Monday, February 25, 2013

DIDA ANASWA NA VIATU VYENYE SILAHA

MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida,’ hivi karibuni alinaswa akiwa amevalia kiatu ambacho kina silaha.


Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa Kinondoni.


RAY AKONGOROKA


MWIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ amezua hofu kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake baada ya kukongoroka ghafla akihisiwa anaumwa, Ijumaa Wikienda limemfuatilia hatua kwa hatua.


KWENYE ‘BETHIDEI’ YA BATULI
Wiki kadhaa zilizopita paparazi wetu alishtuka alipomuona Ray kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji sistaduu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ndani ya Hoteli ya Shamoll iliyopo Sinza ya Lion, Dar akiwa amekongoroka na kuibua maswali kwa wahudhuriaji.
Akiwa ukumbini hapo, minong’ono ilienea kuwa Ray alionekana kukondeana katika kipindi kifupi huku baadhi ya watu wakisikika wakiulizana kulikoni kwani alikuwa meza moja na bonge la mtu, Jacob Steven ‘JB’ hivyo kumfanya kuonekana mdogo mno.


Vincent Kigosi ‘Ray’ alivyokuwa mwaka jana.

VIWANJA VYA LEADERS
Akiwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki iliyopita, Ray aliibua mshtuko kwa mara nyingine hadi jamaa mmoja anayedhaniwa kutokuwa vizuri kichwani kumfuata na kumuwakia akimuuliza kwa hasira kuwa kulikoni akondeana kiasi hicho.

UZINDUZI WA WEMA
Kwa mara nyingine, Ray alizua hofu alipohudhuria kwenye uzinduzi wa ofisi ya Wema Sepetu uliofanyika maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alipoingia watu walipigwa butwaa wakimtazama na wengine kumuonea huruma wakidhani anaumwa.

IJUMAA WIKIENDA LATAKA MAJIBU
Kwa nyakati tofauti, wanahabari wetu walizungumza na Ray ambaye alitoa majibu ya kukinzana na kuzidi kutia shaka.
Ray alimwambia mmoja wa waandishi wetu kuwa kilichosababisha akongoroke kiasi hicho ni mazoezi makali anayofanya ili kupunguza unene.
Katika majibu mengine kwa mwandishi wetu mwingine, Ray alidai kuwa anafanya ‘dayati’ ikielezwa kuwa ikishafika saa 11:00 jioni ndiyo mwisho wake wa kula msosi lengo likiwa ni kupunguza mwili uliokuwa umefumuka.
Kama mtu alimuona Ray kwenye Matamasha ya Serengeti Fiesta mwishoni mwa mwaka jana, akikutana naye lazima amtazame mara mbilimbili hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni kutafuta undani wa madai kuwa huenda staa huyo mkubwa anaumwa kufuatia majibu tofauti aliyoyatoa.


WEMA, DIAMOND FEDHA INAONGEA


WAKATI Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akionesha jeuri ya fedha kwa kufungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliogharimu Sh. milioni 260 hivyo kwa pamoja kuthibisha msemo kuwa fedha inaongea, Ijumaa Wikienda lina data kamili.


Wema akiwa ofisini kwake.…

Monday, February 18, 2013

KICHEKESHO kutoka kwa Masanja Mkandamizaji


Jamaa mmoja alizamia semina ya wasomi iliyokuwa inafanyika Ubungo Plaza. Ukafika muda wa watu kujitambulisha. Wa kwanza akaanza: Naitwa John, niko UDOM mwaka wa pili nasoma Sheria. Wa pili: Naitwa Stella, niko UDSM mwaka wa tatu nasoma Public Relations. Jamaa wa tatu mzamiaji akisuasua sana huku akijishtukia: Naitwa Paulo, niko TANESCO mwaka wa tisa nasoma Mita.
Like ·  ·  · 23 minutes ago · 

LOWASSA RAIS 2015



SASA ni wazi kuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa ndiye atakuwa rais wa awamu ya tano Tanzania mwaka 2015, kutokana na ukweli kwamba kambi zinazosigana ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), zinaonekana kupwaya huku yake ikiwa na watu wenye nguvu kisiasa na kiuchumi, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kusema


Katika vuguvugu la nani awe rais mwaka 2015, uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa tangu uchaguzi ndani ya chama hicho mwaka jana, Lowassa anaonekana kupata mafanikio zaidi kisiasa, ikilinganishwa na mahasimu wake, Benard Membe na Samuel Sitta ambao wanatajwa kutaka kuwania urais baada ya Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake.
Kama ilivyo kwa Lowassa, Sitta ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Membe mwenye kofia ya Uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nao wamekuwa wakidaiwa kuwa na makundi katika harakati za kuusaka urais, japokuwa wenyewe hawajathibitisha.
Uchunguzi huo umeonesha kuwa Lowassa ana mtandao wenye nguvu kisiasa na wachunguzi wa mambo wanasema hata kama vikao vya juu vitamkata jina, kundi lake likiamua nani awe rais uwezekano wa mtu huyo kupita ni mkubwa.
Katika uchaguzi wa chama katika mikoa, wafuasi wengi wa Lowassa walipeta ukilinganisha na makundi mengine yanayotajwa katika kinyang’anyiro cha urais.
Baadhi ya wasomi nchini, walitofautiana kimtazamo kuhusu chaguzi hizo ndani ya CCM. Mhadhiri maarufu wa UDSM, Dk. Benson Bana alisema CCM katika chaguzi hizo imeonesha kwamba hakuna kiongozi yeyote mwenye hati miliki ya chama hicho kwani mtu yeyote anaweza kuingia na kuondoka kwenye chama hicho.
Naye Kisena Mabuba ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alisema: “Tofauti na matarajio ya wengi kuwa CCM ingemeguka, mimi ninachokiona hapa kundi lililobaki na nguvu ni lile la mwenyekiti mwenyewe. Kundi moja limefutwa kabisa na mengine yameshindwa kupata nguvu za kutosha.”

TASWIRA ZA MKUTANO WA CCM KATIKA VIWANJA VYA PILE TEMEKE JIJINI DAR


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.…

Beauty and A beat --- justin bieber ft Nick Minaj




JOKATE ATOA BARAKA KWA DIAMOND


BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Jokate Mwegelo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.






Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na demu wake mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.


Life before Computer kutoka kwa Masanja Mkandamizaji


Life before Computer:

.
.
.
.
.

-Window was a square hole in a room.

-Application was something written in paper.

-Mouse was an animal.

-Keyboard was a Piano.

-File was a important office material.

-Hard Drive was a uncomfortable road trip.

-Cut was done with Knife n Paste was done with Glue.

-Web was spider's home.

-Virus was flu.

-Apple and Blackberry were just fruits

Like ·  ·  · about an hour ago ·

Sunday, February 17, 2013

SAJENTI TAABAN, MATUMAINI BADO HANA MATUMAINI


HUKU mwigizaji Husna Idd ‘Sajenti’ naye akiwa taaban kwa kuzidiwa baada ya kukimbizwa hospitalini na kulazwa, bado hali ya msanii mwenzake, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ haina matumaini akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar.

SAJENTI
Habari zisizokuwa na shaka zilizotua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita zilieleza kuwa Sajenti alizidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake ambapo Ijumaa iliyopita alikimbizwa katika Hospitali ya Kinondoni kwa Dokta Mvungi, Dar akiwa hoi kwa ajili ya vipimo na matibabu.
Ijumaa Wikienda lilifika hospitalini hapo na kumkuta msanii huyo akiwa katundikiwa ‘dripu’ ambapo kwa mujibu wa data za ndani, vipimo vilionesha kuwa alikutwa na malaria na homa ya matumbo hivyo kumfanya aishiwe nguvu.
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Sajenti alikuwa hajaruhusiwa kutoka hospitalini.



Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar.
MATUMAINI
Wakati Sajenti akiombewa na wasanii wenzake arejee katika hali yake ya kawaida, kwa upande wake Matumaini alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kugunduliwa kuwa na tatizo la figo, ini na miguu kuwaka moto.
Naye hali yake bado siyo nzuri tangu aliporejeshwa nchini akitokea Msumbiji akiwa taaban wiki mbili zilizopita.


Scene ya mwisho alioicheza marehemu sharo millionea na kitale


ULIWAHI KUWAZA KAMA WEMA SEPETU SIKU MOJA ANGEKWAMBIA HII NDIO OFISI YAKE MPYA? CHEK PICHAZ
























KAMA HUKUSIKILIZA TOP 20 YA CLOUDS FM FEB 17 2013, LIST IKO HAPA



No. 20 – Butterfly – Q Chief
No. 19 – Nataka Kulewa – Diamond
No. 18 – Mahakama Ya Mapenzi – Linex
No. 17 – Alingo – P Square
No. 16 – Mtima Wange – Amin – Linnah
No. 15 – Dear Gambe – Young Killa
No. 14 – Nipende Kama Nilivyo – Mr Blue
No. 13 – Pete – Ben Pol
No. 12 – Wazo La Leo – Stamina
No. 11 – My Everything – Alikiba
No. 10 – 2030 – Roma Mkatoliki
No. 9 – Kidela – Abdukiba – Alikiba
No. 8 – Dear God – Kala Jeremiah
No. 7 – Walaghai – Bonge La Nyau
No. 6 – Me & You – Ommy Dimpoz – Vanessa Mdee
No. 5 – Kesho – Diamond
No. 4 – My – Ali Nipishe
No. 3 – Mama Yoyo – G Nako – Ben Pol
No. 2 – Utamu – Dully Sykes – Diamond – Ommy Dimpoz
No. 1 – Jambo Jambo – Steve Rn’B


HII NI PICHA YA PADRI ALIYEUWAWA ZANZIBAR, GARI LAKE NA TAARIFA YA WALIOKAMATWA.



MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi  Ameen.


ALICHOSEMA HALIMA MDEE KUHUSU BUNGE KUONDOLEWA LISIONEKANE LIVE?


Najua kama umekua karibu na media katika siku za karibuni, stori kuhusu uongozi wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza mpango wa kutaka bunge lisiwe linaonekana live kwenye TV utakua umeisikia.
Ni maoni mengi ya Watanzania yametolewa huku asilimia kubwa ikionekana kupinga huo mpango ambao lengo lake ni kukwepa kuonekana kwa wabunge wanaovunja kanuni kwa kuropoka na kufanya vurugu.


Kwenye hii post ni maoni maalum ya mbunge wa Kawe Halima Mdee ambae namkariri akianza kwa kusema “mmhh… kwanza ni hoja ya kipuuzi sana na muhimu ikaeleweka kwamba bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya dola, kinachoonekana kutaka kufanyika ni muhimili mwingine wa dola kutokutaka umma ujue ukweli kwa kutumia watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa bunge kwa sababu yeye ndio ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania wasipate taarifa ambazo tokea bunge limeanza kurushwa live wamekua wakizipata tofauti na ambavyo walikua wanapewa hizo taarifa katika mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye sentensi nyingine Mh Mdee amesema “nasema hivyo kwa sababu kupitia bunge Watanzania wamejua mikataba mibovu ya madini, wamejua EPA, wamejua Richmond, Buzwagi, wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa kwa ajili ya bajeti zimekua zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo zimekua zinajadiliwa live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia katibu wa bunge na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna uhakika na tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya kuficha”
“Kama mlikua mnafatilia bunge la juzi mmeona kwamba wameweka sheria kusema kwamba mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG taarifa yake akiisoma haitajadiliwa hadi mwaka tena mwingine upite waende tena kuedit na kuleta majibu ya uongo, kwa hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo Serikali inaona mambo yakiendelea hivi inawezekana 2015 wakifika watakua wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu ajabu… kwa hiyo waache wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni za bunge kama Mbunge anakiuka kanuni” – Halima Mdee

HOME --- CHRIS BROWN (OFFICIAL VIDEO)


JAMBO --- STEVE R N B (OFFICIAL VIDEO)


PICHA ZA KIM KARDASHIAN PINDI ALIPOFIKA NIGERIA

Niliandika on millardayo.com siku chache zilizopita kwamba TV Star Kim Kardashian kutoka Marekani ambae ni mpenzi wa rapper Kanye West, alithibitisha kwenda Nigeria alikopata mwaliko wa kuhost show itakayofanyika february 17 2013 kuhusu wapendanao, tayari ameshawasili Lagos.

Kim K amewasili akiwa watu wawili,  mlinzi mmoja na msaidizi wake mmoja wa kike.






Friday, February 15, 2013

Ney wa mitego amepata ajali


Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Ney wa mitego amepata 
ajali mbaya akiwa na gari lake aina ya Alteza akizungumza 
na teentz Ney alisema... 
"Ilikua saa tisa na nusu usiku nilikua natokea masaki 
kuwachukua washkajin zangu ndo nilikua narudi hom
e Lory la mchanga liliingia nyuma ya gari langu pale kwenye
 mataa ya Maisha Club kwenda moroco na kwa bahati
 mbaya
 jamaa akakimbia kwasababu nahisi alidhani ameoua maana
 gari alienda kuingia kwenye mtaro...
Nashukuru mungu mimi mzima ila mguu tu ndo umeshtuka
 kidogo"......…


Msanii kutoka kundi la TMK WANAUME HALISI anaejulikana kama BK amezikwa leo


Msanii kutoka kundi la TMK WANAUME HALISI anaejulikana kama BK amezikwa leo
kwenye makabuli ya wailesi Temeke kalibu na uwanja wa taifa,,MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema pepo .... amiin.

picha ya leo


BREAKING TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MNIGERIA GOLDIE WA PREZZO


Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.



Kwenye Exclusive interview na millardayo.com october 19 2012 alisema alikua na mpango wa kwenda Marekani kurekodi kolabo yake na mastaa wawili wa muziki ambao ni Keri Hilson na Trey Songs ambao tayari mipango ilikua tayari na kilichobaki ilikua ni makubaliano ya mwisho mwisho tu.


Thursday, February 14, 2013

Bum Kubam --- Nick wa pili ft G nako




KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAMU IJUMAA


Taasisi ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF) imewataka Waislamu Tanzania kutoshiriki katika maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwa lengo la kushinikiza Serikali kurahisisha dhamana kwa katibu mkuu wa baraza kuu la Jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.

Mkurugenzi wa TIPF Sheikh Sadiki Godigodi amesema maandamano hayo yameitishwa kwa maslahi ya watu wachache na hayana manufaa yoyote kwa dini hiyo bali yanalenga kuvunja amani ya nchi.

Amesema tayari viongozi mbalimbali wa kitaifa wa kidini wanatafuta namna ya kuishinikiza Serikali kurahisisha masharti ya dhamana kwa Sheikh Ponda na tayari mazungumzo yanaendelea…. hivyo kufanyika kwa maandamano hayo kutakua ni kuingilia uhuru wa Mahakama.

SENTENSI 3 KUHUSU WIZKID KUANZISHA LEBO YAKE MWENYEWE


Kwenye headlines Nigeria kwa wiki kadhaa sasa hivi kumekua na stori kwamba staa mdogo wa muziki nchini humo Ayo Balogun a.k.a Wizkid ameachana na lebo yake ya E.M.E na sasa anafanya ishu zake mwenyewe.

Stori zilizosambaa kuanzia feb 13 2013 ni kwamba Wizkid ameamua kuanzisha lebo yake mwenyewe inaitwa Star boy Entertainment ambapo studio yake itaachia single yake mpya ya ‘Azonto’ february 15 2013.

Msanii huyu ambae ni baba wa mtoto mmoja amekaririwa akisema lebo hiyo itahusika pia na kusimamia biashara zake nyingine kama Star boy clothing line, Star boy cap na Star boy shoes.

HILI NDIO BASI JIPYA LILILONUNULIWA KWA AJILI YA KUWABEBA WACHEZAJI WA TAIFA STARS.