KIBIBI CHA MIAKA 86 CHAFANYA MAZOEZI YA KUCHANA MSAMBA
TAO OUYUN, kibibi chenye umri wa miaka 86
kutoka China, Jimbo la Zhejiang, kimeendelea kuwashangaza watu kwa
kufanya mazoezi ya kuchana msamba na mengine yanayoonekana ya ajabu kwa
watu wa umri wake ikiwa ni pamoja na kuunyosha mguu wake juu sambamba na
mlingoti.
Kibibi huyo anafanya hivyo akiendeleza
mchezo au mazoezi yanayojulikana kama Tai Chi ambayo amekuwa akiyafanya
kwa miaka 36 sasa baada ya kustaafu kufanya kazi katika kiwanda cha
kusokota nyuzi.
No comments:
Post a Comment