Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za tume ya kuratibu dawa za kulevya jijini Dar Salaam.
Aidha amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya ambalo huchangiwa na mambo mbalimbali yakiwemo; tamaa ya kutaka utajiri wa haraka na mmomonyoko wa maadili .
Amesema madhara ya dawa hizo ni makubwa ikiwa ni pamoja na kuathiri afya za watumiaji , ongezeko la uhalifu na magonjwa ambukizi kama vile homa ya ini, kifua kikuu na UKIMWI.
Aliongeza kusema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada za kupambana na tatizo hilo kwa muda mrefu sana ikiwemo kufuta baadhi ya sheria zilizokuwa zikitumika tangu wakati wa ukoloni ambapo mwaka 1995 Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya dawa za kulevya [Sura 95] inayotumika hadi sasa ilitungwa.
Sheria hii ilianzisha Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya ambayo iko chini Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa lengo la kuratibu na kusimamia tatizo la Dawa za kulevya nchini
Tume hii imekuwa ikishirikiana na vyombo mbalimbali vya dola vinavyojihusisha na tatizo hili kama vile Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Idara ya Uhamiaji, Idara ya Ushuru wa Forodha na Asasi za Kiraia.
No comments:
Post a Comment