Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe ameagiza makampuni ya Mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yafungiwe mara moja.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu muda mfupi uliopita, Dk
Mwakayembe amesema sehemu iliyotokea ajali na kusababisha vifo vya watu
39 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ni sehemu ambayo kila dereva
alikuwa akimuona mwenzake, hivyo ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
“Ile sehemu ipo wazi kabisa, kule kuna kilima na huku kuna kilima na
daraja lipo katikati, kwa hiyo wale madereva walikuwa ni wazembe na
uzembe kama huu unasikitisha sana. Walikuwa wanaonana na hata lile gari
dogo walikuwa wanaliona… hii hali inasikitisha sana,” alisema Dk.
Mkwakyembe.
Alitahadharisa kwamba kuanzia sasa hivi kila basi litakalopata ajali
ya kizembe ataaamuru vyombo husika vilifungie ili kuokoa maisha ya
wananchi. “Katika uongozi wangu madereva wazembe wajuwe kabisa kuwa
sitaweza kuvumilia, nitaamuru wafungiwe mara moja wakisababisha ajali za
kizembe,” alisisitiza Waziri Mwayembe.
No comments:
Post a Comment