Sunday, September 28, 2014

VOLCANO JAPAN: 30 WAHOFIWA KUFARIKI

Moshi kutoka katika mlipuko wa volcano uliotokea jana kwenye Mlima Ontake, Japan.
Jivu la volcano likiwa limefunika nyumba zilizo jirani na mlima huo.
Taswira kutoka mlimani hapo.
WATEMBEA masafa marefu takribani 30 wanahofiwa kufa katika mlipuko wa volcano uliotokea jana kwenye Mlima Ontake nchini Japan.
Watu hao wamekutwa wakiwa hawapumui huku mapigo yao ya moyo yakiwa yamesimama taarifa imeeleza. Taarifa hiyo haikuweka wazi kama wamepoteza maisha maaba uthibitisho wa kifo nchini Japan lazima utolewe baada ya vipimo vya madaktari.
Zaidi ya watu 250 walikuwa wamekwama katika mlima huo japo wengi wao walifanikiwa kuteremka kutoka kwenye mlima huo wenye urefu wa mita 3,067.
Baadhi yao majeruhi wamesema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.

WAKAZI WA MBEYA WAFURIKA KWENYE SEMINA YA KAMATA FURSA

Msanii Mrisho Mpoto akiongea na wakazi wa Mbeya waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa mapema leo ndani ya Ukumbi wa Benjamini Mkapa.Msemaji kutoka GS One, Pius Mkongoti akiongea na wakazi wa Mbeya waliokuwa wamefurika kwenye Semina ka Kamata Fursa, tayari kwa kuwapa mbinu za kutomia huduma ya Bar code. Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego akisalimiana na wakazi wa Mbeya waliokuwa kwenye Semina ya Kamata Fursa muda mfupi baada ya kupewa nafasi ya kujitambulisha kwao na kuwaambia namna alivyojipanga kulishambulia jukwaa la Fiesta usiku wa leo ndani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.Ofisa Utekelezaji wa NSSF, Ally Mkulembo, akwapatia mbinu  za kujikwamua kimaisha wakazi wa Jiji la Mbeya kupitia mafao na huduma mbalimbali za NSSF.Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliyopo Mbeya mjini.Msanii wa Bongo Fleva Godzilah, akishusha mistari kwa wakazi wa Mbeya waliokuwa kwenye Semina ya Kamata Fursa muda mfupi baada ya kupewa nafasi ya kusalimiana nao.Baba Levo, akiwaambia wakazi wa Mbeya namna ambavyo yeye aliweza kutumia Fursa kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF.
Msemaji wa SSRA Stewart Bisanda akiwapatia mbinu mbadala za kujikwamua kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mbeya.Msanii wa Bongo Fleva Hamad Ally 'Madee', akiongea jambo mbele ya wakazi wa Mbeya waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa mapema leo kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kutumia fursa zilizopo mjini hapo.Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikiendelea mapema leo ndani ya Ukumbi wa Benjamin Mkapa.Mwanadada Recho ambaye ni msanii wa Bongo Fleva akicheka baada ya kupokelewa kwa shangwe na wakazi wa Mbeya mara baada ya kuingia kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa ambapo kulikuwa na Semina ya Kamata Fursa.Chipukizi wa Bongo Fleva Baraka Da Prince akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Mbeya Mjini waliokuwa wamefurika kwenye semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Benjamin Mkapa.Estelina Sanga 'Linah', akiimba moja ya mstari uliopo kwenye wimbo wake wa Ole Themba, mara tu baada ya kupewa nafasi ya kusalimiana na wakazi wa Mbeya waliokuwa wamejitokeza kwenye semina ya Kamata Fursa.Meza kuu ya wazungumzaji wa Semina ya Kamata Fursa ikifuatilia baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo kabla ya wazungumzaji hao kukaribishwa kwa kutoa mafunzo na mbinu mbalimbali za kuwawezesha wakazi wa Mbeya kutumia Fursa zipatikanazo mkoani hapo.

MKENYA AVUNJA REKODI BERLIN


Dennis Kimetto.
MWANARIADHA raia wa Kenya, Dennis Kimetto leo amevunja rekodi ya mbio za marathon jijini Berlin nchini Ujerumani kwa ushindi wake wa saa 2, dakika 2 na sekunde 57.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30, amevunja rekodi hiyo akipunguza sekunde 26 katika rekodi iliyowekwa na Mkenya mwenzake Wilson Kipsang ya 2: 03: 23 katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka jana jijini Berlin.
Kimetto amesema: "najisikia vizuri maana nimeshinda mashindano magumu, nilikuwa fiti tangu mwanzo wa mbio hizo na wakati nikikaribia kumaliza nilihisi kuwa nitashinda na kuvunja rekodi"
Orodha ya rekodi zilizowahi kuwekwa kila baada ya miaka 10.

SIMBA HOI KWA POLISI MORO UWANJA WA TAIFA DAR

Kikosi cha timu ya Simba SC kilichoanza dhidi ya Polisi Moro na kuambulia sare ya bao 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha timu ya Polisi Moro kilichoanza dhidi ya Simba SC.
Mshambuji wa Simba CS, Emmanuel Okwi akifunga bao lake dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Emmanuel Okwi akimtoka mchezaji wa Polisi Moro.
Mchezaji wa Simba Jonas Mkude (Katikati) akimtoka mchezaji wa Polisi moro, na  beki MgandJoseph Owino (kushoto).  
SIMBA SC imelazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, tayari Simba SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 32 akimalizia pasi fupi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’

YANGA WAIKANDAMIZA PRISONS 2-1 TAIFA

Mshambuliaji wa Yanga, Genilson Santana 'Jaja' akimpongeza mwenzake Andrew Coutinho (wa kwanza kushoto) aliyeifungia Yanga bao la kwanza dhidi ya Prisons katika Uwanja wa Taifa, Dar leo.
Mchezaji wa Yanga, Andrew Coutinho akijaribu kuipita ngome ya Prisons.
Kikosi cha Prisons kilichoanza dhidi ya Yanga leo.
Kikosi cha Yanga kilichoiua Prisons ya Mbeya mabao 2-1.
Mchezaji wa Yanga, Andrew Coutinho alilalamika baada ya kufanyiwa madhambi uwanjani.
...Andrew Coutinho kazini.
Mshambuliaji wa Yanga, Genilson Santana 'Jaja' akifanya yake.

Saturday, September 6, 2014

Picha za Wasanii muda mfupi baada ya ajali kutokea Musoma.



15September 5 2014 kumetokea ajali kubwa za mabasi mawili ya abiria hapa Musoma na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 likiwa ni tukio baya lililochukua maisha ya ndugu zetu kwenye tarehe iliyokua imepangwa kufanyika tamasha la Serengeti Fiesta.
Muda mfupi baada ya ajali hiyo, Ruge Mutahaba kutoka kwenye kamati ya maandalizi ya Fiesta alikusanyika na Wasanii wote waliokua waimbe kwenye tamasha hili na kuzungumza na Waandishi wa habari juu ya maamuzi yao waliyofikia kuahirisha tamasha hili kutokana na huu msiba.
‘Isingiwezekana sisi kuendelea na tamasha wakati ndugu zetu wamepoteza maisha, kiukweli huu msiba umenigusa sana’ alisema Shilole, Christian Bella alisema ‘kauli mbiu ya Fiesta mwaka huu ni Sambaza upendo, kwa kuizingatia tumeona ni muhimu tuahirishe kulifanya hili tamasha siku hii manake huu msiba umemgusa kila mmoja…. najua uchungu wa kumpoteza ndugu kwenye kifo cha ghafla kama ajali’
14
Adam Mchomvu, Roma, Shilole, Nay wa Mitego, Young Killer na wengine mbele ya waandishi wa habari wakati taarifa za kuahirishwa kwa fiesta zikitangazwa
12Hii picha hapa juu ni muda mfupi baada ya kuahirishwa kwa fiesta, Wasanii walionyesha moyo mkubwa na kuuweka umaarufu pembeni kisha kuongozana wote kwenda kutembelea Majeruhi hospitali na pia kuwapa misaada mbalimbali waliofiwa na wenye ndugu majeruhi.
11Kiukweli Wasanii waliguswa sana na huu msiba ambapo wakiwa hospitalini mmoja alianzisha wazo la kurudi tena leo kujulia hali majeruhi na kutoa misaada mingine kitu ambacho kiliungwa mkono na wengine wote.

9
Mganga mkuu hospitali ya mkoa akiwa ofisini kwake
8
7


4
Ruge Mutahama akiwaongoza Wasanii kukabidhi misaada kwa mganga mkuu
2


Dakika 3 za Wema Sepetu akizungumzia yote yanayosemwa ikiwemo issue ya kuajiriwa na Kajala.


wemaaKupitia mitandao na magazeti siku chache zilizopita ilitoka stori ambayo ilidai Kajala anaelekea kumuajiri Wema Sepetu,leo Wema kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala.
Kupitia You heard ya  XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye[Wema],Wema Sepetu akamjibu>>’Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy’
Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu>>’Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy’
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu>>’Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali’.

Exclusive: Diamond Platnumz azungumza kwa mara ya kwanza mambo 6 kuhusu fujo zilizotokea Ujerumani

Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.12 AMKuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na millardayo.com
1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.38 AM3. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.59 AM6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’
Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.

DK MWAKYEMBE AAMURU KUFUNGIWA MABASI YALIYOSABABISHA AJALI MARA

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe (Picha na Maktaba).
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya  J4 Express  na  Mwanza Coach yafungiwe mara moja.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu muda mfupi uliopita, Dk Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu 39  na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na uzembe kama huu unasikitisha sana. Walikuwa wanaonana na hata lile gari dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk. Mkwakyembe.
Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya wananchi. “Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.

TASWIRA YA AJALI MUSOMA SIKU YA JANA


Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba, Mjini Musoma mchana siku ya jana.

Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Hali Ilikuwa hivi katika eneo la tukio lililotokea ajali ya mabasi hayo kupata ajali baada ya kugongana.

Umati wa watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo lilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 39 kupoteza maisha papohapo.
Gari likiwa ndani ya mto baada ya kutokea ajali.

Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye namba ya usajili T 332 AKK lililosukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni. Gari hili ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.

Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.

Hivi ndivyo uokozi namna ulivyokuwa ukiendelea baada ya ajali kutokea.

  Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

MATUKIO YA AWALI YA AJALI HIYO ILIYOTOKEA MKOA WA MUSOMA NA ZAIDI YA ABIRIA 25 KUPOTEZA MAISHA.

Mabasi hayo yakiwa yamegongana
Baadhi ya miili iliyofariki katika ajali hiyo.




Basi la J4 Express lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba.