Thursday, February 14, 2013

STORI YA KISA CHA MWANAMKE KUCHOMWA NA PASI YA MOTO NA MUMEWE IKO HAPA

 
Taarifa ikufikie kwamba jeshi la Polisi Singida linamshikilia mwanaume mmoja aitwae Baltazary Mushi maarufu kama Sumayuni mwenye umri wa miaka 33 kwa tuhuma za kumuunguza mkewe usoni kwa kutumia pasi ya umeme wakati mke huyo akiwa kalala usiku.
Japo chanzo hakijajulikana, kaimu kamanda wa Polisi Singida Thobias Sedoyeka amesema hilo tukio limetokea nyumbani kwa wanandoa hao Singida na mtuhumiwa tayari wanae na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Mwanamke alieunguzwa ambae ana umri wa miaka 30 amesema ndoa yao imedumu kwa miaka sita na nusu mpaka sasa na kwa kipindi chote hicho amekua akikumbana na vipigo vya mara kwa mara.
Namkariri akisema “siku ya tukio alirudi saa nane nikamfungulia mlango akaingia ndani akalala, aliamka majira ya saa kumi usiku wakati nimelala akawasha pasi ya umeme, ilivyopata moto akaja kuniunguza usoni nikiwa niko usingizini kwa hiyo sikuweza kujitetea kwa lolote nilishtuka nikiwa nimeshaunguzwa, alishanivunja mkono kipindi cha nyuma yakaisha…. mpaka tukio hili la kuniunguza na pasi inaonyesha dhahiri kwamba ni mtu anaweza kutoa hata uhai wangu, nataka sheria inisaidie niweze kupata haki za watoto wangu na niweze kurudi kwetu”
 

No comments:

Post a Comment