WAKAZI WA MBEYA WAFURIKA KWENYE SEMINA YA KAMATA FURSA
Msanii
Mrisho Mpoto akiongea na wakazi wa Mbeya waliojitokeza kwenye Semina ya
Kamata Fursa mapema leo ndani ya Ukumbi wa Benjamini Mkapa.
Msemaji
kutoka GS One, Pius Mkongoti akiongea na wakazi wa Mbeya waliokuwa
wamefurika kwenye Semina ka Kamata Fursa, tayari kwa kuwapa mbinu za
kutomia huduma ya Bar code.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego akisalimiana na wakazi
wa Mbeya waliokuwa kwenye Semina ya Kamata Fursa muda mfupi baada ya
kupewa nafasi ya kujitambulisha kwao na kuwaambia namna alivyojipanga
kulishambulia jukwaa la Fiesta usiku wa leo ndani ya Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya.
Ofisa
Utekelezaji wa NSSF, Ally Mkulembo, akwapatia mbinu za kujikwamua
kimaisha wakazi wa Jiji la Mbeya kupitia mafao na huduma mbalimbali za
NSSF.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, akiongea
jambo wakati wa ufunguzi wa Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa
Benjamini Mkapa uliyopo Mbeya mjini.
Msanii
wa Bongo Fleva Godzilah, akishusha mistari kwa wakazi wa Mbeya
waliokuwa kwenye Semina ya Kamata Fursa muda mfupi baada ya kupewa
nafasi ya kusalimiana nao.
Baba Levo, akiwaambia wakazi wa Mbeya namna ambavyo yeye aliweza kutumia Fursa kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF.
Msemaji wa SSRA Stewart Bisanda akiwapatia mbinu mbadala za kujikwamua kwa kutumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mbeya.
Msanii
wa Bongo Fleva Hamad Ally 'Madee', akiongea jambo mbele ya wakazi wa
Mbeya waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa mapema leo
kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kutumia fursa zilizopo mjini
hapo.
Baadhi
ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya
Kamata Fursa iliyokuwa ikiendelea mapema leo ndani ya Ukumbi wa Benjamin
Mkapa.
Mwanadada
Recho ambaye ni msanii wa Bongo Fleva akicheka baada ya kupokelewa kwa
shangwe na wakazi wa Mbeya mara baada ya kuingia kwenye Ukumbi wa
Benjamin Mkapa ambapo kulikuwa na Semina ya Kamata Fursa.
Chipukizi
wa Bongo Fleva Baraka Da Prince akisalimiana na baadhi ya wakazi wa
Mbeya Mjini waliokuwa wamefurika kwenye semina ya Kamata Fursa ndani ya
Ukumbi wa Benjamin Mkapa.
Estelina
Sanga 'Linah', akiimba moja ya mstari uliopo kwenye wimbo wake wa Ole
Themba, mara tu baada ya kupewa nafasi ya kusalimiana na wakazi wa Mbeya
waliokuwa wamejitokeza kwenye semina ya Kamata Fursa.
Meza
kuu ya wazungumzaji wa Semina ya Kamata Fursa ikifuatilia baadhi ya
mambo yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo kabla ya wazungumzaji hao
kukaribishwa kwa kutoa mafunzo na mbinu mbalimbali za kuwawezesha wakazi
wa Mbeya kutumia Fursa zipatikanazo mkoani hapo.
No comments:
Post a Comment