Thursday, February 28, 2013
ILIKUWA LAZIMA WAFELI
MBALI na mfumo mbaya wa elimu unaolalamikiwa na wadau nchini kwamba umechangia matokeo mabaya ya kidato cha nne, lakini vitendo wanavyovifanya wanafunzi wakiwa shuleni pia vina mchango wa matokeo mabaya, Amani limechimbua.
Mitandao mbalimbali ya Bongo, imerusha picha kadhaa zikiwaonesha wanafunzi wakiwa katika vitendo vinavyoashiria ufuska, usagaji na ngono. Amani lilipata bahati ya kuzungumza na wadau, walimu na wazazi ambapo baadhi yao walikiri kuwa kuna wanafunzi wanaoendekeza vitendo vichafu wakiwa shuleni hali inayosababisha kufanya vibaya katika mitihani.
“We fi kiria, mwanafunzi wa kike anakwenda shuleni akiwa na simu yenye intaneti, anaona matukio machafu ya duniani, huyu anaweza kuzingatia masomo kweli? “Mbaya zaidi, vitendo wanavyoviona kwenye mitandao na wao huviiga kwa kuvifanya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Bakari Mzuri, mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam.
Ikazidi kuelezwa kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wa kike wana uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kiume au watu wazima wa mitaani.
Pia imebainika kuwa wapo wanafunzi, hasa wa vyuo, wanapofunga shule badala ya kurudi kwa wazazi wao kusaidia majukumu ya
kifamilia wanakwenda kuishi na wapenzi wao sehemu nyingine huku wakidanganya makwao kwamba wametakiwa kubaki zamu.
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanaonesha hivi:
Divisheni 0 ni 240,903 (60.1%), divisheni IV ni 103,327 (26%), divisheni III ni 15,426 (3.9%), divisheni II ni 6,433 (1.6%) na divisheni I ni 1,641 (0.49%).
Wakati huohuo, wazazi nchini wamelalamikia matumizi tofauti ya vitabu vya masomo wakisema pia yanachangia matokeo
mabaya ya mitihani.
Walitoa mfano kwa kusema kuwa, utakuta kitabu cha hesabu darasa la nne shule ya msingi ya serikali siyo kinachotumika
shule za msingi za binafsi, hali inayosababisha uelewa tofauti wa wanafunzi.

GOOGLE WAJA NA MIWANI INAYOPIGA NA KUREKODI PICHA KWA MAELEKEZO
TEKNOLOJIA waliyotumia Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na kitu kama "Skype-style video chat".
Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.

Google glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikoni yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass
unaweza tolewa baa.
Kwa nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh. mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani, sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
USIJIDANGANYE…BILA MPENZI MAISHA HAYAWEZI KUWA KAMILIFU
TUNAKUTANA tena kupitia safu hii nikiamini u bukheri wa afya na unaendelea vyema na mishemishe zako za kimaisha kama kawaida. Mimi namshukuru Mungu kwani amekuwa akinitendea mema katika kila siku ya maisha yangu.
Mpenzi msomaji wangu, katika ulimwengu wa mapenzi kuna mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza na kuwafanya baadhi ya watu kuishia kusema kuwa ni bora waishi peke yao kuliko kuwa na wapenzi.
Wanaosema hivyo ni wale ambao wametendwa kwa kiwango kikubwa. Wapo ambao wametokea kuwapenda sana wapenzi wao lakini kinyume chake ikawa ni kulizwa kila siku huku usaliti ukiwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Kimsingi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa na mtu ambaye moyo wako umempa nafasi kubwa sana. Zaidi ya yote inaumiza sana unapompenda mtu lakini yeye akawa hakupendi, matokeo yake yakawa ni mpenzi kukutesa. Kwa hayo kweli unaweza kufikia wakati ukasema ni bora kumuacha na kuishi peke yako.
Cha kujiuliza ni kwamba, ni kweli unaweza kuishi peke yako bila kuwa na mpenzi? Ni wangapi ambao waliwahi kusema hivyo lakini leo hii wako kwenye uhusiano na watu wengine? Ni wengi tu na imetokea hivyo kwa kuwa, mapenzi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya binadamu.
Hata kama una uwezo mkubwa kiasi gani lakini huwezi kusema umetosheka bila kuwa na mpenzi na ndiyo maana wapo ambao wana kila kitu lakini mapenzi yakiwakorofisha kidogo tu wanakonda na kutoona umuhimu wa kuendelea kuishi.
Ndiyo maana tunaambiwa kwamba, tunapokwazwa na wale tuliotokea kuwapenda sana tusione kuwa ni mwisho wa sisi kupenda. Tuone ni hatua ya kuelekea kuwapata wale wenye mapenzi ya kweli na sisi.
Nimeshawahi kusema huko nyuma kwamba, wale ambao leo unawaona wako kwenye uhusiano bora wenye furaha wengi waliwahi kutendwa sana, nikasema katika safari ya kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ni lazima uwe tayari kuumizwa kwanza, huo ndiyo ukweli wenyewe.
Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakata tamaa ya kuwa na mpenzi baada ya kuumizwa na mtu wa kwanza. Hivi unajuaje kama baada ya huyo utampata yule uliyepangiwa na Mungu?
Tusiwe watu wa kukata tamaa mapema na kufikia hatua ya kusema hauko tayari kupenda. Kama hauko tayari kupenda basi utakuwa hutaki kuendelea kuishi na kama ni hivyo ni bora uondoke tu duniani.
Najua wakati mwingine tunatamka maneno hayo kwa hasira hasa tunapofikiria jinsi tulivyopoteza muda wetu kwa watu tuliotokea kuwapenda sana lakini maumivu hayo yasitupeleke kule ambako tunaweza kuyaharibu maisha yetu kwa kupoteza furaha.
Wapo ambao eti mpaka leo wanajifanya ni wagumu. Hawataki kuwa na wapenzi kwa sababu waliwahi kutendwa. Sikatai, hayo ni maamuzi ya mtu lakini watu hao ukijaribu kuwafuatilia utabaini wanakosa furaha iliyokamilika. Wanajikaza wakidhani wanaziridhisha nafsi zao lakini kiukweli wanaathirika sana.
Naomba nisema tu kwamba, unaposema hutaki tena kuwa na mpenzi unajiweka kwenye mazingira mazuri ya kuathirika kisaikolojia. Mpenzi ni muhimu sana kwenye maisha yako lakini uvumilivu pia unatakiwa kuchukua nafasi yake.
Mpende akupendaye na asiyekupenda achana naye ili kumpa nafasi yule ambaye Mungu amepanga kuwa wako. Unapofanyiwa yale ambayo hukutarajia kufanyiwa na ‘mtu’ wako, kama yanavumilika, vumilia lakini kama unaona yanaukwaza moyo wako, muweke pembeni kisha kuwa na subira kwani naamini Mungu hawezi kukutupa.
NDOA ZA MASTAA... ZILIZODUMU, ZINAZOSUASUA NA ZILIZOVUNJIKA
MAANDIKO katika vitabu vitakatifu yanaainisha kuwa mwanamke atamwacha baba na mama yake, ataambatana na mumewe na kuwa mwili mmoja. Vivyo hivyo kwa mwanaume! Hiyo ndiyo ndoa, haijalishi itakuwa imefungwa kidini, kimila au kiserikali (bomani).
Kwenye ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, ndoa kadha wa kadha zimefungwa katika miaka tofauti. Zipo zilizodumu, zinazosuasua na nyingine zimevunjika baada ya wahusika kutofautiana.
Wiki hii Amani linakuchambulia baadhi ya ndoa za mastaa kama ifuatavyo, shuka nayo.
Ndoa ya mwigizaji Aunt Ezekiel aliyofunga na Sunday Demonte mwaka jana, inadaiwa kusuasua kwani tangu bibie aolewe, mumewe alitimkia Dubai huku staa huyo akiahidi kumfuata bila kutimiza ahadi hiyo. Haina tofauti na ile ya staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya aliyeolewa na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwaka 2009 na kudaiwa kuvunjika mwaka jana. Ndikumana alitimka Bongo na kurudi kwao Rwanda akimwacha bibie Bongo akiendelea kula maisha.
Ndoa ya mwanamitindo Jacqueline Patrick aliyofunga na Abdulatif Fundikira mwaka 2011 hivi karibuni ilidaiwa kusuasua. Wakati mume akiwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya mihadarati, mke anadaiwa kujivinjari na wanaume wengine sawa na ya Mbongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’ (2007) ambayo nayo haiko sawa kivile kwani tangu mwaka jana, mke anaishi kivyake Mwanza huku jamaa akitanua Dar.
Kama ni pongezi, zinapaswa kuangushwa kwa mwigizaji Subrina Rupia ‘Cathy’ aliyeolewa na Salim Rupia mwaka 2002, Jacob Steven ‘JB’ aliyeoa mwaka 2004, mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na mumewe Gardner G. Habash ambao walioana mwaka 2005 na wanadumu hadi leo.
Wengine ni Wabongo Fleva Lawrence Marima ‘Marlaw’ na Besta Gasper ambao walioana mwaka 2011 na Joyce Kiria aliyeolewa na Henry Kileo mwaka 2011 ambao hadi leo wanafurahia maisha.
Marlaw na Besta, Banana Zoro na Suzan walioana mwaka 2008, wanatoa ishara nzuri ya kudumu kwenye ndoa kwa wasanii wachanga wa Bongo Fleva kama Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ambaye hivi karibuni alimuoa Halima Ally.
Pia tumsikilizie Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ aliyemuoa Fatma Abdallah mwaka 2011.
Ndoa ya Mtangazaji Hadija Shaibu ‘Dida’ aliyeolewa na Gervas Mbwiga mwaka 2011 ilivunjika mwaka jana tofauti na mwenzake, Sauda Mwilima aliyeolewa na Kauli Juma ‘Best’ mwaka 2012 ambao wanaogelea kwenye mahaba hadi leo.
Baada ya mateso ya ndoa yake ya awali na marehemu William Limbe ‘Ng’wizukulu Jilala’ ambaye alipewa talaka kabla ya mumewe huyo kupatwa na umauti, mwaka 2010, mwigizaji Nuru Nassor ‘Nora’ aliolewa tena na Masoud Ally ‘Luqman’ lakini ndoa hiyo ya pili bahati mbaya ilivunjika mwaka jana.

CLOUDS FM YAIBUKA NA TUZO YA UBORA (SUPERBRANDS) KWA MARA YA TATU MFULULIZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo
lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mradi Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer akimkabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa. Joseph Kusaga mara baada ya Clouds Fm Radio kuibuka na tuzo hiyo ya Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
WAZIRI MUHONGO ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA BG
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa injinia wa BG Group.
Profesa Muhongo akisalimiana na CEO wa BG Group, Chris.
Profesa Muhongo akifuatilia maelezo ya ramani kutoka kwa msemaji wa kampuni ya BG.
Profesa Muhongo akiwa Control room ya kampuni ya BG Group.
Picha ya pamoja.
Urban Pulse Creative inakuletea picha za ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo alipotembelea makao makuu ya kampuni ya BG inayofanya kazi ya uchimbaji wa gesi na mafuta ili kuangalia ufanisi wake na namna gani inavyoweza kutufaa Watanzania ikiwekeza nchini kwetu.

Monday, February 25, 2013
DIDA ANASWA NA VIATU VYENYE SILAHA
MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida,’ hivi karibuni alinaswa akiwa amevalia kiatu ambacho kina silaha.
Kiatu hicho ambacho ni moja ya fasheni zilizoingia, kina misumari pembeni kiasi kwamba akikurushia teke, ni lazima kikutoboe.
Baadhi ya watu waliokiona kiatu hicho walisema kuwa, licha ya kwamba ni fasheni lakini atakayekivaa lazima watu wamgwaye.
“Sasa hiki ni kiatu au silaha? Ukikivaa kwenye msongamano wa watu si utajeruhi, mh! Hizi fasheni za sasa mbona balaa,” alisema Zuhura wa Kinondoni.

RAY AKONGOROKA
MWIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ amezua hofu kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake baada ya kukongoroka ghafla akihisiwa anaumwa, Ijumaa Wikienda limemfuatilia hatua kwa hatua.
KWENYE ‘BETHIDEI’ YA BATULI
Wiki kadhaa zilizopita paparazi wetu alishtuka alipomuona Ray kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji sistaduu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ndani ya Hoteli ya Shamoll iliyopo Sinza ya Lion, Dar akiwa amekongoroka na kuibua maswali kwa wahudhuriaji.
Akiwa ukumbini hapo, minong’ono ilienea kuwa Ray alionekana kukondeana katika kipindi kifupi huku baadhi ya watu wakisikika wakiulizana kulikoni kwani alikuwa meza moja na bonge la mtu, Jacob Steven ‘JB’ hivyo kumfanya kuonekana mdogo mno.

Vincent Kigosi ‘Ray’ alivyokuwa mwaka jana.
VIWANJA VYA LEADERS
Akiwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki iliyopita, Ray aliibua mshtuko kwa mara nyingine hadi jamaa mmoja anayedhaniwa kutokuwa vizuri kichwani kumfuata na kumuwakia akimuuliza kwa hasira kuwa kulikoni akondeana kiasi hicho.
UZINDUZI WA WEMA
Kwa mara nyingine, Ray alizua hofu alipohudhuria kwenye uzinduzi wa ofisi ya Wema Sepetu uliofanyika maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alipoingia watu walipigwa butwaa wakimtazama na wengine kumuonea huruma wakidhani anaumwa.
IJUMAA WIKIENDA LATAKA MAJIBU
Kwa nyakati tofauti, wanahabari wetu walizungumza na Ray ambaye alitoa majibu ya kukinzana na kuzidi kutia shaka.
Ray alimwambia mmoja wa waandishi wetu kuwa kilichosababisha akongoroke kiasi hicho ni mazoezi makali anayofanya ili kupunguza unene.
Katika majibu mengine kwa mwandishi wetu mwingine, Ray alidai kuwa anafanya ‘dayati’ ikielezwa kuwa ikishafika saa 11:00 jioni ndiyo mwisho wake wa kula msosi lengo likiwa ni kupunguza mwili uliokuwa umefumuka.
Kama mtu alimuona Ray kwenye Matamasha ya Serengeti Fiesta mwishoni mwa mwaka jana, akikutana naye lazima amtazame mara mbilimbili hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni kutafuta undani wa madai kuwa huenda staa huyo mkubwa anaumwa kufuatia majibu tofauti aliyoyatoa.

WEMA, DIAMOND FEDHA INAONGEA
WAKATI Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akionesha jeuri ya fedha kwa kufungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliogharimu Sh. milioni 260 hivyo kwa pamoja kuthibisha msemo kuwa fedha inaongea, Ijumaa Wikienda lina data kamili.
Wema akiwa ofisini kwake.…
Monday, February 18, 2013
KICHEKESHO kutoka kwa Masanja Mkandamizaji
Jamaa mmoja alizamia semina ya wasomi iliyokuwa inafanyika Ubungo Plaza. Ukafika muda wa watu kujitambulisha. Wa kwanza akaanza: Naitwa John, niko UDOM mwaka wa pili nasoma Sheria. Wa pili: Naitwa Stella, niko UDSM mwaka wa tatu nasoma Public Relations. Jamaa wa tatu mzamiaji akisuasua sana huku akijishtukia: Naitwa Paulo, niko TANESCO mwaka wa tisa nasoma Mita.
LOWASSA RAIS 2015
SASA ni wazi kuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa ndiye atakuwa rais wa awamu ya tano Tanzania mwaka 2015, kutokana na ukweli kwamba kambi zinazosigana ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), zinaonekana kupwaya huku yake ikiwa na watu wenye nguvu kisiasa na kiuchumi, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kusema
Katika vuguvugu la nani awe rais mwaka 2015, uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa tangu uchaguzi ndani ya chama hicho mwaka jana, Lowassa anaonekana kupata mafanikio zaidi kisiasa, ikilinganishwa na mahasimu wake, Benard Membe na Samuel Sitta ambao wanatajwa kutaka kuwania urais baada ya Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake.
Kama ilivyo kwa Lowassa, Sitta ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Membe mwenye kofia ya Uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nao wamekuwa wakidaiwa kuwa na makundi katika harakati za kuusaka urais, japokuwa wenyewe hawajathibitisha.
Uchunguzi huo umeonesha kuwa Lowassa ana mtandao wenye nguvu kisiasa na wachunguzi wa mambo wanasema hata kama vikao vya juu vitamkata jina, kundi lake likiamua nani awe rais uwezekano wa mtu huyo kupita ni mkubwa.
Katika uchaguzi wa chama katika mikoa, wafuasi wengi wa Lowassa walipeta ukilinganisha na makundi mengine yanayotajwa katika kinyang’anyiro cha urais.
Baadhi ya wasomi nchini, walitofautiana kimtazamo kuhusu chaguzi hizo ndani ya CCM. Mhadhiri maarufu wa UDSM, Dk. Benson Bana alisema CCM katika chaguzi hizo imeonesha kwamba hakuna kiongozi yeyote mwenye hati miliki ya chama hicho kwani mtu yeyote anaweza kuingia na kuondoka kwenye chama hicho.
Naye Kisena Mabuba ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alisema: “Tofauti na matarajio ya wengi kuwa CCM ingemeguka, mimi ninachokiona hapa kundi lililobaki na nguvu ni lile la mwenyekiti mwenyewe. Kundi moja limefutwa kabisa na mengine yameshindwa kupata nguvu za kutosha.”
TASWIRA ZA MKUTANO WA CCM KATIKA VIWANJA VYA PILE TEMEKE JIJINI DAR
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.…
JOKATE ATOA BARAKA KWA DIAMOND
BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake, Jokate Mwegelo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na demu wake mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.

Life before Computer kutoka kwa Masanja Mkandamizaji
Life before Computer:
.
.
.
.
.
-Window was a square hole in a room.
-Application was something written in paper.
-Mouse was an animal.
-Keyboard was a Piano.
-File was a important office material.
-Hard Drive was a uncomfortable road trip.
-Cut was done with Knife n Paste was done with Glue.
-Web was spider's home.
-Virus was flu.
-Apple and Blackberry were just fruits
Sunday, February 17, 2013
SAJENTI TAABAN, MATUMAINI BADO HANA MATUMAINI
HUKU mwigizaji Husna Idd ‘Sajenti’ naye akiwa taaban kwa kuzidiwa baada ya kukimbizwa hospitalini na kulazwa, bado hali ya msanii mwenzake, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ haina matumaini akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar.
SAJENTI
Habari zisizokuwa na shaka zilizotua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita zilieleza kuwa Sajenti alizidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake ambapo Ijumaa iliyopita alikimbizwa katika Hospitali ya Kinondoni kwa Dokta Mvungi, Dar akiwa hoi kwa ajili ya vipimo na matibabu.
Ijumaa Wikienda lilifika hospitalini hapo na kumkuta msanii huyo akiwa katundikiwa ‘dripu’ ambapo kwa mujibu wa data za ndani, vipimo vilionesha kuwa alikutwa na malaria na homa ya matumbo hivyo kumfanya aishiwe nguvu.
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Sajenti alikuwa hajaruhusiwa kutoka hospitalini.

Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar.
MATUMAINI
Wakati Sajenti akiombewa na wasanii wenzake arejee katika hali yake ya kawaida, kwa upande wake Matumaini alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kugunduliwa kuwa na tatizo la figo, ini na miguu kuwaka moto.
Naye hali yake bado siyo nzuri tangu aliporejeshwa nchini akitokea Msumbiji akiwa taaban wiki mbili zilizopita.

KAMA HUKUSIKILIZA TOP 20 YA CLOUDS FM FEB 17 2013, LIST IKO HAPA
No. 20 – Butterfly – Q Chief
No. 19 – Nataka Kulewa – Diamond
No. 18 – Mahakama Ya Mapenzi – Linex
No. 18 – Mahakama Ya Mapenzi – Linex
No. 17 – Alingo – P Square
No. 16 – Mtima Wange – Amin – Linnah
No. 15 – Dear Gambe – Young Killa
No. 16 – Mtima Wange – Amin – Linnah
No. 15 – Dear Gambe – Young Killa
No. 14 – Nipende Kama Nilivyo – Mr Blue
No. 13 – Pete – Ben Pol
No. 12 – Wazo La Leo – Stamina
No. 11 – My Everything – Alikiba
No. 10 – 2030 – Roma Mkatoliki
No. 9 – Kidela – Abdukiba – Alikiba
No. 8 – Dear God – Kala Jeremiah
No. 7 – Walaghai – Bonge La Nyau
No. 6 – Me & You – Ommy Dimpoz – Vanessa Mdee
No. 5 – Kesho – Diamond

No. 4 – My – Ali Nipishe
No. 3 – Mama Yoyo – G Nako – Ben Pol
No. 2 – Utamu – Dully Sykes – Diamond – Ommy Dimpoz
No. 1 – Jambo Jambo – Steve Rn’B
No. 3 – Mama Yoyo – G Nako – Ben Pol
No. 2 – Utamu – Dully Sykes – Diamond – Ommy Dimpoz
No. 1 – Jambo Jambo – Steve Rn’B
ALICHOSEMA HALIMA MDEE KUHUSU BUNGE KUONDOLEWA LISIONEKANE LIVE?
Najua kama umekua karibu na media katika siku za karibuni, stori kuhusu uongozi wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza mpango wa kutaka bunge lisiwe linaonekana live kwenye TV utakua umeisikia.
Ni maoni mengi ya Watanzania yametolewa huku asilimia kubwa ikionekana kupinga huo mpango ambao lengo lake ni kukwepa kuonekana kwa wabunge wanaovunja kanuni kwa kuropoka na kufanya vurugu.
Kwenye hii post ni maoni maalum ya mbunge wa Kawe Halima Mdee ambae namkariri akianza kwa kusema “mmhh… kwanza ni hoja ya kipuuzi sana na muhimu ikaeleweka kwamba bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya dola, kinachoonekana kutaka kufanyika ni muhimili mwingine wa dola kutokutaka umma ujue ukweli kwa kutumia watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa bunge kwa sababu yeye ndio ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania wasipate taarifa ambazo tokea bunge limeanza kurushwa live wamekua wakizipata tofauti na ambavyo walikua wanapewa hizo taarifa katika mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye sentensi nyingine Mh Mdee amesema “nasema hivyo kwa sababu kupitia bunge Watanzania wamejua mikataba mibovu ya madini, wamejua EPA, wamejua Richmond, Buzwagi, wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa kwa ajili ya bajeti zimekua zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo zimekua zinajadiliwa live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia katibu wa bunge na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna uhakika na tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya kuficha”
“Kama mlikua mnafatilia bunge la juzi mmeona kwamba wameweka sheria kusema kwamba mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG taarifa yake akiisoma haitajadiliwa hadi mwaka tena mwingine upite waende tena kuedit na kuleta majibu ya uongo, kwa hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo Serikali inaona mambo yakiendelea hivi inawezekana 2015 wakifika watakua wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu ajabu… kwa hiyo waache wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni za bunge kama Mbunge anakiuka kanuni” – Halima Mdee
Subscribe to:
Posts (Atom)