumizi ya dawa  za kulevya ambalo  huchangiwa na mambo mbalimbali yakiwemo; tamaa ya kutaka utajiri wa haraka na mmomonyoko wa maadili .
Amesema madhara ya dawa hizo ni makubwa  ikiwa ni pamoja na kuathiri afya za watumiaji , ongezeko la uhalifu na magonjwa ambukizi kama vile homa ya ini, kifua kikuu na UKIMWI.
Aliongeza kusema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada za kupambana na tatizo hilo kwa muda mrefu sana ikiwemo kufuta baadhi ya sheria zilizokuwa zikitumika tangu wakati wa ukoloni ambapo mwaka 1995 Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya dawa za kulevya [Sura 95] inayotumika hadi sasa ilitungwa.
Sheria hii ilianzisha Tume ya Kuratibu  Udhibiti wa  Dawa za Kulevya ambayo iko chini Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa lengo la kuratibu na kusimamia tatizo la Dawa za kulevya nchini
Tume hii imekuwa ikishirikiana na vyombo mbalimbali vya dola vinavyojihusisha na tatizo hili kama  vile Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Idara ya Uhamiaji, Idara ya Ushuru wa Forodha na Asasi za Kiraia.

Juma Kaseja atua Ndanda FC ya Mtwara

Juma Kaseja.
Na Nicodemus Jonas
KIPA namba moja wa Taifa Stars, Juma Kaseja dili lake la kwenda kuichezea FC Lupopo ya DR Congo halieleweki na kusisitiza kuwa ameamua kujiunga na timu ya Ndanda FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa ajili ya mazoezi ili kujiweka fiti kipindi hiki ambacho hana timu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaseja ambaye alimaliza mkataba wake na Simba msimu uliopita, alisema kabla ya kusafiri na timu ya taifa, alikuwa akifanya mazoezi na timu hiyo, ingawa anaendelea kufanya mazoezi kwa manufaa ya afya yake.
Aliongeza kuwa, suala la usajili wa Lupopo hapendi kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa yeye bado ni mchezaji huru, lakini baada ya Ndanda kuondoka kwenda Mtwara juzi Jumatano, amejikita zaidi kuendesha shughuli zake binafsi.
“Nimekuwa nikifanya mazoezi na Ndanda, lakini baada ya kuondoka, ninaendelea na shuguli zangu binafsi, siyo lazima kuzijua,” alisema Kaseja huku akiwa hayupo tayari kufafanua kwa undani juu ya usajili wake wa kwenda Lupopo.
Ndanda ilikuwa jijini Dar es Salaam ambapo ilicheza mechi za kirafiki dhidi ya Saigon ya Mwananyamala na Ruvu Shooting ya Pwani, ambapo itaanza kucheza mechi za Daraja la Kwanza keshokutwa Jumapili dhidi ya Friends Rangers kwenye Uwanja wa Nang’wanda, Mtwara.

HII NI BABA LAO!

Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
MDOSI au Kanjibai aliyefahamika kwa jina moja la Milah ambaye ni bosi wa kampuni moja ya ujenzi yenye makao yake Mwenge jijini Dar alinaswa chooni akiwa na mfanyakazi wake, John Carlos ‘Shabani’ (watu walimpachika jina la Shabani kutokana na Kanjibai wa kwenye Komedi) ikidaiwa walikuwa katika mazingira ya ulawiti, Ijumaa ‘Kubwa’ lina sinema yote.
...Choo walipokuwa wamejifungia Milah 'Kanjibai' na John Carlos ‘Shabani’.
Ishu hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wawili hao walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia usumbufu watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.
KISA KILIPOANZA
Siku hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers, Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo. Alisema:
“Jamani hebu njooni haraka hapa kwenye hii kampuni ya ujenzi ya… (jina lipo) iko hapa Mwenge. Kuna bosi wetu mmoja amejifungia chooni na mfanyakazi mwenzetu kwa zaidi ya robo saa sasa, sijajua nini kinaendelea humo ndani. Sisi wengine hapa matumbo ya kuendesha yametushika sijui tufanyaje?!”
Mtoa habari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuwaambiwa mapaparazi wetu waliompokelea simu wachukue Bajaj au Bodaboda ili kuwahi.
Sosi huyo kabla ya kukata simu aliweka wazi ramani ya kufika kwenye choo hicho na kusisitiza kwamba muhimu kuwahi kwa sababu huenda wanagombana.
MAPAPARAZI WAWASHA PIKIPIKI
Kufuatia msisitizo huo, mapaparazi wetu makini  waliwasha pikipiki zao, kila mmoja na yake na kushika njia kuelekea eneo la tukio.
Hata hivyo, kwa kuamini wanaweza kukutana na lolote, waliona ni vyema kwanza kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge ambapo walipewa askari wawili kuelekea eneo la tukio.

...Ndani ya choo walimokutwa.
ENEO LA TUKIO SASA
Timu hiyo iliwasili kwenye eneo la tukio. Mlango wa choo hicho ulikuwa umefungwa lakini kwa mara moja tu haikuwa rahisi kugundua kama ulifungwa kwa funguo au kawaida tu.
 Afande mmoja alijitolea kugonga mlango wa choo hicho ili kupima ushirikiano utakaotolewa na wawili hao au mmoja wao.
Sauti iliyoonekana ni ya Kanjibai kutokana na kushindwa unyoofu wa lugha ya Kiswahili ilisikika ikiuliza:
“Nani wewee… taka nini huku?”
...Wakiwa chini ya ulinzi.
Afande: Sisi ni askari polisi, fungua haraka tunajua mko wawili humo ndani, fungua.
Kanjibai: Subiri kidogo.
Baada ya dakika kadhaa ambazo mapaparazi wetu hawakuzifuatilia, mdosi huyo alifungua mlango na kukutwa akiwa na ‘Shabani’.
WALICHOKUWA WAKIKIFANYA CHOONI
Katika maswali ya harakaharaka nje ya choo hicho kila mmoja alisema la kwake ambalo aliliamini linaweza kumchomoa kwenye skendo hiyo mbaya.
‘Shabani’ alisema yeye aliingia kwenye choo hicho baada ya kuitwa na bosi wake huyo ambapo alishindwa kumkatalia kwa kuogopa kupoteza ajira yake na kama inavyojulikana maisha ya Dar bila kazi ni ngumu kuyamudu.
...Mafuta aliyokutwa nayo Kanjibai ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’.
Alipoulizwa walichokuwa wakikifanya ndani ya choo hicho, Shabani alibaki akiwatumbulia macho maafande, wakati mwingine mapaparazi wetu.
Kwa upande wake Kanjibai alipotakiwa kujieleza kisa cha kuingia chooni na mfanyakazi wake, alisema alimuomba wazame humo ili akamnyoe. Yaani Kanjibai alitaka kunyolewa.
IKAFIKA ZAMU YA KUPELEKWA KITUONI
Afande mmoja aliamuru wawili hao wapelekwe kituo cha polisi, lakini kabla ya kuanza safari, mdosi huyo aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali na kutoa vitu vyake kadhaa na kuwakabidhi wadosi wenzake waliofika ‘kumsaidia’ muda mfupi baada ya kunaswa.
Halafu aliingiza mkono kwenye mfuko mwingine na kutoa mafuta aina ya KY (pichani) ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’ lakini askari alimwambia mafuta hayo yanatakiwa kituoni kwa ajili ya ushahidi hivyo asiwape nduguze.
Breki ya kwanza ilikuwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mwenge ambapo baada ya mahojiano mafupi walihamishiwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ ambapo walihojiwa zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Monday, September 2, 2013

Uzuri wako Jux (Official Video)



MZEE GURUMO: DIAMOND MUNGU ATAKULIPA

MZEE GURUMO: DIAMOND MUNGU ATAKULIPA

Makala: Shakoor Jongo na Musa Mateja
Habari ya mjini wikiendi iliyopita ilikuwa ni juu ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumzawadia gari nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu muziki hivi karibuni, Mzee Muhidin Gurumo aliyekuwa akiitumikia Msondo Music Band.
Tukio hilo lililoibua maneno kibao lilijiri ndani ya Serena Hotel, Posta jijini Dar wakati Diamond au Sukari ya Warembo akizindua video ya wimbo wake mpya wa My Number One na kuhudhuriwa na raia wa kada mbalimbali wakiwemo mastaa wa muziki, filamu, wakurugenzi wa makampuni na watu wa kawaida.
Wakati Diamond akimkabidhi Mzee Gurumo ufunguo wa gari hilo aina ya Fan Cargo lenye thamani ya Sh. milioni 6 alisema:
“Nikikutajia jina la Muhidin Gurumo, basi utajua namzungumzia nani. Ni nguli wa muziki wa dansi nchini Tanzania.
“Takriban wiki imepita tangu kusikika kwa habari za kweli kuhusu kustaafu muziki kwa Mzee Gurumo, binafsi sikuwahi kukutana naye hadi leo hii nilipokutana naye kwenye uzinduzi wa video yangu.
“Nilimualika mzee huyu kwa mapenzi yote, nilisikia juzi pia akisema amekuwa akipendezwa na staili ya muziki wangu na kucheza pia, hayo ni mojawapo ya mambo yaliyonivutia kutaka kumuona mzee huyu.
“Nilipitia kwenye mitandao mingi huku ikiandikwa kuwa kutokana na kazi ya Mzee Gurumo ameweza kuwa kwenye fani zaidi ya miaka 50 lakini hakuwahi kubahatika hata kuwa na baiskeli.
“Jambo hili lilinigusa na kuniumiza moyoni, kuona nguli kama huyu wa muziki ananena vile na kuomba msaada, binafsi leo usiku nimemtunuku gari jipya mzee Gurumo kwenye uzinduzi wa video yangu.
“Nimeamua kutoa kwa moyo mmoja na kwa mapenzi yangu yote kwa mzee wangu.”
Baada ya kukabidhiwa funguo hizo na kutoa shukrani zake kwa kumuombea Diamond baraka kwa Mungu, wanahabari wetu walitaka kusikia anazungumziaje tukio hilo ambapo alisema: “Diamond Mungu atamlipa. Ni kweli nimestaafu bila baiskeli lakini yeye kanipa gari. Mungu ambariki sana.”

GARAMA
Kwa mujibu wa Diamond, video hiyo ambayo itaanza kuruka hewani leo, imetengenezwa na Ogopa Djs nchini Afrika Kusini na imegharimu dola za Kimarekani 30,000 (zaidi ya Sh. milioni 48) huku uzinduzi huo ukigharimu Sh. milioni 18. Haijawahi kutokea Bongo!

WEMA HASIKII kwa Rommy Jonson.

WEMA HASIKII

Na Gladness Mallya
LICHA ya kunaswa katika matukio tofauti, Wema Sepetu hasikii. Safari hii imenaswa picha inayomuonesha akimshushia busu motomoto jamaa anayefahamika kwa jina la Rommy Jonson.
Wema Sepetu akimbusu Rommy Jonson.
Picha hiyo ambayo inamuonesha Wema akiwa anambusu jamaa huyo katika pozi lenye hisia kali za kimalovee, imenaswa juzikati katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo wadau mbalimbali walioiona kwa mara ya kwanza, walitoa maoni yao.
“Mh! Jamani Wema sasa amezidi hata huyu naye? Kama ni picha ya kawaida kwa nini aoneshe hisia za kimalovee kiasi hiki? Kuna kitu,” alihoji mdau mtandaoni ingawa Wema hakujibu chochote.

NI KWELI WANAWAKE WAMEWAZIDI WANAUME KWA MAMBO HAYA 10?

NI KWELI WANAWAKE WAMEWAZIDI WANAUME KWA MAMBO HAYA 10?

1. Wana Nguo Nyingi Kuliko Wanaume.
2. Wanafahamu Nani Ni Baba Halisi Wa Watoto Wao.
3. Ni Wepesi Kupenda Na Wakipenda Hupenda Kweli.
4. Wanaoga Mara Nyingi Zaidi Kwa Siku.
5. Wana Huruma Sana Ingawa Mara Nyingi Huwa Inawaponza.
6. Wana Uwezo Wa Kubadilisha Tabia Ya Mwanaume Muda Wowote.
7. Wana Uwezo Wa Kuishi Na Kupendeza Bila Kuwa Na Kazi Wala Biashara Yoyote.
8. Kwao Nywele Na Kucha Ndo Vitu Vya Kwanza Kufikiria Wakitaka Kutoka.
9. Wana Uwezo Wa Ku-Pretend Kwa Muda Mrefu Zaidi Hasa Kwenye Mapenzi.
10.
Wanaujua uchungu wa mwana sana.
    
Tupia Nyingine Unayodhani Nimeisahau...

MTANDAO WA UNGA WANASWA

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard Jeremiah Monyo aliyekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
MTANDAO hatari wa unga nchini Tanzania umeshanaswa, kwa sasa unafanyiwa kazi kwa kasi na Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, chini ya kamanda wake, Godfrey Nzowa.
Habari njema kuhusu kunaswa kwa mtandao wa unga, zinakuja baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kufanya kazi nzuri na kuwataja watu ambao inadaiwa walihusika katika kupitisha madawa ya kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Madawa ya kulevya.
Sekeseke kuu ni kukamatwa kwa Watanzania wawili, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye ni mwanamitindo na Melisa Edward, nchini Afrika Kusini, wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine, yenye uzito wa kg 120, Julai 5, mwaka huu.
Swali kwamba walipitaje JNIA lilijibiwa na Mwakyembe Jumamosi iliyopita, akafafanua namna Mfumo wa Kamera za Usalama (CCTV), zilivyonasa ‘uhuni’ uliofanyika, hivyo akawataja watumishi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (TAA), Yusuf Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana kuhusika, akaagiza wafukuzwe kazi na polisi kuwakamata.
Baada ya Mwakyembe, moto unaendelea kuwaka na uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mtandao ulionaswa na Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, unagusa mikoa yote nchini.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
Katika mtandao huo, siri kubwa iliyovuja ni majina na jinsi biashara hiyo haramu inavyoendeshwa mkoa kwa mkoa, wilayani mpaka mitaani, vilevile wanamichezo na wasanii mbalimbali ambao imeshabainika kwamba wengi wao wanatumika kusafirisha unga.
Imebainika kwamba mtandao huo, uligundulika baada ya watu 2,075 kukamatwa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu (baadhi yao, picha zao zinaonekana ukurasa wa mbele).
“Watu tuliowakamata kimsingi ni wale wanaotumwa tu. Sasa wale ndiyo wamewataja mabosi wao, wameeleza siri kubwa,” alisema Kamanda Nzowa na kuongeza:
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.
“Haikuwa kazi rahisi, tulitumia mbinu za kiaskari kuwafanya waeleze ukweli. Wamesimulia biashara hiyo inavyofanyika, jinsi watu wenye fedha wanavyowatumia vijana kusafirisha mizigo.
“Tulichobakiza sasa ni kuwakamata wahusika na kuusambaratisha mtandao wenyewe. Hata sasa tunachokifanya ni kupambana na huo mtandao wenyewe, mwisho tutausambaratisha kabisa.”
NI MWAKA WA VITA NZITO
Nzowa, alisema kuwa mwaka huu umeonekana kuwa na vita nzito kwa sababu kuna lindi kubwa la watu ambao wamejiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya licha ya wengi kukamatwa na hata baadhi yao kunyongwa katika nchi za China na Pakistan.
Alisema madawa ya kulevya yenye uzito wa kilo 16,824 (tani 16.8) yamekamatwa kati ya kipindi cha Januari na Juni, mwaka huu, idadi ambayo ni kubwa kuliko vipindi vyote vilivyopita.
Melisa Edward
Alifafanua kwamba wingi huo usitafsiriwe tu kwamba biashara ya madawa ya kulevya inatanuka nchini, isipokuwa itazamwe kwa jicho la pili kwa upana wake jinsi mapambano dhidi ya biashara hiyo yalivyochochewa makali.
“Udhibiti umekuwa mkubwa sana. Isichukuliwe tu kwamba biashara inazidi kushika kasi, hapana, haya ni matunda ya kazi ya udhibiti ambayo inafanyika. Pengine huko nyuma walikuwa wanapishana kwa wingi zaidi lakini mapambano yalikuwa dhaifu, kwa hiyo wafanyabiashara hiyo haramu walikuwa wanajitanua tu.
“Ni wajibu wa kila mtu kumwambia mwenzake aachane na hii biashara, tunapomkamata na ushahidi, hapo anakuwa amekwenda na maji,” alisema Nzowa.
Akichambua zaidi, Nzowa alisema takwimu za madawa ya kulevya aina ya heroin zilizokamatwa katika kipindi hicho ni kilo 30 na washitakiwa ni 45, kati yao wanawake ni wanne.
Alisema, cocaine walikamata kilo nne na watuhumiwa ni 18 ambao ni wanaume watupu na dawa aina ya ephedrine walikamata kilo 12 mshitakiwa ni mmoja mwanaume na bangi ilikamatwa kilo 9,999 na watuhumiwa ni 1,478,  kati yao wanawake ni wawili.
Aliongeza kuwa licha ya kukamata bangi, polisi waliweza kuharibu ekari 300 za mmea huo katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mara wilayani Tarime.
Baadhi ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya
Kamanda Nzowa akaongeza kwamba polisi wanafanya kazi hiyo nzuri kwa kushirikiana na raia wema.
“Hivi sasa tuko makini sana kwa wasanii na wanamichezo wanaotaka kusafiri kwenda nje ya nchi kwa sababu tumegundua kuwa wanatumika kutokana na umaarufu wao,” alisema Nzowa.
Akifafanua zaidi, kamanda huyo alisema wana taarifa kwamba hivi sasa kuna dawa za kulevya za majimaji, hivyo wanaofikiria kusafirisha hizo kwa njia hiyo wanapaswa kujua kuwa watagundulika.
“Hii ni vita ambayo kila anayelitakia mema taifa hili anapaswa kushiriki kupambana na dawa za kulevya,” alisema Kamanda Nzowa.
KWA NINI VIJANA WENGI WANAKIMBILIA UNGA?
Mtafiti maarufu na mwelimishaji wa maisha ya vijana na jamii kwa jumla, James Mwang’amba, alisema kuwa vijana wengi wanaingia katika wimbi la biashara ya madawa ya kulevya kwa sababu ya kukata tamaa.
“Ukifuatilia maisha ya vijana kwa sasa, utagundua kwamba wengi wao wamekata tamaa. Wanahisi hawana njia ya kutoka kimaisha ndiyo maana wanaona fursa yoyote inayokuja mbele yao inafaa hata kama ni hatari.
“Kila mtu anatamani sana maisha ya juu, awe na kipato kikubwa, sasa kwa vile haoni njia nzuri za kufikia ndoto zake, anaamua kujiingiza kwenye usafirishaji wa madawa ya kulevya ili apate fedha za haraka ili naye awe mtu fulani,” alisema Mwang’amba na kuongeza:
“Tatizo kubwa ni hii tofauti ya kipato. Kuna tofauti kubwa sana kati ya wenye nacho na wasio nacho, hii ni hatari sana. Sasa jamii kwa vijana ni hatari zaidi kwa sababu damu inachemka na kuona kila kitu ni rahisi kufanya.
“Hakuna sababu nyingine kwa nini vijana wengi wanakuwa wauza unga, ukweli ni tamaa ambayo inachochewa na hasira ya kuwa na maisha duni wakati wanawaona wengine wakiwa matajiri wakubwa.”

AJILIPUA KWA PETROLI BAADA YA MUME KUOA MKE WA PILI

Na Victor Bariety, Geita
MWANAMKE mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mkoani  Geita amenusurika kifo baada ya kujimwagia mwilini mafuta ya petroli kisha kujilipua baada ya mumewe kuoa mke wa pili.  
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo, Anastazia Kubezya (28) Agosti 8 mwaka huu aliamua kujimiminia petroli mwili mzima kabla ya kuchukua kiberiti na kujilipua, hali iliyosababisha  akimbizwe katika Hospitali ya Geita alikolazwa katika wodi namba saba kwa matibabu.
Akizungumza na gazeti hili, Consolata Raphael ambaye ni dada wa majeruhi huyo alidai kuwa chanzo cha mdogo wake huyo kufikia hatua ya kutaka kutumia njia hiyo ya mkato kwa lengo la kujiua ni wivu wa mapenzi.
Consolata alisema: “Siku ya tukio shemeji yangu George Kubezya (mume wa majeruhi), alifika nyumbani kwa mdogo wangu wa kiume akidai kuwa mkewe huyo anatishia kujiua baada ya kuoa mke wa pili.
“Tukiwa tunaendelea kujadiliana mara alitokea mkewe Kubezya akiwa na viatu vya mwanaye mdogo akamkabidhi mdogo wetu mwingine aitwaye Rozalia akamwambia mpatie mwanaye kwa kuwa anaondoka na hajui atarudi lini.
“Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka na niliwasiliana na ndugu yetu mwingine aitwaye Elizabeth aliyesema Anastanzia alipita kwake akiwa na chupa ikiwa na petroli na walipojaribu kumkimbiza alipotelea gizani.
“Kati ya saa 4 na saa 5 usiku Eliza na wenzake walisikia mtu akilia nje ya nyuma yao na baada ya kutoka nje walikuta Anastanzia akiwa tayari amekwisha jilipua moto, walipomhoji alidai amefanya hivyo ili afe kutokana na mumewe kumuolea mke mwenza na kumleta kwenye nyumba waliyoijenga yeye na mumewe,”alisema Consolata.
Hata hivyo juhudi za kumpata mumewe kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda baada ya kile kilichoelezwa kuwa alitoroka muda mfupi baada ya kumfikisha mkewe hospitalini.
Gazeti hili lilifika hospitalini hapo na kukuta mwanamke huyo aliyelazwa wodi namba nane akiwa anauguzwa chini ya ulinzi wa polisi ili akipona afikishwe mahakamani kwa kosa la kujaribu kujiua.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Adam Sijaona akizungumzia hali ya majeruhi huyo alisema bado si nzuri na wanafanya mpango wa kumhamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.




Number one - Diamond (Official Video)


MARLAW BESTA WAPATA MTOTO

Lawrence Marima ‘Marlaw’ na mkewe Besta Prosper.
BAADA ya kuishi kwenye ndoa kwa muda mrefu hatimaye wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Lawrence Marima ‘Marlaw’ na mkewe Besta Prosper wamejaaliwa kupata mtoto wa kiume.
Kikizunguza na Ijumaa kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, chanzo makini ambacho kiko karibu na wanandoa hao kilisema kuwa wamekuwa wakiweka usiri mkubwa wa maisha yao hasa katika hilo la mimba na hatimaye Agosti 27, mwaka huu Besta alifanikiwa kuitwa mama.
Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Marlaw ambapo alikiri kupata mtoto wa kiume lakini hakuwa tayari kuelezea zaidi akidai muda wa kufanya hivyo bado.
“Kwa sasa bado ni mapema sana kuzungumzia suala la mke wangu kujifungua kwa undani lakini ni kweli tumepata mtoto wa kiume. Mengine muda ukifika nitaongea,”alisema Marlaw.


WANAWAKE WOTE SOMENI HABARI HII...


Pili alijifungua mapacha hao saa 1:00 asubuhi ya Agosti 18, 2013, nyumbani kwake na baadaye kupelekwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar baada ya watoto kuonekana si wa kawaida.
Kufuatia matukio kama hayo, Ijumaa Wikienda lilichimba kwa undani ili kubaini nini husababisha wanawake kubeba ujauzito wenye matokeo ya mapacha walioungana au mtoto mmoja kulemaa kiungo chochote cha mwili.
Mtaalam mmoja aliyesomea mambo ya afya ya uzazi ambaye aliomba hifadhi ya jina, ndiye aliyefunua siri hii nzito ambayo wanawake wengi nchini hawaijui isipokuwa kwa kusoma habari hii leo.
Mtaalam huyo alivitaja vidonge maarufu kwa matibabu ya tumbo la kuendesha viitwavyo Flagyl au Metronidazole kuwa ndivyo vinavyosababisha matatizo hayo.
Alisema vidonge hivyo ni hatari mno kwa afya ya mama mjamzito, hasa kwa mtoto aliye tumboni ambaye anatarajwa kukua na kutoka akiwa amekamilika.
“Wanawake wajawazito, hasa wakiwa wa miezi mitatu ya mwazo, hawatakiwi kabisa kutumia vidonge hivi aina ya Flagyl.
“Hivi vidonge ndivyo husababisha tatizo hili la watoto mapacha kuzaliwa wameungana, kitaalam tunaita Siamese Twins.
“Unajua kwa kawaida mimba huanza kuwa binadamu kamili miezi mitatu tu ya mwanzo, kitaalam tunaita First Trimester ambapo kila kitu kinachopaswa kuwa kiungo cha mwilini hufanyika.
“Baada ya hapo mpaka mwezi wa tisa ni kukua kwa viungo hivyo.
“Katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwanzo kuelekea miezi mingine hadi tisa, mwanamke akitumia Flagyl kwa sababu viungo vinakuwa, ni rahisi kwa watoto kuungana au kuzaliwa wakiwa na ulemavu wowote,” alisema mtaalam huyo.
Mtaalam huyo alisema vidonge hivyo ambavyo hupatikana kirahisi kwenye maduka ya madawa (famasi) hutumiwa zaidi kwa matatizo ya tumbo, hasa la kuendesha.
“Kwa nchi za wenzetu (zilizoendelea), ili mtu auziwe vidonge ambavyo vinaweza kuleta madhara lazima awe na karatasi ya maelekezo ya matumizi kutoka kwa daktari.
“Hakuna daktari wa kweli hata mmoja atakayekubali kumpa Flagyl mwanamke mjamzito, kwa sababu anajua madhara yake,” alisema.
Kuhusu Pili Hija, mapacha wake walifanyiwa upasuaji Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo cha Tiba ya Mifupa (Moi) chini ya daktari wa upasuaji wa watoto, Dk. Zaituni Bokhary.
Mtoto aliyebaki ni yule aliyezaliwa akiwa na kichwa, ilibidi kumuondoa asiye na kichwa kwa sababu asingeweza kuwa binadamu kamili.
Dokta Bokhary alisema hii ni mara ya kwanza kwa jambo hilo kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Mara ya mwisho lilitokea mwaka 1984.


Sunday, September 1, 2013

GIROUD APELEKA KILIO TOTTENHAM

 Santi Cazorla wa Arsenal akikwaana na Paulinho (kushoto).
 
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud leo amepeleka kilio Tottenham baada ya kuipatia timu yake bao la ushindi katika dakika ya 23 ya mchezo. Giroud aliunganisha krosi safi kutoka kwa Theo Walcott na kuwafanya vijana wa Wenger kuibuka kifua mbele na pointi tatu dhidi ya mahasimu wao Tottenham Hotspur. Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Emirates jijini London na Arsenal wameshinda bao 1-0.
Katika mtanange huo, vikosi vilikuwa kama ifuatavyo:
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Wilshere (Flamini 43), Rosicky (Monreal 78), Cazorla, Walcott (Sagna 90)
Tottenham: Lloris; Walker, Dawson, Vertonghen, Rose; Capoue (Sandro 74), Paulinho; Townsend (Lamela 74), Dembele (Defoe 68), Chadli; Soldado





DIAMOND AFUNGUKA KUTENGENEZA NUMBER ONE AFRIKA KUSINI



Msanii Mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka na kuelezea sababu za kuamua kufanya video ya ngoma yake mpya ya Number One nchini Afrika Kusini. Diamond aliyetumia kiasi cha Dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya shilingi milioni 48 za Kitanzania kutengeneza video hiyo, ameeleza hayo katika video aliyoiweka kwenye Blog yake inayoonyesha maandalizi ya utengenezaji wake. Diamond anasemaa ameamua kuifanyia nchini Afrika Kusini ili kuwa na kitu tofauti, kupata mandhari, washiriki na radha tofauti.
ANGALIA BEHIND THE SCENE NA DIAMOND MWENYEWE AKIELEZEA KUHUSU VIDEO YA NUMBER ONE HAPA CHINI: