Friday, August 29, 2014
RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MBANDE-KONGWA 16.5KM
CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA ULAYA
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA HABARI BILA KUPOTOSHA UMMA
KAMPUNI YA MATANGAZO YANAYOTEMBEA (TRIA) YAZINDULIWA RASMI TANZANIA
DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA akisoma risala yake wakati wa uzinduzi wa matangazo hayo.
TRUSHAR
KHETIA Mkurugenzi Mtendaji wa TRIA akikata utepe wakati akizindua rasmi
matangazo hayo nchini Tanzania, wa pili kulia ni ZULFIKAR MOHAMED
Meneja Mkuu wa kampuni ya TRANSPAPER EXPRESS na mwisho kulia ni DIANA
LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA na kushoto ni
AZDA AMANI Meneja wa Huduma Shirika la ndege la PRECISION AIRLINE ambao
ni wateja wa kampuni ya TRIA.
Kampuni ya matangazo kwa kutumia vifaa tembezi yaani matangazo yanayotembea imezinduliwa rasmi jijini Dar esSalaam.
Akiongea na waandishi wa habari pamoja na
wageniwengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi ulifanyika
katika hanga la shirika la ndege la Precision yenye makao makuu yake
eneo la uwanja wa ndege jijini Dar esSalaam, mkurugenzi mtendaji na
muasisi wa TRIA bw. Trushar Khetia amesema kuwa TRIA ni kampuni ya
kimataifa inayojishughulisha na matangazo yawekwayo juu, nje au ndani ya
fifaa safirishi kama mabasi ya kusafiria ndani na nje ya miji, ndege na
usafiri wa majini maarufu kama boti au meli.
“Tumezoea kuona ama kusikia matangazo
malimbali ya kibiashara nay ale ya kijamii yaani matangazo yasiyo ya
kibiashara yakifanyika kupitia kwenye TV REDIO magazeti na majarida hapa
nchini lakini leo TRIA inawathibishia wafanya biashara wa Tanzania na
wengine kuwa matangazo yanaweza kufanyika popote wakati wowote tena kwa
gharama ndogo” alisema bwana Trushar na kuongeza kuwa TRIA ina lenga
kuwainua watanzania hasa vijana wadogo na kuwafanya watambue fursa zao
katika maisha sambamba na kuwaongezea matumaini makubwa wamiliki wa
mabasi, ndege, daladala namakapuni ya usafirishaji katika kunufaika
kutokana na biashara zao za usafirishaji.
Aidha bwana Trushar amesema kuwa kampuni
yake pamoja na kwamba haitegemi kufanya biashara kwa hasara hailengi pia
kutengeneza faida tu bali kuleta ufanisi na changamoto endelevu katika
sekta ya masoko na matangazo ambapo vijana wadau na wateja wa huduma
hiyo wataweza kupiga hatua za kimaendeleo kibiashara sambamba na
kuongezeka kwa soko la ajira hususana kwa vijana wa kitanzania “TRIA
Tanzania hailengi kutengeneza faida tu bali pia kuleta maendeleo yenye
tija kibiashara kwa wale watakaokuwa wateja wetu na wadau kwa ujmla,
lakini pia ajira kwa vijana wenye uwezo tofauti tofauti wa kufanya kazi
pamoja na wale wenye utaalamu wa kuandaa na kutengeneza matangazo haya”
alisema Khetia.
Kwa upande wake mwakili wa Conica katika
hafla hiyo Bi Diana Lavender amesema Conoca imekuwa mteja mkubwa wa TRIA
nchini Kenya na kwakutambua ubora wa kazi zinafanywa naTRIA Conica
imeamua kuunga na TRIA kwakuendelea kufanya matangazo yake hapa chini
“tumekuwa wateja wa hii kampuni mda mrefu sasa huko nchini Kenya na
kutoka na mafanikio makubwa tumeweza kupata kupitia matangazo yetu
yanayofanywa na TRIA tumeonelea kuwa ni vizuri kuja kufanya hayo
matangazo hapa Tanzania hasa pale tuliposikia kwamba TRIA inaanzisha
tawi hapa nchini” alisema Lavender na kuongeza kuwa kufanya matangazo
kupitia mabasi, ndege, daladala, treni, vyombo vya usafiri wa majini ni
sehemu ya mapambo ya mji na njia zake kwani matangazo haya hutengenezwa
vizuri na kufanya kuvuta macho ya wengi kila ipitapo “ni ma mabasi yetu
huko Kenya maarufu kama matatu ukipita ukiona vile inavutia lazima
utafurahia na kwamba lazima unaweza kutaka kupanda hiyo basi” aliongeza.
Naye mwakilishi kutoka shirika la ndege la
precision hapa nchini ambao ni moja kati ya wadau wa karibu kabisa na
TRIA Bi Azda Amani amesema kuwa uwekezaji wa biashara mbalimbali hasa
biashara ngeni kama hayo ni sehemu ya kuongeza na kukuza pato la taifa
na kupitia kodi kwa kampuni husika lakini pia kwa wamiliki wa mabasi,
ndege na vinginevyo pamoja na wale wamiliki wa matangazo yatakawekwa
kwenye magari haya watalipia kodi “ni furaha kuona wawekezaji wakubwa na
wadogo wakiingia kila siku hapa nchini kuwekeza kibiashara na
kwakufanya hivi nchi yetu ina kuwa pia kiuchumi kupitia kodi kutoka kwa
watoa huduma na wahudumiwa wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi
na biashara nchini” alisema Amani
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Zulfikar
Mohamed kutoka Transpaper ameisifia TRIA kwa hatua iliyofikia na
kuwataka watanzania kuiga mfano huo muhimu na kwenda kuwekeza pia katika
nchi jirani hata kimataifa “ mimi nipewa fursa ya kuzindua tawi la TRIA
hapa Tanzania na kwakweli nimefurahia fursa hii.
Naomba kuwapongeza sana wahusika wote
waliokaa na kuona kwamba mimi naweza kuwa mgeni rasmi wa kuzindua mradi
huu muhimu lakini pia nawasifia watanzania kwa kuwa waungwana wakubwa
sana kuwapokea wawekezaji kutoka pande zote za dunia bila kujali rangi
kabila wa udini, kwa hili mko vizuri sana na nawapongeza sana niwaombe
tu kwamba igeni huu mfano mzuri na nyinyi mkawekeze biashara zenu katika
nchi nyingine kwa manufaa ya watoto wenu na watanzania wote” alisema
Mohamed nakuongeza kuwa maendele ya kiuchumi katka taifa lolote huletwa
na wenye nchi kupitia biashara yenye tija na inayovuka mipaka na kuleta
fedha za kigeni.
WAPIGANAJI WA ISIS WATOA ONYO LINGINE KWA MAREKANI
Mateka 15 wa Kikurd wanaoshikiliwa na wapiganaji wa ISIS.
SAA chache baada ya kuuwa wanajeshi 300 wa Syria, Kundi la wapiganaji
wa ISIS limetoa onyo lingine kwa Marekani likiachia video
inayowaonyesha mateka 15 wa Kikurd ambao nao watauawa iwapo Marekani
haitaondoa majeshi yake.
ISIS wamesema wataendelea kuwachinja mateka hao mpaka Marekani itakapoondoa majeshi yake.
Katika video hiyo, Kundi la ISIS linaonekana likimchinja mmoja wa
mateka hao wa Kikurd waliokamatwa wakati wa mapigani nchini Iraq.
Wapiganaji
wa ISIS wakiwaswaga wanajeshi zaidi ya 200 waliokamatwa katika ngome ya
anga ya Tabqa nchini Syria katika jangwa kuelekea eneo la mauaji.
Tuesday, August 12, 2014
Bunge kutumia zaidi ya Tsh milioni 142 kukodi vipaza sauti
Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha (AICC).
Katibu wa Bunge maalumu Yahya Khamis Hamad alithibitisha kukodiwa kwa
vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12 na kwamba kila gharama ya
chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani (Dola moja ni wastani wa
Sh1,650).
Kwa maana hiyo Bunge hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni
kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na
kamati hizo na kwa siku 16 ambazo kamati zitakutana, jumla gharama hizo
zitafikia Sh142.56.“Vifaa vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa vilikuwa siyo standard (viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka ukumbi wa mikutano wa AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifunga,” alisema katibu wa bunge.
Ushahidi mwingine wa Chris Brown na Rihanna wapo karibu kurudiana
Japokuwa picha haipo clear sana lakini inaonyesha Chris Brown alivyokwenda back stage ambapo alikuwepo Rihanna kwenye moja ya show za tour hiyo.
Picha haionyeshi vizuri lakini kuna mashahidi wengi wanasema kwamba Chris Brown alikuepo backstage akiwa na Tyga na welienda kwa ajili ya Rihanna.
NAY NDIYE ‘MDUDU’ NDOA YA WEMA
IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki.
Ushauri huo umekuwa mwiba kwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu ambaye amekuwa na ndoto ya kuolewa na staa huyo anayekimbiza kitaani na wimbo wake wa Mdogomdogo.
Akifafanua zaidi kuhusiana na ushauri huo, Nay alisema: “Kuna mifano mingi sana nimeiona kutoka kwa wasanii ambao wameoa, wengi wao wameshasanda sasa mdogo wangu (Diamond) na yeye alipoleta hoja ya kutaka kuoa nikaona sasa anatafuta shimo la kwenda kujifukia, nikamshauri aache.”
MATUKIO 9 YALIYOFURAHISHA
Ijumaa iliyopita ni siku ambayo haitasahaulika kwenye kumbukumbu za wengi kutokana na kufanyika kwa tamasha kubwa la Usiku wa Matumaini ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yafuatayo ni mambo tisa yaliyotingisha kwenye tamasha hilo.
Timu hizo zilipoingia uwanjani kupasha misuli, watu walisimama na kuanza kushangilia kwa nguvu huku wakilitaja jina la Ali Kiba na zaidi walifurahi walipomuona Jacob Stephen ‘JB’. Matokeo ya mechi hiyo, Bongo Fleva waliwalaza Bongo Muvi kwa bao 1-0.
VIDUKU VYA BONGO MUVI
Japokuwa walifungwa, wanawake wa Bongo Muvi walionekana wakicheza kiduku huku mashabiki wakiwashangilia kwa nguvu na kuleta shangwe za aina yake.
SHOO KALI YA ROMA, JUMA NATURE
Wakali hawa wa muziki wa Bongo Fleva waliwafurahisha sana mashabiki ambapo uwanja mzima ulisimama na kucheza huku wakiimba nyimbo za wasanii hao wakati wakipafomu.
NDONDI ZA JB, CLOUD
JB na Cloud 112 walionekana kama wanaigiza kwani walikuwa wanadondoka mara kwa mara wakati pambano baina yao likiendelea, baadaye JB aliibuka na ushindi.
MASHABIKI KUSHANGILIA KWA STAILI MBALIMBALI
Ukweli ilikuwa ni siku ya matumaini na furaha kwani mashabiki kila mmoja alikuwa akishangilia kwa staili yake, wapo waliovua mashati na kubaki tumbo wazi huku wakicheza, wapo mashabiki wa kiume waliokuwa wanakata mauno kama wanawake na kuwa kivutio kikubwa uwanjani hapo.
SHILOLE KUTAKA KUVUA NGUO
Hii ilikuwa ni hatari kwani mwanadada wa muziki wa mduara , Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alifanya shoo ya nguvu lakini wakati anataka kufika mwisho akataka kuvua nguo kutokana na mzuka aliokuwa nao kwani alikuwa akiimba ‘nivue muone’ mashabiki nao wakawa wanaitikia ‘vua’, watu walipiga kelele za furaha kutokana na kufurahishwa na shoo ya mwanadada huyo.
SHABIKI KUMGANDA MBUNGE
Ukiwa na mapenzi na kitu hutaona aibu! Baada ya wabunge kumaliza mechi shabiki mmoja alipenyeza uwanjani na kumganda mheshimiwa Mwigulu Nchemba huku akiwa amevua shati na alipokuwa akizunguka naye uwanjani alikuwa akifika sehemu anapiga magoti kwenye miguu ya mheshimiwa huyo na kunyoosha mikono juu na kuwa kivutio kwa watu waliokuwepo uwanjani hapo.
SHOO YA KIBA, YEMI FUNGA KAZI
Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba kufanya shoo ya nguvu alifuatiwa na mwanadada huyu kutoka Nigeria, Yemi Alade ambapo mashabiki walifurahia kwani walikuwa wamemsubiri kwa muda mrefu.
ALI KIBA KUBEBWA
Kutokana na kufanya shoo nzuri, Ali Kiba alijikuta katika mikono ya msanii wa muziki na filamu, Simon Mwapagata ‘Rado’ ambaye alimbeba na kumzungusha uwanjani hapo huku akiimba, ukweli ilikuwa noma sana!
MWIGULU, RIDHIWANI KIKWETE MZUKA 100%
KWELI raha jipe mwenyewe!
Usemi huo ulidhihirika wikiendi iliyopita ndani ya Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini (Night of
Hope) ambapo wabunge mashabiki wa Yanga walikipiga na wabunge mashabiki
wa Simba na kutia fora kwa kushangiliwa wakati wa mtanange huo.
Katika mchuano huo, wabunge wa Yanga
waliwagaragaza wa Simba kwa mabao 3-2 hali iliyosababisha uwanja ulipuke
kwa kelele za kushangilia kutoka kwa mashabiki na wapenzi halisi wa
Yanga waliokuwepo uwanjani hapo.
Kama vile hiyo haitoshi, baada ya kipyenga cha mwisho, wabunge wa
Yanga walipanda mzuka na kuanza kuuzunguka uwanja wakisherehekea ushindi
wao.Wabunge waliotia fora zaidi kwa kushangilia huku wakionesha hisia kali ni Mbunge za Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete ambaye baada ya ushindi huo alikimbilia kwa mashabiki wa timu hiyo na kuvua jezi yake ya juu na kuwatupia, hali hiyo iliyomfanya kubaki tumbo wazi.
Naye Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alikuwa sanjari na Ridhiwani ambapo yeye aliwarushia mashabiki wake ‘skafu’ aliyokuwa amejifunga shingoni, hali ambayo ilimfanya shabiki mmoja kuchomoka alikokuwa na kumfuata mheshimiwa huyo uwanjani na kuungana naye kushangilia.
Wakati huo, shabiki huyo alikuwa amevua shati na kuonekana kutoamini macho yake kwani kila wakati alikuwa akipiga magoti na kumshika miguu mheshimiwa huyo.
Matukio ya wabunge hao yaliwafurahisha mashabiki waliokuwa uwanjani hapo na shangwe kuwa kubwa kupindukia.
“Jamani sijui niseme nini, najiona kama naota hivi kwa sababu nampenda sana Mwigulu na leo nimemuona na nimemshika na kushangilia naye.
Nina raha sana na sijutii kuja kwenye tamasha hili,” alisikika akisema shabiki huyo.
Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti kwa wabunge wa Simba ambao baada ya kipigo hicho, walianza kulalamika kuwa wamehujumiwa na refarii wa mchezo huo, Othman Kazi.
Kwa upande wa muziki, mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade aliwakonga nyoyo mashabiki na baadaye akakiri kwamba alifikiri itakuwa ni shoo ndogo, kumbe ni kubwa kiasi hicho, akaeleza jinsi alivyofurahi na kutamani kualikwa tena Tanzania.
AUNT EZEKIEL: NITAHAKIKISHA NAMPA PENZI MUME WA MTU
Makubwa! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefungukia madai ya kutoka na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa mtu akisema hakuna ukweli wowote zaidi ya kutaka kuchafuliwa.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunt ambaye gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko liliripoti tukio la kutaka kufanyiziwa na mke wa dansa huyo aitwaye Mwengi Ally, alisema anamshangaa mwanamke huyo lakini ili kumkomoa atahakikisha anafanya kweli ili kama ni kunuka, kinuke kihalali.
Alisema kwamba yeye ni mke wa mtu asiyeweza kujirahisi kwa kutembea na kijana huyo na kwamba kama ni kujuana ni kwa sababu ya Diamond ambaye ni shemeji yake kwa Wema.
“Amenichafulia sana, siwezi kutembea na Moze, najiheshimu. Lakini kwa kuwa ameamua kunipakazia, nitahakikisha namtega mumewe na nikimnasa nampa penzi ili kama ni hizo vurugu azifanye kihalali,” alisema Aunt na kusisitiza:
“Siwezi kuwa na uhusiano na Moze, yule mwanamke alikuwa na nia ya kuifanya jamii inifikirie vibaya lakini amenoa.” Hivi karibuni kundi la watu likiongozwa na Mwengi lilifika nyumbani kwa Wema Sepetu likimsaka Aunt ili kumshikisha adabu kutokana na madai ya kutoka na mume wa mtu huyo.
JOKATE, DIAMOND WAONEANA AIBU!
Kwa mara ya kwanza tangu walipomwagana, mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wanadaiwa kuoneana aibu walipokutana laivu.
Akiwa na mtangazaji mwenzake, Edzen Jumanne, wikiendi iliyopita Jokate alidaiwa kushindwa kumbana Diamond kwa maswali wakati akimhoji kwenye kipindi kitakachoruka hewani hivi karibuni kupitia TV1.
Baadaye Diamond alitupia mtandaoni picha akiwa na zilipendwa wake huyo hivyo kuibua mjadala mzito kuwa huenda bado wanapendana huku wenyewe wakipiga kimya.
Subscribe to:
Posts (Atom)