Saturday, July 19, 2014

AUNTY ATAMANI KUZAA

Stori: Maria Halimoja
Mkali wa sinema za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema anatamani iwe leo au kesho apate mtoto kwani umri wake unaruhusu.Akipiga stori mbili-tatu na paparazi wetu, Aunty alisema kuwa anatamani kuwa mama si kwa kufuata mkumbo bali anataka kuwa mama kwani sasa ni muda muafaka kwake.
Mkali wa sinema za Kibongo, Aunty Ezekiel
“Natamani kwelikweli na mimi siku moja niwe mama wa mtoto sema tu sijabahatika kupata ila naendelea kumuomba Mungu ili ndoto zangu ziweze kutimia,” alisema Aunty Ezekiel.

UCHAWI KABURINI KWA RECHO

Richard bukos na ISSA MNALLY
AMA kweli duniani imani  imekwisha! Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo, Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tunguli za kichawi zikiwa juu ya kaburi la Marehemu Recho Haule.
Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
Muonekano wa tunguli hizo kwa karibu zaidi.
SIMU YAPIGWA GLOBAL
Baada ya mpashaji huyo naye kushuhudia mauzauza hayo alipiga simu kwenye Ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa na kupokelewa na  kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambapo alimweleza mkuu wa zamu hali ilivyo juu ya kaburi hilo.
toa habari: “Jamani hapo ni Global?”
OFM: “Ndiyo. Tukusaidie?”
Mtoa habari: “Kama mnaweza, njooni kwenye Makaburi ya Kinondoni haraka sana. Juu ya kaburi la Recho kumewekwa vitu kama vya ushirikina.”
OFM: “Tupe dakika sifuri tu.”
Mama aliyefika kaburini hapo akishudia tunguli hizo.
OFM WATINGA NA PIKIPIKI
Kama kawaida mkuu wa zamu aliwatuma mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walikwenda mpaka eneo la tukio na kukuta vitu hivyo ambavyo ni tunguri moja iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja (huenda likawa viza) na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
WALINZI WATAFUTWA
Baada ya kujionea vitu hivyo, mapaparazi wetu walikwenda kuwauliza walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:
Mmoja wa vijana waliofika kaburini hapo na kushuhudia tukio hilo.
“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa aliwaona walioviweka.  Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo kaburi.”
NDUGU WA MAREHEMU WENGINE
Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini watu  waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni  mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye alikataa kutaja jina lake.
Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema havina tena mamlaka  ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.
Mtu aliyekuwa akifanya usafi kwenye makaburi hayo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
BABU ASEMA NI NDUMBA
Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu kuivuta nyota ya marehemu.
Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao walichelewa kwani kwa kawaida kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada ya mwili wa marehemu kuzikwa.
“Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.
Marehemu Recho Haule akiwa na Mpenzi wake, Saguda enzi za uhai wake.
SAGUDA WA RECHO SASA
Baada ya hapo, mapaparazi wetu walimsaka aliyekuwa mchumba wa marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina.
Saguda akaenda mbele zaidi kwa kusema: ”Nitakwenda kukutana na walinzi wa makaburi wanieleze kinagaubaga kulikoni kaburi la mchumba angu kuchezewa hivyo.”

ODAMA: SIKWENDA NJE KUJIUZA

WIKI iliyopita mwigizaji Jennifer Kyaka ‘Odama’ alifafanua mambo mbalimbali aliyopitia maishani likiwemo suala la kuficha ujauzito na mambo mengine ambayo yawezekana ulikuwa huyajui juu yake.
Leo tunamalizia makala haya kwa kutazama majibu ya maswali mbalimbali ambayo nilimuuliza na kuyatolea ufafanuzi. UNGANA NAYE…
Mwigizaji wa filamu za kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’
Mwandishi: Wasanii mnatajwa sana kwenye masuala ya ushirikina ili mng’ae kisanii, kwa nini msimtegemee Mungu?
Odama: Uchawi upo, huwezi kuukwepa lakini inategemea na mtu anaundekeza kiasi gani. Binafsi siamini katika hayo mambo. Namtegemea Mungu zaidi.
Mwandishi: Malengo yenu kama kampuni ni nini katika gemu la filamu za Kibongo?
Odama: Kama kampuni malengo yetu makubwa ni kuvuka mipaka ya Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya Wanigeria ambao wanaonekana kututangulia kimaendeleo.
Mwandishi: Kila mtu kwenye sanaa huwa anakuwa na mtu aliyemvutia hadi kuingia, kwa upande wako, ni nani alikufanya uingie kwenye sanaa?
Odama: Msanii ambaye alikuwa akinivutia kabla sijaanza uigizaji ni Monalisa (Yvonne-Chery Ngatwika). Uhalisia wake katika uigizaji ndiyo kitu kilichokuwa kikinivutia kwake ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye sanaa.
Mwandishi: Wasanii wengi mnatajwa kuwa mnakwenda nchi za nje kujiuza, hili unalizungumziaje?
Odama: Kila mtu ana uhuru wa kusema kile anachojisikia lakini kwa upande wangu sina ‘comment’ (maoni) kwa sababu mimi huwa nikienda nje ya nchi nafuata ishu maalum.
Mwandishi: Ishu maalum ndiyo ipi maana hata wewe uliwahi kutajwa katika sakata hili.
Odama: Weee, uniache kabisa. Mimi mara nyingi nakwenda kwa kazi maalum. Kwa mfano safari yangu ya mwisho kwenda (China) nilifuata vifaa vya ofisi kama kamera na vitu vingine.
Mwandishi: Tunafahamu huna muda mrefu tangu ujifungue, lini sasa utaanza kuingia mzigoni au utabaki kama mkurugenzi na hutaigiza tena?
Odama: Hobi yangu ni kuigiza, siwezi kuacha fani hii kwa sababu naipenda. Nasubiri tu mtoto atimize miezi mitatu, nitaanza kazi kama kawaida. Sasa hivi ana miezi miwili.
Mwandishi: Naona umekuwa bongenyanya, huoni kama inaweza kukuharibia ukapoteza mvuto wa kimwonekano utakapoanza kuigiza?
Odama: Ni kweli kwa sasa nimenenepa sana, lakini nafikiria kuanza mazoezi taratibu na nina imani mwili wangu wa kawaida utarudi tu.
Mwandishi: Kwa nini usianze sasa mazoezi, huoni kadiri muda unavyozidi kwenda na wewe unazidi kunenepa?
Odama: Siwezi kuanza mazoezi kwa sasa kwa sababu nilijifungua kwa oparesheni hivyo lazima nikae kama miezi sita hivi ndiyo nipige mazoezi ya nguvu kuepuka kufumua mshono bure.
Mwandishi: Wasanii kwa sasa mna makundi katika mitandao ya kijamii, utakuta timu flani imemdiss flani, hivi unaona kuna umuhimu wowote kwa msanii kuwa na hizo timu?
Odama: Mimi sioni ubaya wa kuwa na hizi timu kwa sababu zinamfanya msanii azungumze kwa ukaribu na mashabiki wake ila tatizo linakuja kwa wale ambao wanazitumia kwa kurushiana matusi, hapo ndipo tatizo linapokuja. Tukizitumia vizuri, hazina madhara.
Mwandishi: Katika maisha yako ya sanaa, ulishawahi kukwazwa na jambo au msanii mwenzako ukateseka kila wakati.
Odama: Huwa napenda kufurahi na kusahau kila wakati, siwezi kukaa na dukuduku moyoni hivyo kama yalitokea nimeshayasahau. Sikumbuki.
Mwandishi: Msanii gani wa kiume anakuvutia jinsi anavyoigiza kwa sasa?
Odama: Walikuwepo wengi huko nyuma ila kama ulivyosema kwa sasa namkubali zaidi Gabo, ni msanii mzuri sana sema kama watu wengi hawajamshtukia.
Mwandishi: Mashabiki wako wangependa kumjua baba wa mtoto huyo na pengine mna mipango gani?
Odama: Mtoto wangu anaitwa Jason kuhusu baba yake watamjua siku si nyingi, wasikonde! Mipango inakuja wakae mkao wa kula.Mwandishi: Asante kwa ushirikiano wako tangu mwanzo hadi mwisho.
Odama: Karibu sana, nawapenda wote.

WEMA AMLIPUA KAJALA, KISA UNAFIKI!

Shakoor jongo na MUSA MATEJA
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25)
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
Wema Sepetu akiwa na shosti wake mpya, Anti Ezekiel.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
Wema Sepetu akiwa na shosti yake, Kajala Masanja.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014: WABUNGE KUTWANGANA ‘LIVE’

AGOSTI 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi kwani Watanzania watashuhudia matukio makubwa ya burudani kupitia Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Miongoni mwa matukio hayo ni ndondi za waheshimiwa wabunge ambapo mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangala atakazichapa ‘kavukavu’ na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mratibu wa tamasha hilo lenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya sekondari nchini, Luqman Maloto alitaja burudani kibao zitakazolipamba tamasha hilo ikiwemo mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na wenzao wa Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie.
Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangala akiongea na wanahabari wa Global Publishers (hawapo pichani).
“Wabunge wa Yanga sasa hivi wanatamba na usajili mpya wa Ridhiwani Kikwete wakati wenzao wa Simba wakiwa na Geodfrey Mgimwa sasa sijui mwaka huu nani ataibuka bingwa kwani mwaka jana Yanga walishinda kwa ushindi mdogo wa 1-0,” alisema Maloto.
Yemi alade wa Nigeria kulitikisa jukwaa
Maloto alisema kwa upande wa burudani ya muziki, atadondoka mkali kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade ambaye ameahidi kumtafuta Johnny wake katikati ya maelfu ya mashabiki watakaojitokeza uwanjani siku hiyo.
Hapatoshi kwenye soka
Kama hiyo haitoshi, Maloto alisema katika upande wa mpira wa miguu, mwaka jana kwenye tamasha hilo mechi kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva, Bongo Fleva waliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 safari hii mambo yatakuwaje?
“Tayari Bongo Movie wameshataja kikosi kamili kitakachoongozwa na kipa wao mahiri Mzee Majuto ‘King’ huku wakiwa kambini chini ya kamati ya ufundi inayoongozwa na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ wakiahidi kuwateketeza kabisa Bongo Fleva,” alisema Maloto.
Kwenye kipengele cha ndondi, Maloto alisema pia kutakuwa na kipute kikali kati ya bondia anayeshikilia mkanda wa UBO (Universal Boxing Organization), Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’ atakayezipiga na mpinzani wake wa siku nyingi, Mada Maugo ‘Mbunge Mtarajiwa’ huku mwanamuziki Khalid Chokoraa akipimana ubavu na Said Memba, Jacob Steven ‘JB’ atamaliza ubishi unaoendelea kwa sasa kwa kuchapana na Cloud 112 pambano hilo likiwa na raundi nne tu.
Maloto alisema, burudani haitaishia hapo, anga la muziki litashambuliwa na Ally Saleh ‘Ali Kiba’ ambapo atapanda jukwaani na kupiga nyimbo zake zote kali sambamba na kutoa sapraizi ya ukimya wake kwa mara ya kwanza.
Mastaa wengine watakaopokezana kipaza sauti ni pamoja na Meninah, R.O.M.A Mkatoliki, Madee, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Wema Sepetu ambaye ataimba nyimbo za bebi wake ‘Diamond’ pamoja na wengine kibao.
“Listi ya waburudishaji ni ndefu, wasomaji waendelee kufuatilia magazeti ya Global Publishers watajuzwa kadri siku zinavyosogea,” alisema Maloto.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LIVE: YEMI ALADE, SHILOLE KUONYESHANA KAZI AGOSTI 8, 2014


ZIARA YA RAIS KUFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKUZO, SONGEA

2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za makazi Mkuzo na kukaribishwa na wenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe (mwenye tisheti ya pundamilia).
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la tukio ambako alizindua mradi huo.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
5
Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
6
Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
8
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo . Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
9
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo .
10
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia tukio hilo.
11
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga miji vizuri na kuboresha madhari.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
14
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
15
Msafara wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
1
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF, LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya "Nyumba yangu, Maisha yangu" ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea ukubwa wa nyumba - kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.

Friday, April 25, 2014

kocha wa zamani wa Barca Vilanova afariki dunia

Kocha wa zamani wa Barcelona Tito Vilanova amefariki akiwa na miaka 45, imetangaza Club hiyo.
Katika statement waliyoitoa Barca wamesema: " Club inatoa pole juu ya kifo cha TitoVilanova, ambae amefariki leo hii akiwa na miaka 45, Barcelona.
Vilanova, Midfielder wa zamani, alikuwa akiugua ugonjwa wa saratani ya koo kwa zaidi ya miaka 2, ugonjwa uliomlazimisha kuachia ngazi kama boss wa barca. 

Vilanova alichukua madaraka kwa Guardiola mwanzoni mwa msimu wa 2012/2013, lakini alilazimka kuchukua likizo ya miezi minne kati ya December 2012 na April 2013 kwa ajili ya matibabu nchini Marekani, na kutibiwa.
Vilanova ambae alilazwa katika hospitali iliyoko Barcelona wiki iliyopita ameacha mke na watoto wawili

Baada ya kukutana kwa siku 67,Bunge maalum la katiba kuahirishwa leo.

bungeeeBunge maalum la katiba leo April 25 linahairishwa bila kupitisha ibara hata moja kati ya 240 ambazo zimo katika rasimu ya katiba bunge hili linahairishwa mpaka mwezi Agosti mwaka huu huku likiendelea kujadili sura ya kwanza na ya sita yenye jumla ya ibara 19 zinazohusu masuala yanayojega msingi wa aina ya muungano unayopendekezwa.
Tume ya mabadiliko ya katiba katika rasimu ya katiba iliyowasilishwa bungeni na aliyekua Mwenyekiti wake Jaji Warioba ilipendekezwa muundo wenye shirikisho la serikali 3,pendekezo ambalo bado limeleta mtafaruku bungeni baada ya kutengeneza pande mbili bungeni kutokana na mgawanyiko huo kauli zenye utata,kejeli,matusi,dhihaka na ubaguzi ni mambo yanayojitokeza sana kwenye sura hizo mbili.
Miongoni mwa vitu vinavyolaumiwa kwa bunge hili la katiba ni matumizi ya lugha zisizofaa kwenye uchangiaji bila kujali kuwa bunge hilo linatazamwa na watu wa rika mbalimbali.

Hii ni kali nyingine kutoka Kenya,Cheki ugumu wa sheria hii mpya inayotaka kuundwa.

Kenya's Supreme Court judges file into the chamber during the opening of the 11th Parliament in NairobiSheria mpya inatengenezwa Kenya sheria hiyo itawataka wanaowazungumzia wakuu wa serikali kufanya mazoezi ya kutosha kwani sheria hii ikipitishwa basi inamaana kwamba Rais,Naibu wake na wake zao pekee ndiyo watakao pewa jina Mtukufu au His/Her Excellency.
Unaambiwa yeyote atakaye kosa kuzingatia hilo adhabu yake atafungwa mwaka mmoja Gerezani au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za Kenya sawa na dola elfu 12 za Marekani.
Yeyote atakaye vunja sheria ya kukosa kumuita Mbunge kwenye bunge la kitaifa Mheshimiwa au Honorable atafungwa mwaka mmoja au faini ya shilingi milioni mbili pesa za Kenya.
Kwenye mpangilio Rasmi wa Itifaki ama pecking order Rais atafatiwa na Naibu wake kisha Spiker wa bunge la taifa,Jaji mkuu,Seneta,Mbunge wa Jimbo na wa mwisho ni Gavana.
Sheria hiyo pia inapendekeza kwamba spika wa bunge la taifa kuitwa Right honourable ama Mheshimiwa mkuu na Jaji mkuu kuitwa his/herloadship,itakua kosa vile vile kumuita mwakilishi wa Jimbo Mheshimiwa hilo ni jina la Mbunge wa Bunge la Taifa peke yake.
Muswada huo uliotungwa na kuwasilishwa Bungeni na Mbunge Mheshimiwa Aden keynan anaye sema kwamba sheria hiyo itasaidia kutoa mpangilio wa vyeo kwa Taifa pia anapendekeza kwamba watumishi wa umma watakao jilimbikizia vyeo watatozwa faini ya Dola milioni mbili.
Mswada huo unajadiliwa Bungeni wakati magavana serikali ya kitaifa, wabunge na mahakama wako kwenye vita vya kubaini ni nani anauwezo wa kutekeleza majukumu na mamlaka ya kutoa muelekeo kwenye maswala mbali mbali yanayo husu usimamizi.

Okwi: Simba SC imenipa magari sita


Okwi huyo akiondoka!
Shakoor Jongo na Musa Mateja
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Emmanuel Okwi, kwa sasa yupo nchini Uganda, aliondoka juzi Jumatano na kuzungumza na Gazeti la Championi Ijumaa pekee huku akiitaja Simba.
Okwi ambaye aligoma kucheza mechi za mwishoni mwa Ligi Kuu Bara, msimu uliomalizika hivi karibuni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alikuwa hajamaliziwa malipo ya usajili wake, amefunguka kuwa Simba ndiyo ambayo imemfanya kuwa vizuri kiuchumi.
Okwi akiingia ndani ya uwanja kwa ajili ya ukaguzi.
Raia huyo wa Uganda ambaye alisajiliwa ‘bure’ Étoile du Sahel ya Tunisia akitokea Simba, kabla ya baadaye kutua AS Villa ya Uganda na kisha Yanga, ameishukuru Simba kuwa ndiyo iliyochangia neema nyingi na kumfanya ajiweke vizuri kiuchumi kwa kuwekeza zaidi nchini kwao Uganda.
Okwi amesema kuwa alipokuwa Simba ni wakati ambapo aliweza kufanya mambo mengi ya kukuza pato lake ikiwemo kununua magari sita aina ya Fuso kwa ajili ya biashara, magari mengine binafsi pamoja na nyumba ya kifahari.
“Naipenda sana Tanzania na nina mambo yangu mengi tu huku,” alisema Okwi muda mfupi kabla ya kuondoka nchini, juzi, aliendelea kufunguka:
“Siyo mshahara pekee wa Simba lakini nilipokuwa pale nilikuwa nikipata vitu vingi, mfano kuna mwanachama mmoja mwanamke alinipa gari, mashabiki nao walikuwa wakinipa vitu vingi, nawashukuru sana kwa yote.”
Okwi akienda kupanda ndege.
Okwi aliongeza kuwa anarejea Uganda kwa kuwa Ligi Kuu Bara imemalizika lakini akatoa kauli kuwa atarejea baada ya wiki tatu kwa ajili ya kukamilisha mambo yake binafsi.
“Kuna vitu fulani nitakuja kuvifanya, siwezi kuvizungumza kwa kuwa ni vyangu binafsi, lakini nafikiri muda ukifika nitazungumza mengine mengi, Watanzania watajua, huu siyo wakati sahihi,” alisema Okwi.
Wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, Okwi alisindikizwa na watu wawili waliokuwa wamebeba mabegi yake, alipofuatwa na mwandishi wa habari (siyo wa Championi) akaweka simu sikioni na kutotaka kuzungumza chochote.
Lakini baada ya kuachwa iligundulika baadaye kuwa simu ilikuwa imezimwa na alikuwa haongei na mtu yeyote.

CHUCHU NA RAY KAMA KIM NA KANYE

KUKOPI na kupesti bila kuboresha! Mastaa wenye mapenzi kama ya njiwa kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wamekuwa wakitupia swaga za picha kama zile za Kim Kardashian na mwandani wake, Kanye West.
Wasanii wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wakijiachia.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Chuchu na Ray ambao majina yao yameunganishwa na kuwa Chura wamekuwa wakichukua sampo za picha za akina Kim nao kujifotoa kisha kuzisambaza.
“He! Mmewaona Chuchu na Ray? Eti wanakopi na kupesti swaga kama zile za Kim na Kanye kisa mapenzi yamekolea,” alisema mdau mmoja baada ya kuziona picha hizo mtandaoni.

WEMA: NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL 13!

Stori:Na Shakoor Jongo KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo wako, siku zote ukikaa nacho kitazidi kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu ambaye umeshibana naye na kumsimulia, moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo!
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa Kajala Masanja.
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwa kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta kumlipia mwanadada huyo zile Sh. milioni 13 za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na Ijumaa katika exclusive interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye pia ni staa mkubwa wa sinema za Kibongoalisema kuwa kuna mambo mazito ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye gogoro kubwa na Kajala.Wema au Beautiful Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo yamemsababishia maumivu ya moyo na kutokwa machozi kila wakati.
“Leo (anataja jina la mwandishi), ngoja nikuelezee kila kitu kinachohusiana na mimi na Kajala juu ya tofauti zetu.“Naamini baada ya kusimulia kisa na mkasa nitakuwa nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani ya moyo wangu.
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia ishu inayonihusu mimi na Kajala,” alianza kufunguka Wema.
UZINDUZI WA KIGODORO
Katika maelezo yake, cha kwanza, Wema ni uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo yeye alisema kuwa alianza kuyaamini yale yaliyokuwa yakisemwa na watu kuhusiana na Kajala.
Wema alisema kabla ya tukio, akiwa saluni akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi huo, ghafla Kajala alimharibia ‘mudi’. “Unajua ile Saluni ya (anataja jina la saluni) pale Kinondoni, ina sehemu mbili, juu na chini, sasa mimi nilikuwa juu na Aunt (Ezekiel) tunatengeneza nywele.
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye.
“Kweli nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo...Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua.
“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha.
“Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” alitiririka Wema.
SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA MIRROW
Wema alisema kuwa baada ya kutofautiana pale saluni, hakuwa na kinyongo, safari ya Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii wao wa Bongo Fleva anayesimamiwa na Kampuni ya Endles Fame Production.
Wakiwa njiani, kwa mujibu wa Wema, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea kutoa ya moyoni: “Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea fedha zake.
“Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi?
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali alinikopesha?
“Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia kwa watu (anataja jina la mwandishi)?
“Iliniuma sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”
WAREJEA DAR, MAANDALIZI YA FILAMU YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar, alimwambia Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.
Alisema kwamba Kajala alikubali na kusema kuwa atachangia Sh. milioni tano katika bajeti ya filamu hiyo.Baada ya kusikia hivyo, Wema alisema alifarijika, alipokwenda kumweleza ‘bebi’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, naye Diamond akasema atatoa Sh. milioni tano hivyo jumla itakuwa Sh. milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa imepangwa ya Sh.milioni nane.
Anaendelea: “Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza nyingine.
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata