Mkurugenzi
Mkuu wa Biashara wa Raha, Akash Karia (kushoto) akielezea huduma za
internet zitolewazo na Raha kwa wanahabari (hawapo pichani). Pembeni ni
viongozi wa kampuni hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Akash.
Mkurugenzi Mkuu wa Teknolojia, Nyangu Meghji (katikati) akielezea maboresho yaliyofanywa na Raha katika huduma za internet.
Viongozi wa Raha wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano na wanahabari.
KAMPUNI inayotoa huduma za internet nchini, Raha, imepanua wigo wa
mawasiliano katika internet kwa kutumia teknolojia za 4G WiMax Solution
pamoja na Fiber Optic.
Raha kwa sasa wanatoa huduma za internet katika mikoa mbalimbali nje
ya Dar es Salaam ikiwemo Tanga na Arusha kwa kutumia teknolojia ya
rahaSpots ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma bora popote alipo.
Kwa maboresho haya, Raha wanawaahidi huduma bora zaidi wateja wake
ikiwemo kuperuzi kwa haraka mitandao mbalimbali ya kijamii na tovuti.
No comments:
Post a Comment