Saturday, December 21, 2013

Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, amejiuzulu


Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, amejiuzulu bungeni hivi punde baada ya kutakiwa na wabunge awajibike kwa vitendo viovu vilivyofanywa na wanausalama wakati wa Operesheni Tokomeza!

FOMU ZA KUMNG’OA WAZIRI MKUU PINDA ZALETWA BUNGENI

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ameingia na fomu bungeni hivi punde kwa ajili ya kukusanya saini za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya ripoti iliyofichua maovu yaliyofanyika katika Operesheni Tokomeza.

BARNABA, SHILOLE NGOMA DROO AVUTA NDINGA YA MIL.25

Stori: Shakoor Jongo
FEDHA inaongea. Siku chache baada ya mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kuvuta mkoko Toyota Lexus, mkali wa Bongo Fleva, Elias Barnaba naye amemjibu kwa kuvuta Mark X.
  Mkoko mpya wa mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aina ya Toyota Lexux.
Barnaba ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo kisha wakamwagana, ameamua kuvuta gari hilo ambalo lina thamani ya Sh. Mil 25 sawa na lile la Shilole.
Akizungumza na paparazi wetu, Barnaba aliweka plain kuwa amenunua mkoko huo ambao anaamini utaendana na mishemishe zake za kimuziki ambapo kwa wakati huu ameona gari hilo ndilo linamfaa.
Elias Barnaba naye amemjibu kwa kuvuta Mark X.
“Namshukuru Mungu kwamba ndoto zangu za kuvuta gari ya aina hii zimetimia, sijui huko mbeleni nitakuwa na ndoto za kumiliki gari gani lakini kwa sasa acha nikae humu kwanza,” alisema Barnaba.
Kabla ya kununua mkoko huo, Barnaba staa wa songi la Sorry alikuwa akimiliki gari aina ya Oppah yenye thamani ya Sh. Mil 16 sawa na Shilolo ambaye pia alikuwa na gari aina hiyo kabla ya kununua Toyota Lexus.

PUNGUZO KUBWA LA BEI ZA NGUO ZA KIKE


PUNGUZO KUBWA LA BEI ZA NGUO ZA KIKE!!
Kuna Punguzo la Bei katika duka la Sachques Clothing Store, Blouse, Skirts, Blazers, Trousers - Tshs 10,000/=, Short Dresses- 15,000; Long Dresses & Jump Suit-25,000; Hand Bags, Accessories na Viatu pia vipo kwenye PUNGUZO LA BEI, SIMU NAMBA 0774801316, Tupo Kijitonyama Police Mabati DSM, wa Mikoani tunatuma kwa maBasi. Tembelea www.facebook.com/SachquesClothingStore kuona vitu zaidi

WAPIGWA MIMBA BILA NDOA

Stori: WAANDISHI WETU
HII ni funga mwaka! Mastaa wa Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Recho Haule, Belina Mgeni na Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ wamejikuta wakiumalizia mwaka 2013 wakiwa ‘vitumbo ndii’ licha ya kuwa bado hawajaolewa, Risasi Jumamosi lina data kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wasanii hao wamebeba mimba hizo kwa nyakati tofauti na wamekuwa wakijificha kukwepa aibu ya kubeba ujauzito kabla ya kufunga ndoa.
                                                                    Belina Mgeni.
“Wanaona aibu kubeba ujauzito kabla ya ndoa, wamekuwa wakijificha na mbaya zaidi hawataki kujionesha maana wengi wao hawajawatambulisha wachumba wao  kwa wazazi wao,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotaja jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka ukweli wa habari hiyo ambapo jitihada zilizaa matunda kwa kupatikana kwa picha za mastaa hao zikionesha tayari vitumbo ndii.
                                                                Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Baadhi yao, picha zilionesha mimba zikiwa ni kubwa huku wengine zikionekana ndiyo bado changa. Aunty Lulu, Belina walionekana dhahiri kuwa ni waleo au kesho, matumbo yao yalionekana ‘live’ ni makubwa, Odama yeye ilionekana bado halijajitokeza vizuri.
                                                                             Recho Haule.
Kwa upande wa Recho Haule, rafiki wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, alipenyeza habari kuwa mimba aliyonayo shosti wake huyo ni ya mpenzi wake wa kitambo, Saguda George lakini naye amekuwa akijifungia ndani kukwepa macho ya watu.
“Recho ni mjamzito lakini amekuwa akijificha kukwepa kamera za mapaparazi si unajua tena uchumba wake na Sagunda kila mmoja alikuwa akiufatilia magazetini!”
                                                                    Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Baada ya mapaparazi wetu kujitosheleza na ushahidi wa picha, zoezi la kuwasaka wasanii hao ili kujua wahusika wa mimba hizo lakini simu zao ziliita muda mrefu bila kupokelewa.
Baadhi ya mashabiki walioongea na Risasi Jumamosi, hawakusita kuonesha hisia zao kwa mastaa hao, kila mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya mastaa hao.
“Unajua kama Belina naona amebeba mimba ila yuko kwenye process ya kufunga ndoa ingawa sijui ni lini kwani niliwahi kumsikia akisema kuwa anaweza kufunga ndoa soon” alisema shabiki mmoja, mwingine akasema hivi:
“Sisi tujuavyo kioo cha jamii maana yake ni mtu kufanya yale yanayofaa kuigwa lakini kwa hawa mastaa wetu  wamefanya tofauti, wote wamebeba mimba bila ndoa, sasa jamii itajifunza nini kutoka kwao?”

TUME YA KATIBA KUKABIDHI RASIMU YA PILI DESEMBA 30

Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakabidhi rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, Desemba 30, mwaka huu.
Makabidhiano hayo yatafanyika katika hafla itakayofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuiandaa.
Rasimu hiyo ya pili inatolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa rasimu ya kwanza ya ambayo ilijadiliwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyokaa kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Ibara ya 20 (2) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, mara baada ya Rais kukabidhiwa rasimu hiyo, itachapishwa katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine ndani ya siku 31.

Pia katika kipindi hicho, Rais anatakiwa kuitisha kikao cha Bunge Maalumu la Katiba kwa ajili ya kupitisha rasimu iliyopendekezwa. Kutokana na hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa Bunge la Katiba litaanza vikao vyake Februari, 2013.

Taarifa ya Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid iliyotolewa jana ilieleza kuwa Tume hiyo itakabidhi rasimu hiyo kwa Marais Kikwete na Dk Shein katika hafla itakayohudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

Tume hiyo ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili Desemba 15 mwaka huu lakini Rais Kikwete aliiongezea siku 14 zaidi hadi Desemba 30, mwaka huu.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete kuiongezea muda tume hiyo ilikuwa ya pili. Mara ya kwanza iliomba kuongezewa muda wa siku 45, kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu. Kabla ya kuomba kuongezewa muda mara ya kwanza, ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 30.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza Tume hiyo kufanya kazi kwa miezi 18 licha ya kuwa inampa Rais mamlaka ya kuiongezea muda usiozidi siku 60.

Hatua ya Rais kuiongezea muda kwa mara ya pili, ilitafsiriwa kama kutoa fursa kwa wajumbe wake kujipanga upya baada ya kifo cha mwenzao, Dk Sengondo Mvungi kilichotokea Novemba 12, mwaka huu huko Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga.

Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotolewa Juni 4, mwaka huu.

Saturday, November 9, 2013

TUNAMJUA ZAIDI JAY Z, HATUMUELEWI KIDA WAZIRI

TUNAMJUA ZAIDI JAY Z, HATUMUELEWI KIDA WAZIRI

Mambo vipi maanko?
Awali ya yote, ninaomba kuomba radhi kwamba katika makala iliyopita, kwa bahati mbaya, niliandika kwa makosa kwamba Chonya alipatikana katika kitabu cha Kuli. Usahihi ni kwamba huyu jamaa alipatikana katika kitabu cha Shida na ninawashukuru wote walionikosoa!
Mimi ni shabiki wa Arsenal. Nina furaha kwamba timu yangu ilishinda mechi yake ya Jumatano dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na nadhani kesho Jumapili, tunaweza kuwakalisha chini Man United pale kwao Old Trafford katika Ligi Kuu England!
Ni shabiki wa vitu vingi sana, napenda soka, muziki, filamu na kila aina ya burudani. Ninafurahishwa na baadhi ya watu katika michezo tofauti kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakifanya vizuri. Ninapopenda kitu cha Ulaya, ujue na hapa nyumbani kipo kama kile ninachokishabikia na kama sina, basi ni lazima niwe na sababu.
Nimesema ninapenda soka na ni shabiki wa Arsenal kule Ulaya, hapa nyumbani, kiasili ni shabiki wa Simba, lakini niliachana na ushabiki wa kupenda kupindukia baada ya kugundua mambo mengi ya ajabu yanayofanyika katika klabu zetu hizi mbili za Kariakoo wakati ule nikiwa Mwandishi wa michezo.
Nikakataa ushabiki huo, sisi tunalia kwa uchungu tunapofungwa, kumbe viongozi wanashangilia, wanajua nini walichofanya. Nina miaka mitatu sijakanyaga uwanjani na hata msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara sijui ulivyo!
Unajua kwa nini nimeanza hivi? Ni kwa sababu wanafunzi wengi wako hivi. Wanapenda sana vitu vya Ulaya, wenyewe wakisema mbele, lakini hawana wanachojua hapa nyumbani. Wanatumia muda mwingi kujifunza mambo ya Kimarekani kuliko kujiuliza kuhusu Tanzania na Afrika.
Leo hii ukifika katika shule zetu na vyuo, wanamuziki, wacheza filamu na wanamichezo wa nje wanafahamika zaidi kuliko watu kama hao wa hapa nyumbani. Watakuambia kuhusu Justin Bieber, kazaliwa wapi, kapiga nyimbo gani, anapenda nini na kila kinachomhusu, ikiwa ni pamoja na girlfriend wake, lakini hawana wanachojua kuhusu Abdalah Gama!
Sio vibaya kushabikia vitu vya nje, lakini basi kwa nini hatupendi kuhoji kuhusu vya kwetu? Shule ni sehemu ya kujifunza, hasa utamaduni, ujasiri na uzalendo wetu. Tunao watu waliofanya vizuri sana katika kuufikisha utamaduni wetu hapa ulipo, lakini hakuna mtu anayehangaika kutaka kuwajua.
Utashangaa wanafunzi wanaweza kumgundua mwanamuziki mkongwe wa Marekani, Jeniffer Lopez katika picha, lakini mtaani wakashindwa kumtambua Kida Waziri. Tunawapenda mastaa wetu kwa mfano akina Diamond, AY, Profesa Jay, H Baba, Ray C, Jay Dee, Linah, Barnaba na wengineo, lakini ni nadra sana kusikia wanafunzi wakiuliza kwa nini Sinza jijini Dar es Salaam kuna eneo linaitwa Kwa Remmy!
Nadhani tunakosea sana. Tunadharau sana vyetu na kuvisifu, hata kama havina ubora vile vya nje. Siyo kila kitu chetu kinafundishwa shule, vitu vingine vinataka udadisi tu wa sisi wenyewe. Kwa mfano ukiachana na akina Kinjekitile, Mkwawa, Munyigumba, Mirambo, Songea na wenzao walio katika historia, nani anatufundisha kuhusu akina Moris Nyunyusa, Mzee Makongoro na hata Mbaraka Mwishehe?
Tunatakiwa kuwa wadadisi wa kupenda sana kujua vya kwetu. Ni jambo la kushangaza kwamba kuna wazungu wanaijua nchi yetu kuliko baadhi yetu, maana sisi muda wote tupo Facebook, Twitter na Instagram ili kujua mambo ya kina Jay Z, badala ya kujiuliza kwa nini Nyerere anaonekana katika televisheni leo, miaka zaidi ya 25 baada ya kufariki kwake?

Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha-9

Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha-9

Tunaendelea na mada yetu ya Makosa 10 wanawake huyafanya wakiwa faragha kutoka pale tulipoiishia wiki iliyopita.
Endelea...
Nilishaeleza huko nyuma kwamba ni vizuri kuzungumza wakati wa tendo. Hata kama wewe ni mvivu, jibidishe katika kuulainisha ulimi wako ili uwe unatamka maneno matamu, yanayoongeza hamu na mzuka wa kuendelea kuwajibika shughulini.
Unaweza kudhani ni kitu kidogo lakini ukweli ni kwamba wengi wamepata alama nyingi na kuonekana bora zaidi kwa sababu ya maneno yao faragha, matamshi na ubunifu wa kusifia. Kitaalamu, maneno matamu hunogesha tendo kwa kuongeza mshawasha.
Dunia imechafuka, usaliti umekuwa mkubwa na watu hawaogopi. Tafakari; unasalitiwa na mwenzi wako ambaye anatenda dhambi kwa kutoka na mkali wa maneno yenye kutia ‘wazimu’ kunako eneo mahsusi. Akirudi kwako, anabaini wewe upoupo tu, kazi yako kuhema kwa nguvu na kufumba macho.
Anakosa msisimko, zaidi unamkata stimu kwa sababu kwa yule anayekusaliti hukutana na manjonjo mengi. Mwisho unajikuta unapigwa kibuti bila kupenda. Tafadhali sana, yapo mambo ambayo unaweza kusema huwezi na ukavumiliwa lakini siyo hili la kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha ‘maraha’.
Narudia tena, usiseme mwenzi wako anatosheka kwa sababu anakwambia amefika kileleni, la hasha! Kitu ambacho unatakiwa kuzingatia kila siku ni kama raha unazompa zina kiwango stahiki. Hakikisha huoneshi udhaifu kwenye kipengele chochote.
Mpaka hapo, bila shaka tumekubaliana kuzungumza ni muhimu, jukumu ulilonalo ni kuangalia aina ya mazungumzo. Yale ambayo hayachombezi, hayana mshawasha, hayahusu tendo, maana yake hayana mashika katika kipengele ambacho wewe nay eye mpo.
Haiwezekani katikati ya tendo unaongea: “Jana ulichelewa kurudi nyumbani.” Kuzungumza hivyo ni kujikosea wewe mwenyewe, kwani utamfanya mwenzi wako akatike stimu, kwa hiyo hata kiwango chake cha uwajibikaji kitapungua, hivyo hatakuhudumia kwa kiwango bora.
Nyongeza hapa ni kujiepusha na makelele. JJifunze kunong’ona, tena unong’onaji wenyewe ufanye masikioni mwake. Pata picha umemkumbatia mwenzi wako, hisia zake zipo juu na mshawasha (orgasm), unasomeka kwa asilimia 100, halafu wewe unamnong’oneza maneno matamu.
Kufanya hivyo, utamfanya mwenzio achanganyikiwe. Kama hujui, huo ndiyo uchawi ambao unaweza kumsababishia mpenzi wako awe anakuwaza kila anapokuwa mbali na wewe. Picha yako itamjia kichwani mwake kwa utamu, kila atakapokuwa anafikiria tendo.
Sasa basi, kuhusu kuzungumza na kutozungumza, nakushauri ujibiidishe kuzungumza kwa kunong’ona. Lainisha ulimi ili sauti yako iwe inatoka ikiwa imejaa mahaba. Nong’ona sikioni kwake, hapo ndipo utapatia. Hili siyo jukumu la kihisia, mwanaume na mwanamke, wote ni wajibu wao.

DHIBITI MAYOWE
Miguno ya mahaba na zile sauti tamu za malalamiko, zinaruhusiwa. Mayowe ambayo yanaleta kelele kwa kawaida hayaruhusiwi. Unashauriwa kuyadhibiti ili usigeuke kero kwa mwenzi wako, ukamnyima uhuru wa kufurahia tendo, kadhalika naye aweze kukuhudumia inavyotakiwa.
Busara hapa ni kwamba kwa nyumba zetu za Uswahilini, huwezi kupiga mayowe halafu ukakwepa kusikika nje. Hivyo basi, mayowe yako yanaweza kumfanya mwenzi wako ashindwe kujiamini, aamue kupunguza dozi ili kukufanya usiendelee kupiga makelele.
Atakapopunguza, itakufanya ukose uhondo uliostahili kutoka kwake. Vilevile hali hiyo, itamfanya mwenzi wako kupoteza umakini wa tendo, kwani badala ya kwenda nawe sawa, mkipanda na kushuka, anaweza kukutegea na kusikilizia zaidi makelele yako.
Msimamo wako ni mmoja tu, kuacha makelele! Kama kuna kungwi alikufundisha uwe ‘unabweka’ hovyo, kwamba ndiyo utamkosha roho mwenzi wako, huyo naye hajui. Badili mtazamo, fuata mwongozo huu ili ukuweke kisasa, vilevile ukujenge kimahaba zaidi.
HITIMISHO
Pitia vipengele 10 ambavyo nimevibainisha katika makala haya, vifanyie kazi, nakuhakikishia kwamba utakuwa mpya kimahaba, mwenye mtazamo wa kisasa. Wewe ni bora sana, ni suala la kujibiidisha tu na utaona matunda yake.

AKATWA NYETI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

AKATWA NYETI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Dustan Shekidele, Morogoro
MBALI na mtu mmoja kufariki dunia na wengine 24 kujeruhiwa na kulazwa kwenye Hospitali ya Bwagala, Turiani mkoani hapa, mwanaume mmoja amekatwa nyeti zake katika mapigano ya wakulima na wafugaji Jumanne iliyopita.
Mapigano hayo yaliyoshuhudiwa na mwandishi wetu yalipoteza amani iliyokuwa  kwenye Kijiji cha Dihombo Kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero.
Mashuhuda kadhaa walimwambia mwandishi wetu kwamba, mtu aliyekatwa  nyeti alikutana na wakulima hao wenye hasira waliokuwa wakimvamia mgeni yeyote waliyemuona  mbele yao.
“Wakulima walikuwa na silaha za jadi kama vile mapanga, mishale ya sumu na marungu, walimkuta mtu huyo aliyekuwa akipita na kumvamia kisha kumpiga na alipoanguka chini mkulima mmoja alimkata nyeti zake,” alisema shuhuda aliyejitambilisha kwa jina la Kibwana.
Mtu aliyekatwa nyeti (angalia picha ukurasa wa mbele) hakufahamika jina lake mara moja, lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba alikimbizwa hospitali ili kunusuru maisha yake.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima nao waliumizwa vibaya katika tukio hilo lililosababisha kifo cha mfugaji Yusuf Mdutu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa mapigano hayo huku akisema kuwa msako mkali unaendelea kuwakamata wahusika.

ALLY CHOKI AVUTA MKOKO KULINDA HESHIMA

ALLY CHOKI AVUTA MKOKO KULINDA HESHIMA

Stori: Shakoor Jongo
ILI kulinda heshima ya ukurugenzi, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki amevuta mkoko Toyota Prado yenye thamani ya shilingi milioni 52.
Mkoko mpya wa Ally Choki aina ya Toyota Prado ofisi za GPL.
Choki amenaswa na ndinga hiyo juzikati jijini Dar ambapo paparazi wetu alipomuuliza sababu za kuongeza ndinga hiyo ilihali ana magari mengine likiwemo Toyota Noah, Choki alitaja kigezo cha heshima kuwa sababu iliyomfanya anunune ndinga hiyo.
Muonekano wa mbele wa Toyota Prado.
“Unajua kila kitu kinakwenda na mipango lakini wakati mwingine heshima ya mtu inajengwa na vitu vidogovidogo hivyo niliona angalau ndinga kama hii inaendana na mimi, siyo kwamba nimenunua kuonesha jeuri, hapana lakini heshima nayo inahusika barabarani,” alisema Choki.
Kuhusu suala la kujipendelea kununua magari yeye kama mkurugenzi, Choki alisema yeye na bendi yake huwa hawana matatizo ya magari ya kusafiria ndiyo maana wana magari zaidi ya saba yanayotumika kwa shughuli za bendi.
Choki kama mkurugenzi na muimbaji, anakuwa mwanamuziki wa kwanza kumiliki gari la thamani katika wanamuziki wa dansi Bongo.

MTOTO ANYOFOLEWA JICHO

MTOTO ANYOFOLEWA JICHO

HAKIKA ni mateso na inauma kusikiliza maelezo yake.
MTOTO Khalidi Juma mwenye umri wa miaka minne, mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali baada ya jicho lake moja kutolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa, huku lingine nalo likilegea.
Mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo.
Akizungumza na gazeti hili, mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo, alisema alimzaa mtoto huyo akiwa na afya njema, lakini alipofikisha umri wa miezi tisa ndipo alipogundua kitu cheupe kwenye mboni ya jicho lake.
Baada ya hali hiyo, alisema alimpeleka katika hospitali inayotibu watu wenye ulemavu mbalimbali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar, ambako baada ya kupimwa, aliambiwa mwanaye alikuwa na kansa.
Mtoto Khalidi Juma  jicho lake moja limetolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa.
“Baada ya kuambiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa kansa sikuwa na jinsi, nilikubali afanyiwe upasuaji kwa ajili ya kuliondoa jicho hilo ili kuokoa maisha yake,” alisema.
Mama huyo alisema ilipofika mwaka 2012, jicho lingine lilianza kumuuma huku likiwa linavimba, lakini alipompeleka katika Hospitali ya Muhimbili, aliambiwa kansa imeshaenea mpaka kwenye ubungo, hivyo arudi naye nyumbani kwani hawezi kuishi kwa muda mrefu.
“Kwa kweli nilivyoambiwa hivyo nilinyong’onyea mwili mzima nikawa sina jinsi kabisa na nikapoteza matumaini kabisa ya mwanangu kuendelea kuishi tena,”alisema.
Alisema alirudi nyumbani huku maumivu ya kijana wake yakiendelea na mwishoni, jicho lake likawa halioni tena. Kuhusu jicho lililotolewa, mama huyo alisema alikuwa akilitoa na kulirudisha kwa ajili ya kulisafisha, lakini hivi sasa hawezi kulitoa tena kwa vile kuna nyama zilizolishika na hivyo kumsababishia maumivu makali mno mwanaye hasa kichwani.
“Unavyotuona hapa usiku hatulali kabisa, mtoto ni kulia kwa maumivu, amefikia wakati hawezi kula vizuri na anatumia muda mwingi kulia,” alisema.
Mama huyo aliongeza kueleza kuwa kutokana na hali ya mwanaye, anakosa muda wa kufanya chochote cha kujiingizi kipato, hivyo kuwa katika wakati mgumu mno kimaisha, hasa kwa vile baba mzazi wa mtoto huyo alimkimbia tokea alivyoanza kuumwa.
“Mimi naamini kabisa labda nikipata msaada nikienda hata kwa wachina nitapata hata dawa ya kumpunguzia mtoto wangu maumivu anayoyapata kwa hivi sasa,” alisema.
Kwa ye yote ambaye ataguswa na habari hii na angepeta kutoa msaada wa aina yo yote, anaweza kuwasiliana na mama mzazi anayetumia simu nambari 0656 042017.

MZEE WA UPAKO:NILIKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA

MZEE WA UPAKO:NILIKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA

LITOKEA lakini haikuandikwa kwa sababu haikudakwa! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi jijini Dar es Salaam (GRC), Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kuwa aliwahi kukamatwa na kuwekwa lupango katika Gereza la Keko, Dar kwa siku 14 akituhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ‘unga’, Risasi Jumamosi lina sauti yake.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’.
Akizungumza kwa uso wenye majonzi na siha ya huzuni mwishoni mwa wiki iliyopita kanisani kwake Ubungo- Kibangu, Dar, Mzee wa Upako alisema hawezi kuisahau siku hiyo ambayo shetani aliamua kukunjua kucha zake kumwelekea yeye.
Alisema ishu hiyo ilimkuta mwaka 2005 akiwa tayari mtumishi wa Mungu aliye hai, lakini anachomshukuru Mungu ni kwamba alimsimamia kwa nguvu zote.

MCHEZO MZIMA ULIVYOKUWA
Akizungumzia mchezo mzima ulivyokuwa, Mzee wa Upako alisema siku ya tukio (hakuitaja) akiwa kanisani hapo na waumini wake ghafla walitokea askari polisi ambao idadi yao haikumbuki.
Alipotaka kujua shida yao, walisema wao wanatokea Polisi Central, Dar na walikwenda pale kufanya naye mahojiano na kumpekua kwani alikuwa akihisiwa anajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.“Polisi walikuja kanisani wakafanya upekuzi, wakaenda nyumbani  nako wakafanya hivyohivyo kisha wakaondoka zao baada ya kutokuona chochote,” alisema Mzee wa Upako.
                                                                               Kamanda Nzowa.

POLISI WA INTERPOL WATUMIKA
Mzee wa Upako anaendelea kufunguka: Siku mbili mbele  wakaja wengine, wakasema wao ni Polisi wa Kimataifa (Interpol). Nao wakasema wamekuja kunipekua, lakini wao licha ya kutokukuta chochote walinikamata na kunipeleka Mahabusu ya Gereza la Keko, Dar ambapo nilikaa kwa muda wa kama wiki mbili.

AZITAJA SIKU ZA MAJARIBU
Mzee wa Upako: Hakika zilikuwa ni siku za majaribu kwangu kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, lilikuwa ni jambo ambalo sijawahi kulifanya achilia mbali kuliwaza.
Licha ya kukaa kwa wiki mbili kule mahabusu, Polisi wa Interpol nao walijiridhisha kwamba mimi sifanyi biashara hiyo, wakaniachia huru niendelee kumtumikia Mungu wangu.
                                                                 Madawa ya kulevya.

AWAGUNDUA WABAYA WAKE
Mchungaji huyo maarufu kwa msemo wake WATASHINDANA, LAKINI HAWATASHINDA aliendelea kusema kuwa aligundua kukamatwa kwake kulitokana na mpango wa siri uliofanywa na baadhi ya wachungaji wenzake (hakuwataja majina) kwa ajili ya kumdhoofisha kiimani.
“Zilikuwa ni mbinu chafu za kunidhoofisha kiimani kutoka kwa baadhi ya wachungaji wenzangu wenye wivu na huduma yangu. Lakini kwa jina la Yesu aliye hai walishindwa, watashindana lakini hawatashinda,” alisema Mzee wa Upako.

AHISI KUONDOLEWA HADHI
Mzee wa Upako alisema tukio hilo aliliona kama la kumwondelea hadhi katika jamii, hususan kwa waumini wake lakini kwa kuwa yeye ni ‘super charge’ kamwe hawezi kuruhusu imani yake iyumbishwe na hila za muovu shetani.

ANACHOMSHUKURIA MUNGU
Mchungaji huyo alisema baada ya kutoka Keko alimshukuru Mungu kwa vile hakuna chombo chochote cha habari kilichofuatilia juu ya sakata hilo na kwamba gazeti hili (Risasi Jumamosi) linakuwa la kwanza kuandika.
“Nashukuru hakuna chombo chochote cha habari kilichogundua juu ya habari hiyo, ninyi mnakuwa wa kwanza kuijua na hata kuiandika kama mtapenda,” alisema Mzee wa Upako.

APINGA DHANA YA WATUMISHI WA MUNGU KUUZA UNGA
Akizungumzia kwa undani sakata la watumishi wa Mungu kujihusisha na biashara ya unga, Mzee wa Upako alisema:
“Siamini kama kweli kuna watumishi wa Mungu wa hapa Tanzania wanafanya biashara hiyo. Kinachotokea ni kwamba, watu wamekuwa wakiwasingizia watumishi kwa sababu zao.”

WAUMINI WAKE SASA
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi liliwasiliana na baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambapo walisema mtumishi wao huyo amekuwa akionewa kijicho kutokana na mafanikio yake ya kiroho na kimwili.
“Sisi waumini wa GRC tukisikia lolote baya kuhusu Mzee wa Upako huwa hatushtuki kwa sababu wapo baadhi ya watumishi wa Mungu wanamuonea kijicho kwa sababu ana mafaniko ya kiroho na kiimani,” alisema muumini mmoja bila kutaja jina.
Mwingine alisema nguvu kubwa ya kiroho aliyonayo mtumishi huyo imemfanya aibue maadui wasio na hofu ya Mungu kwa kumpakazia skendo mbalimbali wakiamini akichafuka waumini watamkimbia.
Jumatano iliyopita, paparazi wetu alifika Kituo Kikuu cha Polisi (Police Central), Dar na kuulizia ishu hiyo ambapo afande mmoja alisema anayeweza kujua ni IGP Mstaafu, Omary Mahita ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya kiganjani kutokupatikana hewani.

VICTORIA HAMMAH: SIACHI SIASA HADI NIPATE DOLA MILIONI 1

VICTORIA HAMMAH: SIACHI SIASA HADI NIPATE DOLA MILIONI 1

Victoria Hammah amekuwa akisema amekuwa na shinikizo la kuiba pesa za umma.
Naibu waziri wa mawasiliano nchini Ghana Victoria Hammah ameachishwa kazi baada ya kunukuliwa akisema kuwa atasalia katika siasa hadi atakapo pata fedha kiasi cha dola milioni moja.

Anaonekana katika kanda ya video akisema kuwa ukiwa na pesa unaweza kuwashawishi watu. Bi Hammah bado hajatoa tamko lolote kuhusiana na mkanda huo wa video au hatua ya kufutwa kazi. Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema Bi Hammah alikuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa rais John Mahama mwaka jana.

Baada ya uteuzi wake baadhi ya wadadisi walionya kuwa ana umri mdogo sana kuweza kuhudumu katika serikali.Mwezi Agosti alinukuliwa akisema kuwa kuna shinikizo za kumtaka aibe fedha za umma kwa kuwa watu hudhani kwamba yeye ni tajiri kwa sababu ya wadhifa wake wa uwaziri.Katika kanda hiyo alisikika akisema kuwa hatatoka katika siasa hadi atakapopata dola milioni moja.Pia alisikika akimkosoa waziri mwenzake akisema hana akili,ana sura mbaya na anapenda sana kujigamba na kuwafokea watu. Chanzo ni BBC Swahili.

Friday, October 25, 2013

KIBIBI CHA MIAKA 86 CHAFANYA MAZOEZI YA KUCHANA MSAMBA

KIBIBI CHA MIAKA 86 CHAFANYA MAZOEZI YA KUCHANA MSAMBA

Ouyun, akichana msamba.
…Akiwa ameunyoosha mguu wake juu sambamba na mlingoti.
TAO OUYUN, kibibi chenye umri wa miaka 86 kutoka China, Jimbo la Zhejiang, kimeendelea kuwashangaza watu kwa kufanya mazoezi ya kuchana msamba na mengine yanayoonekana ya ajabu kwa watu wa umri wake ikiwa ni pamoja na kuunyosha mguu wake juu sambamba na mlingoti.
Kibibi huyo anafanya hivyo akiendeleza mchezo au mazoezi yanayojulikana kama Tai Chi ambayo amekuwa akiyafanya kwa miaka 36 sasa baada ya kustaafu kufanya kazi katika kiwanda cha kusokota nyuzi.

DUDE ADAIWA KUTOKA NA KIMADA WA MBUNGE

DUDE ADAIWA KUTOKA NA KIMADA WA MBUNGE

Stori: Gladness Mallya
STAA wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameshushiwa madai mazito kuwa ameingia penzini na kimada wa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalo), aliyetajwa kwa jina maarufu la Fetty.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kiko karibu na msanii huyo, mbunge huyo kwa sasa ameshagundua kuwa Dude ana uhusiano na ‘nyumba ndogo yake’ hiyo.
Taarifa hizo zilizidi kudai kuwa, hapo awali mheshimiwa huyo ‘hakukausha nyayo’ kwa mrembo huyo lakini baada ya kugundua hali ya ‘sintofahamu’ baina ya Fetty na Dude, amesitisha ukaribu na mrembo huyo.
Baada ya kutonywa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Dude ili kujua ukweli wa mambo, alipopatikana alisema:
“Ni kweli hata mimi hizo habari nimezisikia kutoka kwa wasanii wenzangu na zinaniumiza sana kwani mimi najua Fetty ana bwana wake tena mheshimiwa.
Naogopa sana kutekwa, naomba kupitia gazeti hili huyo mheshimiwa aelewe kwamba mimi sina uhusiano mbaya na mwanamke wake, tumefahamiana kupitia filamu tu,” alisema Dude.
Fetty alipotafutwa kwa njia ya simu,  iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

AUAWA KWA KUIBA KUKU WATATU!

AUAWA KWA KUIBA KUKU WATATU!

Stori: Mwandishi wetu, Mbeya
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Frank William Shoka (30) mkazi wa Kitongoji cha Katusi, Kijiji cha Mjere, Wilaya ya Mbeya vijijini mkoni hapa ameuawa kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid.
Kuku walioibiwa.
Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20, mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manani na kuchukua kuku hao wakati yeye akiwa hayupo.
Aidha, Dismas alisema baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa nao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya na alipomuuliza juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Hata hivyo, baada ya marehemu Shoka kushindwa kutoa maelezo sahihi juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga mazingira yaliyomfanya apoteze maisha.
Ndugu wakiwa na mwili wa marehemu.
NDUGU WAKAA NA MAITI KWA SAA NANE!
Hata hivyo, baada ya tukio hilo hakuna mwananchi hata mmoja aliyediriki kukaa na maiti hiyo isipokuwa ndugu wake ambao walikaa na marehemu kwa muda usiopungua saa nane.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji  hicho, Evarist Benny ambaye alitoa taarifa Kituo cha Polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi na  Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.

MMOJA WA KUKU WALIIBIWA ATAGA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati polisi wanakamilisha taratibu na kumkabidhi marehemu kwa ndugu,   mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai jambo lililozua mshangao miongoni mwa mashuhuda.

KUTOKA IJUMAA:
Si jambo jema hata bkidogo kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi, kwani sheria zipo ili zifuatwe na kama mtu amekwenda kinyume cha sheria hizo basi afikishwe kwenye vyombo vinavyohusika na sheria itachukua mkondo wake

DANGURO LA MADENTI LAFUMULIWA

DANGURO LA MADENTI LAFUMULIWA

Na Waandishi Wetu
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wamefanikiwa kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo mbalimbali jijini Dar.
Madenti hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro hilo lililopo ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.
KERO
Awali kikosi kazi cha OFM kilipokea malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Mzazi:Halooo…nazungumza na OFM?
OFM: Ndiyo…tukusaidie nini?
Mzazi: Mna habari?
OFM: Tunazo nyingi lakini ukitupatia ya kwako tutaifanyia kazi ipasavyo.
Mzazi: Tunawaamini OFM mnatisha kama njaa. Sisi ni wazazi wa hapa Buguruni-Sokoni. Kuna danguro hapa kwa kweli yanayofanyika ni aibu tupu. Tunaomba mje mjionee wenyewe mfanye kazi yenu.
OFM: Nini hasa kinafanyika?
Mzazi: Yaani vitendo vya ngono vinafanyika na sasa hivi hata kwa nje wapo watu wanafanya biashara haramu ya ngono hivyo watoto wetu wanashuhudia vitu vya ajabu na kondomu zimezagaa kila kona.
OFM: Sawa, tuachie tufanye kazi yetu.
Mzazi: Oke, lakini naomba chondechonde msinitaje wala kuonesha namba yangu kwa sababu hii ni biashara ya watu nitamwagiwa tindikali bure!
OFM: Tunaheshimu vyanzo vyetu hatuwezi kukutaja popote kwani siyo maadili ya kazi yetu.
OFM KAZINI
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, vijana wa OFM waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya makachero wa OFM walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za kutosha huku wakiwarekodi wahusika (madenti wanaojiuza na wanaume wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya kazi bila wao kushtuka.
BEI
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia buku mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na kuendelea.
Mmoja wa vijana hao wa OFM alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji ambapo alipofika na kujionea mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo kuwa alikuwa amepokea simu ya dharura.
USHUHUDA MBAYA
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani, anasimulia: “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.”
TAARIFA POLISI
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua danguro hilo, OFM iliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo.
Bila kusita, kamanda huyo aliteua vijana wake kutoka Kituo Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.
DENTI IFM
Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa na polisi, mmoja wa madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.
Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja hicho cha maasi ni denti aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.
Denti mwingine aliyekamatwa katika msala huo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.
MUUZA KONDOM NAYE MBARONI
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa njemba mmoja aliyekuwa ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.
Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza mwili.
NYUMA YA NONDO
Baada ya kuhojiwa kuhusika na biashara haramu ya ngono na kukiri, watuhumiwa hao wote waliwekwa nyuma ya nondo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la kesi namba BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
WAZAZI SOMENI HAPA
Uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa madenti hao na wengine wengi jijini Dar, wamekuwa wakiaga kwao kuwa wanakwenda masomoni lakini kumbe wanaishia kwenye madanguro yaliyojazana jijini kwa ajili ya kujiuza.
Huku wazazi wakitoa fedha nyingi na huduma nyingine wakiamini watoto wao wanasoma, hali ni tofauti kwani madenti wengi wamekuwa wakiishia kwenye vitendo vya kihuni na kufeli masomo na maisha kwa jumla kisha kugeuka mzigo kwa familia.