Kwa mara ya kwanza tangu walipomwagana, mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wanadaiwa kuoneana aibu walipokutana laivu.
Akiwa na mtangazaji mwenzake, Edzen Jumanne, wikiendi iliyopita Jokate alidaiwa kushindwa kumbana Diamond kwa maswali wakati akimhoji kwenye kipindi kitakachoruka hewani hivi karibuni kupitia TV1.
Baadaye Diamond alitupia mtandaoni picha akiwa na zilipendwa wake huyo hivyo kuibua mjadala mzito kuwa huenda bado wanapendana huku wenyewe wakipiga kimya.
No comments:
Post a Comment