Taasisi ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF) imewataka Waislamu Tanzania kutoshiriki katika maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwa lengo la kushinikiza Serikali kurahisisha dhamana kwa katibu mkuu wa baraza kuu la Jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
Mkurugenzi wa TIPF Sheikh Sadiki Godigodi amesema maandamano hayo yameitishwa kwa maslahi ya watu wachache na hayana manufaa yoyote kwa dini hiyo bali yanalenga kuvunja amani ya nchi.
Amesema tayari viongozi mbalimbali wa kitaifa wa kidini wanatafuta namna ya kuishinikiza Serikali kurahisisha masharti ya dhamana kwa Sheikh Ponda na tayari mazungumzo yanaendelea…. hivyo kufanyika kwa maandamano hayo kutakua ni kuingilia uhuru wa Mahakama.

No comments:
Post a Comment