Thursday, March 13, 2014
SAMIA HASSAN NDIYE MAKAMU MWENYEKITI BUNGE LA KATIBA
Samia
Suluhu Hassan ndiye Makamu Mwenyekiti wa Kudumu Bunge Maalum la Katiba
baada ya kupata kura 390 sawa na 74% na kumshinda mpinzani wake Amina
Abdallah Amour aliyepata jumla ya kura 126 sawa na 24%. Kwa matokeo
hayo, Samia Hassan ataungana na Samuel Sitta aliyechaguliwa jana kuwa
Mwenyekiti wa Kudumu wa bunge hilo katika mchakato mzima wa kupata
katiba mpya.`
RAHA YAPANUA WIGO WA MAWASILIANO YA INTERNET TANZANIA
Raha kwa sasa wanatoa huduma za internet katika mikoa mbalimbali nje ya Dar es Salaam ikiwemo Tanga na Arusha kwa kutumia teknolojia ya rahaSpots ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma bora popote alipo.
Kwa maboresho haya, Raha wanawaahidi huduma bora zaidi wateja wake ikiwemo kuperuzi kwa haraka mitandao mbalimbali ya kijamii na tovuti.
RAIS WA BAYERN MUNICH AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3 KWA KUKWEPA KODI
Rais wa Bayern Munich amehukumiwa kwenda jela kwa kifungo cha miaka mitatu na miezi sita kutokana na kosa la kukwepa kodi.
Uli Hoeness, 62, alikiri kukwepa kodi inayofikia kiasi cha €18.5 million kupitia akaunti zake za benki za siri lakini utetezi wake wa kukiri kosa akidhania ungemsaidia kuepukana na adhabu ya kifungo ulishindwa kumsaidia.
Mwendesha mashtaka alitaka Hoeness afungwe jela miaka mitano na nusu kwa kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.
Mwishowe, jaji wa mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo akaamuru mwanasoka huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi atumikie kifungo cha miaka 3 na miezi sita.
Uli Hoeness, 62, alikiri kukwepa kodi inayofikia kiasi cha €18.5 million kupitia akaunti zake za benki za siri lakini utetezi wake wa kukiri kosa akidhania ungemsaidia kuepukana na adhabu ya kifungo ulishindwa kumsaidia.
Mwendesha mashtaka alitaka Hoeness afungwe jela miaka mitano na nusu kwa kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.
Mwishowe, jaji wa mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo akaamuru mwanasoka huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi atumikie kifungo cha miaka 3 na miezi sita.
GARI LA WIZARA ZANZIBAR LAPINDULIWA KWA MAWE!
Habari zilizopatikana mchana huu kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa vijana wenye mikokoteni inayovutwa na Ng'ombe wamefanya vurugu na kuanza kupiga mawe magari ya serikali huku wakijerui wafanyakazi wa serikali kadhaa. Katika kadhia hiyo, walisababisha gari la Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Mhe. Khamis Musa kupinduka kama linavyoonekana pichani. Inaelezwa kuwa chanzo cha vurugu hizo ni kupigwa marufuku kwa mikokoteni hiyo kuingia mjini, kitendo ambacho kinapingwa na wamiliki.
RAIS KIKWETE APOKEA RIPOTI YA MGAWANYIKO WA WATU KWA UMRI NA JINSI LEO IKULU, DAR
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho
(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa baada ya kupokea Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia
kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014 Ikulu
jijini Dar es Salaam.
USIJIDANGANYE, NDOA SIYO MAJARIBIO!-2
Lazima wote wawe wana hisia za kweli kutoka ndani ya mioyo yao.
Wiki iliyopita nilianza kwa kueleza mambo ya msingi ya kuzingatia wakati ukimtaka mwenzi wa maisha yako. Leo tunaingia katika hatua nyingine. Twende tukaone.
MAPENZI HALISI
Sifa nyingine muhimu ya kumwangalia mwenzi anayefaa kuwa naye kwenye ndoa ni pamoja na yule mwenye mapenzi ya kweli hasa. Mapenzi ya kweli huonekana haraka sana. Penzi la dhati halijifichi.
Hujitokeza hadharani, wakati mwingine bila hiyari.
Mwenye sifa hii ni msikivu (kwa wanaume na wanawake), muelewa na anayetoa kipaumbele kwa mwenzake. Kama anakupenda kwa dhati ni lazima akupe kipaumbele katika mambo yake.
Si msiri na hutoa nafasi kwa mwenzake kutoa mawazo yake katika mambo yanayomhusu. Hatua hii hutokana na namna anavyomuona mwenzake kama sehemu ya maisha yake.
HUYU HAFAI!
Unaweza kuwa na mpenzi na mkapanga mipango mbalimbali ya baadaye ikiwemo ndoa lakini akawa na kasoro kubwa zilizojificha. Wakati mwingine kasoro hizo unaweza kuziona lakini usijue kama ni kubwa zinazoweza kuwa tatizo kubwa katika maisha yenu ya ndoa.
Mara nyingi kasoro za mwingine zinaweza kufichwa na mapenzi ya dhati yaliyopo ndani ya mtendwa. Mathalani wewe una mpenzi wako, kwa vile ndani yako kuna mapenzi ya dhati, mwenzako anaweza kuwa anakosea tena makosa makubwa, lakini ukajikuta unavumilia, kudharau au kupuuzia!
Zipo dalili nyingi za mpenzi asiyefaa, lakini hapa nakuletea zile za muhimu zaidi.
USALITI
Katika makosa makubwa kabisa kwenye uhusiano ni pamoja na kusaliti. Kama mwenzi wako anakusaliti na una ushahidi wa kutosha (hasa kama umemfumania) ni dalili mbaya kwenye ndoa.
Mtu wa aina hiyo hafai kabisa kumfikiria kuungana naye katika ndoa.
KIBURI
Pia ni dalili mbaya. Mtu mwenye dharau na kiburi hawezi kuwa sahihi, maana huko ndani ya nyumba kutakuwa ni majibizano yasiyo na maana.
Aliye sahihi anapaswa kuwa msikivu, mwenye kupima kila kinachotoka kwenye ulimi wake. Kama katika kipindi cha awali tu, anakuwa mkorofi, vipi kwenye ndoa? Fikiri hili kwa makini.
KIPIGO
Wengi wanaweza wasione kama hili lina maana, lakini nataka kuwaambia, mtu anayetumia nguvu na kumwadhibu mwenzake kwa kipigo, siyo mwenzi sahihi.
Tabia hii zaidi ipo kwa wanaume. Kosa dogo tu anamwangushia mwenzake kipigo. Kupigana si mapenzi. Kama bado mpo kwenye uchumba tu, kosa dogo kipigo, vipi mkiingia kwenye ndoa? Tafakari jambo hili utaona ni kasoro kubwa sana.
MBINAFSI
Hili ni tatizo lingine. Kama mnahitaji kuwa katika muunganiko wa ndoa, ubinafsi ni sumu. Mwenzi mwenye tabia ya lake linakuwa lake mwenyewe na lako linakuwa lenu hafai kwenye ndoa.
ASIYEJITOA
Hili nalo ni tatizo. Unaweza kuwa na tatizo kubwa na kwa kulitazama unaamini kabisa kwamba mwenzako anaweza kukusaidia, lakini hataki tu. Mathalani unaumwa, anaweza kushindwa hata kufika kukujulia hali - hafai.
Hata kama unampenda kwa kiwango gani, huyu hafai kabisa kuwa nawe kwenye ndoa.
Wiki ijayo tunaingia katika sehemu ya mwisho ya mada hii, USIKOSE!
UFUSKA LOKESHENI
BAADHI ya wasanii wa filamu za Kibongo hivi karibuni walinaswa wakifanya vitendo vichafu katika eneo lao la kurekodia ‘location’ pande za Oysterbay jijini Dar, Ijumaa lina uthibitisho wa kutosha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu wasanii hao walinaswa wakifanya vitendo hivyo vilivyo nje ya maadili ya Mtanzania kwa uwazi bila ya kumuogopa mtu yeyote.
Chanzo chetu kilijipenyeza katika kambi ya wasanii hao iliyopo eneo hilo na kuwanasa wakifanya vitendo hivyo vichafu.
“Wameweka kambi kwenye nyumba moja Mikocheni na wamekuwa wakienda kushuti kwenye Ufukwe wa Coco, yaani nimekuwa nikiwafuatilia matendo yao, siyo mazuri. Wanavaa nguo nusu utupu, wanafanya vitendo vinavyoashiria usagaji mbele za watu bila aibu, njooni muwafichue.
“Kuna picha ambazo nimewapiga bila wao kujijua, zinatia kinyaa, mbaya zaidi wengi wao ni wadogowadogo na huenda wamewadanganya wazazi wao kuwa wameenda shule kumbe wapo huku,” kilisema chanzo hicho.
Nyota 9 wayeyuka mazoezini Simba
Na Martha Mboma
WACHEZAJI tisa wa Simba walishindwa kufika mazoezini kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar, jana kutokana na sababu tofauti ikiwemo ya majeraha na matatizo ya kifamilia.
Wachezaji hao ni Amissi Tambwe ambaye ana jeraha kichwani, Zahoro Pazzi ambaye ana tatizo la enka na Gilbert Kaze anayesumbuliwa na goti.
Wengine ambao ni majeruhi ni: Donald Musoti, Betram Mwombeki, Said Ndemla, Abubakari Hashimu, Uhuru Selemani na Abdulhalim Humud ambapo wote hawa wawili wana matatizo ya kifamilia.
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amesema asilimia kubwa ya kikosi chake ni majeruhi ndiyo maana hawaonekani mazoezini hapo kwa siku kadhaa.
“Ninaamini wachezaji wote hao tutakuwa nao pamoja tutakapoanza mazoezi Jumatatu,” alisema Loga.
WACHEZAJI tisa wa Simba walishindwa kufika mazoezini kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar, jana kutokana na sababu tofauti ikiwemo ya majeraha na matatizo ya kifamilia.
Wachezaji hao ni Amissi Tambwe ambaye ana jeraha kichwani, Zahoro Pazzi ambaye ana tatizo la enka na Gilbert Kaze anayesumbuliwa na goti.
Wengine ambao ni majeruhi ni: Donald Musoti, Betram Mwombeki, Said Ndemla, Abubakari Hashimu, Uhuru Selemani na Abdulhalim Humud ambapo wote hawa wawili wana matatizo ya kifamilia.
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amesema asilimia kubwa ya kikosi chake ni majeruhi ndiyo maana hawaonekani mazoezini hapo kwa siku kadhaa.
“Ninaamini wachezaji wote hao tutakuwa nao pamoja tutakapoanza mazoezi Jumatatu,” alisema Loga.
Sunday, February 16, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)



