MAANDIKO katika vitabu vitakatifu yanaainisha kuwa mwanamke atamwacha baba na mama yake, ataambatana na mumewe na kuwa mwili mmoja. Vivyo hivyo kwa mwanaume! Hiyo ndiyo ndoa, haijalishi itakuwa imefungwa kidini, kimila au kiserikali (bomani).
Kwenye ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, ndoa kadha wa kadha zimefungwa katika miaka tofauti. Zipo zilizodumu, zinazosuasua na nyingine zimevunjika baada ya wahusika kutofautiana.
Wiki hii Amani linakuchambulia baadhi ya ndoa za mastaa kama ifuatavyo, shuka nayo.
Ndoa ya mwigizaji Aunt Ezekiel aliyofunga na Sunday Demonte mwaka jana, inadaiwa kusuasua kwani tangu bibie aolewe, mumewe alitimkia Dubai huku staa huyo akiahidi kumfuata bila kutimiza ahadi hiyo. Haina tofauti na ile ya staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya aliyeolewa na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwaka 2009 na kudaiwa kuvunjika mwaka jana. Ndikumana alitimka Bongo na kurudi kwao Rwanda akimwacha bibie Bongo akiendelea kula maisha.
Ndoa ya mwanamitindo Jacqueline Patrick aliyofunga na Abdulatif Fundikira mwaka 2011 hivi karibuni ilidaiwa kusuasua. Wakati mume akiwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya mihadarati, mke anadaiwa kujivinjari na wanaume wengine sawa na ya Mbongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’ (2007) ambayo nayo haiko sawa kivile kwani tangu mwaka jana, mke anaishi kivyake Mwanza huku jamaa akitanua Dar.
Kama ni pongezi, zinapaswa kuangushwa kwa mwigizaji Subrina Rupia ‘Cathy’ aliyeolewa na Salim Rupia mwaka 2002, Jacob Steven ‘JB’ aliyeoa mwaka 2004, mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na mumewe Gardner G. Habash ambao walioana mwaka 2005 na wanadumu hadi leo.
Wengine ni Wabongo Fleva Lawrence Marima ‘Marlaw’ na Besta Gasper ambao walioana mwaka 2011 na Joyce Kiria aliyeolewa na Henry Kileo mwaka 2011 ambao hadi leo wanafurahia maisha.
Marlaw na Besta, Banana Zoro na Suzan walioana mwaka 2008, wanatoa ishara nzuri ya kudumu kwenye ndoa kwa wasanii wachanga wa Bongo Fleva kama Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ambaye hivi karibuni alimuoa Halima Ally.
Pia tumsikilizie Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ aliyemuoa Fatma Abdallah mwaka 2011.
Ndoa ya Mtangazaji Hadija Shaibu ‘Dida’ aliyeolewa na Gervas Mbwiga mwaka 2011 ilivunjika mwaka jana tofauti na mwenzake, Sauda Mwilima aliyeolewa na Kauli Juma ‘Best’ mwaka 2012 ambao wanaogelea kwenye mahaba hadi leo.
Baada ya mateso ya ndoa yake ya awali na marehemu William Limbe ‘Ng’wizukulu Jilala’ ambaye alipewa talaka kabla ya mumewe huyo kupatwa na umauti, mwaka 2010, mwigizaji Nuru Nassor ‘Nora’ aliolewa tena na Masoud Ally ‘Luqman’ lakini ndoa hiyo ya pili bahati mbaya ilivunjika mwaka jana.

No comments:
Post a Comment