Lawrence Marima ‘Marlaw’ na mkewe Besta Prosper.
BAADA ya kuishi kwenye ndoa kwa muda mrefu hatimaye wasanii wa muziki
wa kizazi kipya, Lawrence Marima ‘Marlaw’ na mkewe Besta Prosper
wamejaaliwa kupata mtoto wa kiume.Kikizunguza na Ijumaa kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, chanzo makini ambacho kiko karibu na wanandoa hao kilisema kuwa wamekuwa wakiweka usiri mkubwa wa maisha yao hasa katika hilo la mimba na hatimaye Agosti 27, mwaka huu Besta alifanikiwa kuitwa mama.
Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Marlaw ambapo alikiri kupata mtoto wa kiume lakini hakuwa tayari kuelezea zaidi akidai muda wa kufanya hivyo bado.
“Kwa sasa bado ni mapema sana kuzungumzia suala la mke wangu kujifungua kwa undani lakini ni kweli tumepata mtoto wa kiume. Mengine muda ukifika nitaongea,”alisema Marlaw.
No comments:
Post a Comment