Muda mfupi baada ya ajali hiyo, Ruge Mutahaba kutoka kwenye kamati ya maandalizi ya Fiesta alikusanyika na Wasanii wote waliokua waimbe kwenye tamasha hili na kuzungumza na Waandishi wa habari juu ya maamuzi yao waliyofikia kuahirisha tamasha hili kutokana na huu msiba.
‘Isingiwezekana sisi kuendelea na tamasha wakati ndugu zetu wamepoteza maisha, kiukweli huu msiba umenigusa sana’ alisema Shilole, Christian Bella alisema ‘kauli mbiu ya Fiesta mwaka huu ni Sambaza upendo, kwa kuizingatia tumeona ni muhimu tuahirishe kulifanya hili tamasha siku hii manake huu msiba umemgusa kila mmoja…. najua uchungu wa kumpoteza ndugu kwenye kifo cha ghafla kama ajali’
Adam
Mchomvu, Roma, Shilole, Nay wa Mitego, Young Killer na wengine mbele ya
waandishi wa habari wakati taarifa za kuahirishwa kwa fiesta
zikitangazwa
Ruge Mutahama akiwaongoza Wasanii kukabidhi misaada kwa mganga mkuu
No comments:
Post a Comment