Na Martha Mboma
WACHEZAJI tisa
wa Simba walishindwa kufika mazoezini kwenye Uwanja wa Kinesi,
Shekilango jijini Dar, jana kutokana na sababu tofauti ikiwemo ya
majeraha na matatizo ya kifamilia.
Wachezaji hao ni Amissi Tambwe ambaye ana jeraha kichwani, Zahoro
Pazzi ambaye ana tatizo la enka na Gilbert Kaze anayesumbuliwa na goti.
Wengine ambao ni majeruhi ni: Donald Musoti, Betram Mwombeki, Said
Ndemla, Abubakari Hashimu, Uhuru Selemani na Abdulhalim Humud ambapo
wote hawa wawili wana matatizo ya kifamilia.
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amesema asilimia kubwa ya
kikosi chake ni majeruhi ndiyo maana hawaonekani mazoezini hapo kwa siku
kadhaa.
“Ninaamini wachezaji wote hao tutakuwa nao pamoja tutakapoanza mazoezi Jumatatu,” alisema Loga.
No comments:
Post a Comment