Msanii Mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Nasibu Abdul 'Diamond
Platnumz' amefunguka na kuelezea sababu za kuamua kufanya video ya ngoma
yake mpya ya Number One nchini Afrika Kusini. Diamond aliyetumia kiasi
cha Dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya shilingi milioni 48 za Kitanzania
kutengeneza video hiyo, ameeleza hayo katika video aliyoiweka kwenye
Blog yake inayoonyesha maandalizi ya utengenezaji wake. Diamond anasemaa
ameamua kuifanyia nchini Afrika Kusini ili kuwa na kitu tofauti, kupata
mandhari, washiriki na radha tofauti.
ANGALIA BEHIND THE SCENE NA DIAMOND MWENYEWE AKIELEZEA KUHUSU VIDEO YA NUMBER ONE HAPA CHINI:
No comments:
Post a Comment