Sunday, February 17, 2013
KAMA HUKUSIKILIZA TOP 20 YA CLOUDS FM FEB 17 2013, LIST IKO HAPA
No. 20 – Butterfly – Q Chief
No. 19 – Nataka Kulewa – Diamond
No. 18 – Mahakama Ya Mapenzi – Linex
No. 18 – Mahakama Ya Mapenzi – Linex
No. 17 – Alingo – P Square
No. 16 – Mtima Wange – Amin – Linnah
No. 15 – Dear Gambe – Young Killa
No. 16 – Mtima Wange – Amin – Linnah
No. 15 – Dear Gambe – Young Killa
No. 14 – Nipende Kama Nilivyo – Mr Blue
No. 13 – Pete – Ben Pol
No. 12 – Wazo La Leo – Stamina
No. 11 – My Everything – Alikiba
No. 10 – 2030 – Roma Mkatoliki
No. 9 – Kidela – Abdukiba – Alikiba
No. 8 – Dear God – Kala Jeremiah
No. 7 – Walaghai – Bonge La Nyau
No. 6 – Me & You – Ommy Dimpoz – Vanessa Mdee
No. 5 – Kesho – Diamond

No. 4 – My – Ali Nipishe
No. 3 – Mama Yoyo – G Nako – Ben Pol
No. 2 – Utamu – Dully Sykes – Diamond – Ommy Dimpoz
No. 1 – Jambo Jambo – Steve Rn’B
No. 3 – Mama Yoyo – G Nako – Ben Pol
No. 2 – Utamu – Dully Sykes – Diamond – Ommy Dimpoz
No. 1 – Jambo Jambo – Steve Rn’B
ALICHOSEMA HALIMA MDEE KUHUSU BUNGE KUONDOLEWA LISIONEKANE LIVE?
Najua kama umekua karibu na media katika siku za karibuni, stori kuhusu uongozi wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza mpango wa kutaka bunge lisiwe linaonekana live kwenye TV utakua umeisikia.
Ni maoni mengi ya Watanzania yametolewa huku asilimia kubwa ikionekana kupinga huo mpango ambao lengo lake ni kukwepa kuonekana kwa wabunge wanaovunja kanuni kwa kuropoka na kufanya vurugu.
Kwenye hii post ni maoni maalum ya mbunge wa Kawe Halima Mdee ambae namkariri akianza kwa kusema “mmhh… kwanza ni hoja ya kipuuzi sana na muhimu ikaeleweka kwamba bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya dola, kinachoonekana kutaka kufanyika ni muhimili mwingine wa dola kutokutaka umma ujue ukweli kwa kutumia watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa bunge kwa sababu yeye ndio ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania wasipate taarifa ambazo tokea bunge limeanza kurushwa live wamekua wakizipata tofauti na ambavyo walikua wanapewa hizo taarifa katika mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye sentensi nyingine Mh Mdee amesema “nasema hivyo kwa sababu kupitia bunge Watanzania wamejua mikataba mibovu ya madini, wamejua EPA, wamejua Richmond, Buzwagi, wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa kwa ajili ya bajeti zimekua zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo zimekua zinajadiliwa live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia katibu wa bunge na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna uhakika na tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya kuficha”
“Kama mlikua mnafatilia bunge la juzi mmeona kwamba wameweka sheria kusema kwamba mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG taarifa yake akiisoma haitajadiliwa hadi mwaka tena mwingine upite waende tena kuedit na kuleta majibu ya uongo, kwa hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo Serikali inaona mambo yakiendelea hivi inawezekana 2015 wakifika watakua wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu ajabu… kwa hiyo waache wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni za bunge kama Mbunge anakiuka kanuni” – Halima Mdee
PICHA ZA KIM KARDASHIAN PINDI ALIPOFIKA NIGERIA
Niliandika on millardayo.com siku chache zilizopita kwamba TV Star Kim Kardashian kutoka Marekani ambae ni mpenzi wa rapper Kanye West, alithibitisha kwenda Nigeria alikopata mwaliko wa kuhost show itakayofanyika february 17 2013 kuhusu wapendanao, tayari ameshawasili Lagos.
Kim K amewasili akiwa watu wawili, mlinzi mmoja na msaidizi wake mmoja wa kike.
Friday, February 15, 2013
Ney wa mitego amepata ajali
Msanii wa muziki wa kizazi kimpya Ney wa mitego amepata
ajali mbaya akiwa na gari lake aina ya Alteza akizungumza
na teentz Ney alisema...
"Ilikua saa tisa na nusu usiku nilikua natokea masaki
kuwachukua washkajin zangu ndo nilikua narudi hom
e Lory la mchanga liliingia nyuma ya gari langu pale kwenye
mataa ya Maisha Club kwenda moroco na kwa bahati
mbaya
jamaa akakimbia kwasababu nahisi alidhani ameoua maana
gari alienda kuingia kwenye mtaro...
Nashukuru mungu mimi mzima ila mguu tu ndo umeshtuka
kidogo"......…
Msanii kutoka kundi la TMK WANAUME HALISI anaejulikana kama BK amezikwa leo
Msanii kutoka kundi la TMK WANAUME HALISI anaejulikana kama BK amezikwa leo
kwenye makabuli ya wailesi Temeke kalibu na uwanja wa taifa,,MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema pepo .... amiin.
BREAKING TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MNIGERIA GOLDIE WA PREZZO
Ni taarifa ambayo kila aliekua karibu na Goldie kwenye page zake za facebook na twitter inakua ngumu kuamini, taarifa rasmi zimeripoti kwamba Goldie ambae ni mwakilishi wa Nigeria kwenye BBA 2012 AMEFARIKI muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria akitokea Marekani ambapo bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com october 19 2012 alisema alikua na mpango wa kwenda Marekani kurekodi kolabo yake na mastaa wawili wa muziki ambao ni Keri Hilson na Trey Songs ambao tayari mipango ilikua tayari na kilichobaki ilikua ni makubaliano ya mwisho mwisho tu.
Thursday, February 14, 2013
KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAMU IJUMAA
Taasisi ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF) imewataka Waislamu Tanzania kutoshiriki katika maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwa lengo la kushinikiza Serikali kurahisisha dhamana kwa katibu mkuu wa baraza kuu la Jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
Mkurugenzi wa TIPF Sheikh Sadiki Godigodi amesema maandamano hayo yameitishwa kwa maslahi ya watu wachache na hayana manufaa yoyote kwa dini hiyo bali yanalenga kuvunja amani ya nchi.
Amesema tayari viongozi mbalimbali wa kitaifa wa kidini wanatafuta namna ya kuishinikiza Serikali kurahisisha masharti ya dhamana kwa Sheikh Ponda na tayari mazungumzo yanaendelea…. hivyo kufanyika kwa maandamano hayo kutakua ni kuingilia uhuru wa Mahakama.

SENTENSI 3 KUHUSU WIZKID KUANZISHA LEBO YAKE MWENYEWE
Kwenye headlines Nigeria kwa wiki kadhaa sasa hivi kumekua na stori kwamba staa mdogo wa muziki nchini humo Ayo Balogun a.k.a Wizkid ameachana na lebo yake ya E.M.E na sasa anafanya ishu zake mwenyewe.
Stori zilizosambaa kuanzia feb 13 2013 ni kwamba Wizkid ameamua kuanzisha lebo yake mwenyewe inaitwa Star boy Entertainment ambapo studio yake itaachia single yake mpya ya ‘Azonto’ february 15 2013.
Msanii huyu ambae ni baba wa mtoto mmoja amekaririwa akisema lebo hiyo itahusika pia na kusimamia biashara zake nyingine kama Star boy clothing line, Star boy cap na Star boy shoes.

KWA WAPENDANAO: MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU VALENTINE'S DAY!
LEO ni Sikukuu ya Wapendanao. Siku maalumu kwa ajili ya kuoneshana mapenzi ya dhati. Ni siku muhimu sana yenye maana kubwa kwa kila mtu, maana upendo hauchagui.
Maana halisi ya siku yenyewe inaharibiwa na watu wanaotumia fursa ya Valentine’s Day kufanikisha matakwa ya misukumo ya tamaa za miili yao. Kama unabisha nenda gesti ukaulizie chumba leo, kila mahali utakuta kumejaa!

ASILI YAKE NI NINI?
Asili yake hasa ni Roma. Ni siku ya kumkumbuka mtakatifu Padre Valentino ambaye alifungwa na kuhukumiwa kunyongwa katika Utawala wa Dola ya Warumi alipokuwa akitetea vijana waoane badala ya kuzini.
Mtakatifu Valentino aliuawa siku na tarehe kama ya leo, ndiyo maana ikatangazwa rasmi kuadhimishwa kwa ajili ya kumkumbuka kama Baba wa Upendo – mtetezi wa wanandoa.
Aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius.
SIYO NGONO, ANASA!
Baadhi ya watu wameibadilisha maana ya siku hii muhimu kwa wapendanao. Wenyewe wanahisi kuwa ni siku ya kufanya mambo yasiyofaa. Kwao, wapendanao ni ngono. Kuna ambao huanzisha uhusiano siku hiyo kwa lengo la kupata mtu wa kustarehe naye, hili ni kosa.
Kama mtazamo wako ni kutafuta mpenzi mpya na kwenda kustarehe naye utakuwa unakosea sana. Haina maana ya ngono wala anasa na kuharibu fedha kwenye ulevi. Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kwa lengo la kuifanya siku yako kuwa nzuri.
KUMBUKA NDUGU
Inawezekana unaishi kwenye mji mwingine, kazi zinakubana kila siku na hupati muda wa kuwasiliana mara kwa mara na ndugu zako. Siku ya leo ni nzuri kwako kuwakumbuka na kuwaonesha kwamba unawapenda.
Wapo watu muhimu zaidi katika maisha, wazazi. Mpigie simu mama/baba yako, mwambie unavyompenda na kuthamini malezi aliyokupa hadi kufikia umri ulionao. Kama unaweza watumie hata zawadi kwa ajili ya kuonesha mapenzi yako kwake.
Ondoa fikra mbaya kichwani mwako rafiki yangu. Waza kuhusu mema na kupendana kwa dhati, hapo utakuwa umekwenda sawa na maana ya sikukuu yenyewe.
WAKUMBUKE WAHITAJI
Katika jamii yetu kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wazee na wahitaji wengine. Tumia ulichojaliwa kushiriki nao. Siyo lazima iwe fedha, hata chakula na mavazi. Inawezekana una nguo unazodhani hazifai, wape wenzako ambao wanahitaji hapo utakuwa umeonesha namna unavyotambua na kuiadhimisha kwa usahihi.
Ifanye siku hii kuwa ya tofauti zaidi kwa kudumisha uhusiano wako na mpenzi wako na kuzungumzia changamoto mbalimbali za uhusiano wenu kuliko kuwaza starehe na anasa ambazo hupoteza fedha.
Happy Valentine’s Day!

BABA KANUNBA AFUNGUKIA DHAMANA LULU!
KAMA ilivyodhaniwa na wengi kwamba baba wa staa wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa atazungumzia dhamana ya Elizabeth Michael ‘Lulu’, kweli ameibuka na kusema yupo makini kufuatlia mwenendo mzima wa kesi hiyo ya kuua bila kukusudia.
Hivi karibuni, Baba Kanumba alipiga simu kwenye dawati la Amani na kusema dhamana hiyo ya Lulu haimuumizi kichwa kwa sababu kila mtu ana haki ya kupewa dhamana kutokana na sheria ila yupo makini kufuatilia mwenendo wake.
VAZI LA SHYROSE BANJI FULL UTATA
VAZI alilotinga Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji limezua utata kufuatia kuonesha sehemu yake ya tumboni (kitovu).
Utata huo umekuja mara baada ya picha inayomuonesha mbunge huyo akiwa amejipara (tazama pichani) na kuvalia vazi hilo ambalo linamuonesha sehemu hiyo nyeti na kutupiwa mtandaoni.
“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau…

“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau mtandaoni.
“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau mtandaoni.
STORI YA KISA CHA MWANAMKE KUCHOMWA NA PASI YA MOTO NA MUMEWE IKO HAPA
Japo chanzo hakijajulikana, kaimu kamanda wa Polisi Singida Thobias Sedoyeka amesema hilo tukio limetokea nyumbani kwa wanandoa hao Singida na mtuhumiwa tayari wanae na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Mwanamke alieunguzwa ambae ana umri wa miaka 30 amesema ndoa yao imedumu kwa miaka sita na nusu mpaka sasa na kwa kipindi chote hicho amekua akikumbana na vipigo vya mara kwa mara.
Namkariri akisema “siku ya tukio alirudi saa nane nikamfungulia mlango akaingia ndani akalala, aliamka majira ya saa kumi usiku wakati nimelala akawasha pasi ya umeme, ilivyopata moto akaja kuniunguza usoni nikiwa niko usingizini kwa hiyo sikuweza kujitetea kwa lolote nilishtuka nikiwa nimeshaunguzwa, alishanivunja mkono kipindi cha nyuma yakaisha…. mpaka tukio hili la kuniunguza na pasi inaonyesha dhahiri kwamba ni mtu anaweza kutoa hata uhai wangu, nataka sheria inisaidie niweze kupata haki za watoto wangu na niweze kurudi kwetu”
Wednesday, February 13, 2013
matumaini anahitaji msaada zaidi
afya ya msanii wa vichekesho nchini, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ kuonekana kuendelea vyema na kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Amana jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini, Michael Sangu ‘Mike’ amewataka wadau kumsaidika ili afanyiwe uchunguzi zaidi.
Mike aliyasema hayo hivi karibuni alipoongea na Tollywood Newz na kubainisha kuwa Matumaini anatakiwa afanywe uchunguzi wa figo na ini ili aweze kupona kisawasasawa.
“Ingekuwa vyema kama tungejitolea kumsaidia apate vipimo kwenye hospitali kubwa, kwani amerudishwa nyumbani lakini siyo mtu mwenye hali ya kuridhisha, anayetaka kumsaidia atumie namba 0718 951 355,” alisema Mike.
Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)