Sunday, September 22, 2013

MECHI YA SIMBA, MBEYA CITY YAINGIZA MILIONI 123

Simba SC wakimenyana na Mbeya City jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.
Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE REDD'S MISS TANZANIA 2013

Redd's Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi. Kushoto ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na mshindi wa tatu, Clara Bayo (kulia).
Redd's Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akipozi na washiriki wenzake wa shindano hilo.
Happiness Watimanywa akiwa na ufunguo wa gari lake alilojishindia.
Warembo walioingia tano bora.
Gari la Redd's Miss Tanzania 2013.
Happiness Watimanywa akikabidhiwa ufunguo wa gari lake aina ya Toyota IST.
Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' akitumbuiza wakati wa shindano hilo.

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA VYAMA VYA UPINZANI, JANGWANI

Viongozi wa upinzani wakishikana mikono kuonyesha mshikamano wakati wa mkutano wa hadhara wa kutafuta katiba mpya.
  Wananchi wakipunga mikono wakati wa mkutano huo.
  Freeman Mbowe akihutubia wananchi.
 Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia.
Askofu Kakobe akihutubia.
Viongozi wa upinzani kutoka kushoto: Emmanuel Makaidi (NLD), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) wakiwa katika mkutano wa kudai mchakato huru wa katiba mpya.
  Baadhi ya wakazi wa jiji wakifuatilia mkutano huo.
Wananchi wakiwa na mabango wakati wa mkutano huo.
Wananchi wakisikiliza kwa makini hoja za mkutano huo. 
Mwananchi aliyepagawa na hoja za Profesa Lipumba akizuiwa na mabaunsa baada ya kutaka kuvuka uzio.
Mwananchi akionyesha kuguswa na hoja za mkutano.  

RAY C NA ZAMARADI KIMENUKA SASA NI PAKA NA CHUI

So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram. 

page Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo:
aae8fb521c4a11e3842d22000a1f9ada_7
 Picha hiyo aliiandikia maneno haya:

Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini… ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado.. Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii.. sometimes inabidi coz mwisho wa siku mi ni binaadamu tu wa kawaida.”
Wema naye aliongeza kwa kuchangia: Mbona majanga….. dont waste ur tym to fools maamy…. nawe utaonekana a fool… fanya yako… wanaokufatilia wanatamani wawe kama wewe… na si kingine its called ENVY.”
“Sina hata time nae mammy bado ana vichembechembe kwenye ubongo.. maana ghafla tu anaanza kuniparamia jamani.. lol!!! Kishafulia anatafuta kick kwa kugombana na watu.. mtu wa zamani,” aliongeza Zamaradi.
Japokuwa Zamaradi hakutaja wazi nani mlengwa wa ujumbe huo, ni Ray C mwenyewe ndiye aliyejibu kwenye maelezo ndani ya post yake kwenye mtandao huo akisema:
“Hihihi kazi kwelikweli mi naweza posts zangu watu wanajihisi au wanaumia. Tatizo skuliiiii shauri yako #uki skuli kdg wala matatizo hakuna ila km huja skuliii mweeeh unakua mbulula mama we hujui fanya yako achana na watu weusi,” aliandika Ray C.
Aliongeza tena, “Haswa anajiona kichwa kumbe mbulula haswaa Hana lolote,Watu wameanza shughuli hizo anazofanya wenzie tulishazifanya kitambooooooooo,tushauza sura sanaaaaaaaaaa zaid ya miaka. 12 namuangalia simmalizi maana haeleweki.”

Haukuishia hapo, Zamaradi aliongeza tena kwa kuweka post mpya.

886c292a1c5c11e383d722000a1f99fc_7
“Nashusha sana hadhi yangu kwakweli dealing with watu wenye hasira na maisha ya watu wengine… this is not ME kabisa. Una mengi ya kutukaniwa lkn mi ni binaadamu ninaejua baya na zuri.. maisha yashakushinda wewe sasa USIPANIC.. jipange. Ushafanywa yote ya dunia ntakuweza wapi mie mtu wa zamani,” aliandika Zamaradi kwenye picha hiyo.

AL SHABAAB WATHIBITISHA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA KIGAIDI NAIROBI

Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia
-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa
KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shabulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.
Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake.
Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

MASOGANGE AANIKA YA JELA

Stori: Waandishi Wetu
JUZI jijini Dar es Salaam zilisambaa taarifa kuwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amefutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kufuatia taarifa hizo, Risasi Jumamosi lilianza kuwatafuta watu wenye uhakika wa madai hayo ili kuujua ukweli. Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye orodha ya kutafutwa ni pamoja na Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, mchumba wa Masogange aliyepo Bongo, Evans Komu na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa.
ALIVYOSEMA AFANDE NZOWA
Wa kwanza kupatikana alikuwa Kamanda Nzowa ambaye  alisema:
“Ninachojua mimi, Agnes na mwenzake (Melisa Edward) bado wanashikiliwa. Kesi yao ilikuwa Jumatano (Septemba 18, 2013), itatajwa tena Novemba mwaka huu.”
Nzowa akapiga hatua zaidi kwa kusema kwamba aliwahi kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwahoji akina Masogange kabla ya kupandishwa kizimbani Jumatano iliyopita lakini hawakumpa ushirikiano.

BALOZI WA TANZANIA, AFRIKA KUSINI
Baada ya Kamanda Nzowa, Risasi Jumamosi lilimtafuta Balozi wa Tanzania Sauzi, Msuya akasema:
“Mimi sina uhakika, ilimradi umeniambia nitafanya hivyo maana nimekuwa nikifuatilia sana maisha yao wakiwa jela. Lakini pia napenda muwaambie vijana wa Tanzania, wanapokuja huku wawe kamili, waje kwa uhalali, wawe na fedha za kujikimu wakiwa huku mpaka watakaporudi.”
MCHUMBA WA MASOGANGE SASA
Baada ya kuzungumza na balozi huyo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Evans na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri Masogange kuwa huru, akasema:
“Ni kweli mchumba ‘angu Agnes yuko huru. Wasiomjua ndiyo walikuwa wanasema, wameniambia mambo mengi sana kuhusu yeye lakini nilivumilia. Namshukuru Mungu Agnes amerudi tena mikononi mwangu.”
Evans alikwenda mbele zaidi kwa kumuunganisha mwandishi wetu na Agnes kule Sauzi ambapo walizungumza kwa dakika ishirini na mbili.
Risasi: Mambo Eg?
Masogange: Poa, mzima wewe?
Risasi: Mi mzima bwana, pole, nasikia uko huru?
Masogange: Ee, namshukuru sana Mungu.
Risasi: Hivi hebu niambie kwa ufupi, hali ya magereza ya huko ikoje?
Masogange:  Ni balaa, nimekuwa nikiishi maisha magumu sana. Unajua kuishi na watu ambao si taifa lako ni tatizo kubwa, hakuna amani, inachosha akili na kila kitu.
“Ilifika mahali nilitamani ningepata matatizo haya nikiwa nyumbani lakini si ugenini.”
AFUNGA NA KUOMBA
Agnes alienda mbele zaidi kwa kusema amekuwa akifunga na kuomba kila siku kwa muda wote akimlilia Mungu amsaidie kutoka kwenye janga lake.
“Nilifunga sana, pia nilikuwa naomba maombi mazito kabisa. Nimekonda kwa sababu ya kufunga huko.”
USAGAJI
Kuhusu vitendo vya usagaji, staa huyo alisema kuwa askari wa Sauzi wako makini sana na hilo na wanatoa somo kila mara linalokataza tabia ya usagaji na kwamba mtu akibainika anaweza kufunguliwa shitaka jipya.
ALIWAHI KUTILIWA SHAKA
Alisema alishawahi kuitwa na Melisa na kuulizwa kuhusu uhusiano wao, akajieleza kuwa ni mama mkubwa kwa mdogo, ikawa nafuu yao lakini walihisiwa vibaya kutokana na ukaribu wao.
ADAI ALIWAHI KUTONGOZWA NA ASKARI
Risasi: Tuliwahi kusikia kwamba kuna askari wanakutongoza kutokana na wowowo lako. Je, madai haya ni ya kweli?
Agnes: (kicheko), watu wanachonga sana. Unajua mimi nina mchumba wangu jamani.
Risasi: Lakini kuna ukweli wa madai hayo?
Agnes: (akakata simu).
Swali hapa linaweza kuwa hivi, kama hajaachiwa huru kwa nini aliongea na simu akiwa gerezani? Jibu lipo. Masogange amekuwa akipatikana hewani mara kadhaa licha ya kuwa gerezani.
WATU WAMSOMA KWENYE INSTAGRAM
Kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambao hakuwa hewani tangu Julai mwaka huu, usiku wa Septemba 17, 2013 aliandika hivi:
“Thanks God nimeamini wewe ulikuwa pamoja na mimi katika maombi yangu na thanks kwa wote mliokuwa mkiniombea, Mungu kapokea maombi yenu.”
Halafu akaendelea: All praise and glory to the Lord almighty I thank you for my freedom, amen (Sifa zote ni kwa Bwana, nakushukuru kwa uhuru wangu, amen).
LINAVYOSEMA RISASI JUMAMOSI
Risasi Jumamosi linaweka wazi kwamba, Agnes awe ameachiwa au hajaachiwa, lakini watu wote waliotafutwa ili wazungumze walipatikana na walisema kama ambavyo imeandikwa.
VIPI KUHUSU REHEMA FABIAN?
Wakati tunakwenda mitamboni kuna habari zilisambaa kwamba, Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kukamatwa nchini China.
Madai yamesema mengi, lakini hakuna mwenye kusema wazi kisa nini ingawa wengine walidokeza habari za unga.
MASOGANGE...
Stori: Waandishi Wetu

JUZI jijini Dar es Salaam zilisambaa taarifa kuwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amefutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kufuatia taarifa hizo, Risasi Jumamosi lilianza kuwatafuta watu wenye uhakika wa madai hayo ili kuujua ukweli. Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye orodha ya kutafutwa ni pamoja na Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, mchumba wa Masogange aliyepo Bongo, Evans Komu na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa.

ALIVYOSEMA AFANDE
NZOWA
Wa kwanza kupatikana alikuwa Kamanda Nzowa ambaye  alisema:
“Ninachojua mimi, Agnes na mwenzake (Melisa Edward) bado wanashikiliwa. Kesi yao ilikuwa Jumatano (Septemba 18, 2013), itatajwa tena Novemba mwaka huu.”
Nzowa akapiga hatua zaidi kwa kusema kwamba aliwahi kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwahoji akina Masogange kabla ya kupandishwa kizimbani Jumatano iliyopita lakini hawakumpa ushirikiano.

BALOZI WA TANZANIA,
AFRIKA KUSINI
Baada ya Kamanda Nzowa, Risasi Jumamosi lilimtafuta Balozi wa Tanzania Sauzi, Msuya akasema:
“Mimi sina uhakika, ilimradi umeniambia nitafanya hivyo maana nimekuwa nikifuatilia sana maisha yao wakiwa jela. Lakini pia napenda muwaambie vijana wa Tanzania, wanapokuja huku wawe kamili, waje kwa uhalali, wawe na fedha za kujikimu wakiwa huku mpaka watakaporudi.”

MCHUMBA WA
MASOGANGE SASA
Baada ya kuzungumza na balozi huyo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Evans na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri Masogange kuwa huru, akasema:
“Ni kweli mchumba ‘angu Agnes yuko huru. Wasiomjua ndiyo walikuwa wanasema, wameniambia mambo mengi sana kuhusu yeye lakini nilivumilia. Namshukuru Mungu Agnes amerudi tena mikononi mwangu.”
Evans alikwenda mbele zaidi kwa kumuunganisha mwandishi wetu na Agnes kule Sauzi ambapo walizungumza kwa dakika ishirini na mbili.
Risasi: Mambo Eg?
Masogange: Poa, mzima wewe?
Risasi: Mi mzima bwana, pole, nasikia uko huru?
Masogange: Ee, namshukuru sana Mungu.
Risasi: Hivi hebu niambie kwa ufupi, hali ya magereza ya huko ikoje?
Masogange:  Ni balaa, nimekuwa nikiishi maisha magumu sana. Unajua kuishi na watu ambao si taifa lako ni tatizo kubwa, hakuna amani, inachosha akili na kila kitu.
“Ilifika mahali nilitamani ningepata matatizo haya nikiwa nyumbani lakini si ugenini.”

AFUNGA NA KUOMBA
Agnes alienda mbele zaidi kwa kusema amekuwa akifunga na kuomba kila siku kwa muda wote akimlilia Mungu amsaidie kutoka kwenye janga lake.
“Nilifunga sana, pia nilikuwa naomba maombi mazito kabisa. Nimekonda kwa sababu ya kufunga huko.”

USAGAJI
Kuhusu vitendo vya usagaji, staa huyo alisema kuwa askari wa Sauzi wako makini sana na hilo na wanatoa somo kila mara linalokataza tabia ya usagaji na kwamba mtu akibainika anaweza kufunguliwa shitaka jipya.

ALIWAHI KUTILIWA SHAKA
Alisema alishawahi kuitwa na Melisa na kuulizwa kuhusu uhusiano wao, akajieleza kuwa ni mama mkubwa kwa mdogo, ikawa nafuu yao lakini walihisiwa vibaya kutokana na ukaribu wao.

ADAI ALIWAHI
KUTONGOZWA NA ASKARI
Risasi: Tuliwahi kusikia kwamba kuna askari wanakutongoza kutokana na wowowo lako. Je, madai haya ni ya kweli?
Agnes: (kicheko), watu wanachonga sana. Unajua mimi nina mchumba wangu jamani.
Risasi: Lakini kuna ukweli wa madai hayo?
Agnes: (akakata simu).
Swali hapa linaweza kuwa hivi, kama hajaachiwa huru kwa nini aliongea na simu akiwa gerezani? Jibu lipo. Masogange amekuwa akipatikana hewani mara kadhaa licha ya kuwa gerezani.

WATU WAMSOMA KWENYE INSTAGRAM
Kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambao hakuwa hewani tangu Julai mwaka huu, usiku wa Septemba 17, 2013 aliandika hivi:
“Thanks God nimeamini wewe ulikuwa pamoja na mimi katika maombi yangu na thanks kwa wote mliokuwa mkiniombea, Mungu kapokea maombi yenu.”
Halafu akaendelea: All praise and glory to the Lord almighty I thank you for my freedom, amen (Sifa zote ni kwa Bwana, nakushukuru kwa uhuru wangu, amen).

LINAVYOSEMA RISASI
JUMAMOSI
Risasi Jumamosi linaweka wazi kwamba, Agnes awe ameachiwa au hajaachiwa, lakini watu wote waliotafutwa ili wazungumze walipatikana na walisema kama ambavyo imeandikwa.

VIPI KUHUSU REHEMA
FABIAN?
Wakati tunakwenda mitamboni kuna habari zilisambaa kwamba, Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kukamatwa nchini China.
Madai yamesema mengi, lakini hakuna mwenye kusema wazi kisa nini ingawa wengine walidokeza habari za unga.

KIOJA KORTINI

Stori: Richard Bukos
KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni, Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka lake la uzururaji.Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alikuwa akimsomea shtaka hilo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, William Mutaki na alipotakiwa kukiri au kukanusha kosa lake, mtuhumiwa huyo alibaki kimya akiwa amemtumbulia macho hakimu.Katika hali isiyotarajiwa, mtuhumiwa huyo alionekana akijikamua kama anayejisaidia na ghafla, harufu kali ya kinyesi ikatanda mahakamani hapo.Hakimu alitahayari kufuatia tukio hilo, kwani aliziba pua yake kwa kutumia koti lake na kuuliza chanzo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho kortini, lakini katika hali iliyoashiria kama ni kiburi, kijana huyo hakujibu chochote zaidi ya kutazama chini, licha ya swali hilo kurudiwa zaidi ya mara tatu.Kutokana na kosa hilo ambalo liliharibu na kusimamisha karibu shughuli zote za mahakama kwa muda, Hakimu Mutaki alimhukumu kijana huyo kwenda jela kwa muda wa miezi sita ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Kana kwamba haitoshi, askari waliokuwepo mahakamani hapo walilazimika kumchapa bakora kijana huyo ili kumlazimisha kupiga deki baada ya eneo hilo kuchafuka vibaya kwa kinyesi kilichochanganyika na mkojo.

Friday, September 13, 2013

Huu ndio mjengo wa Madee uliopo Mbezi jijini Dar

Raisi wa Manzese, Madee anatarajia kuhamia Mbezi sasa, na huko sijui kama atakuwa Raisi au niaje niaje. Nasema hivyo kwasababu Madee ameonyesha picha ya mjengo wake uliokamilika kwa asilimia kubwa uliopo maeneo ya Mbezi jijini Dar.

kukamilika kwa mjengo huo kumetokana na mafanikio makubwa aliyoyopata baada ya kukubalika kwa single yake "Pombe Yangu"
hiki ndicho alichokiandika madee 
"siri ya utajiri ni ubahiriii#hahaha welkam white houze@mbezi dsm#"

H Baba na Flora Mvungi wapata mtoto wa kike wampa jina la Tanzanite

Msanii H Baba na mkewe Flora Mvungi wamefanikiwa kupata mtoto wa kike jana jioni majira ya saa 12:30 katika hospitali ya Maria Stope iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kama unakumbuka hapo awali H Baba alisema kama akifanikiwa kupata mtoto wa kike au kiume basi atampa jina 'Tanzanite' hatimaye amefanikiwa kupata wa kike na kumpatia jina la Tanzanite.

Hii ndio cake ya birthday ya Ommy Dimpoz na ujumbe aliouandika kwa familia marafiki na mashabiki wake

Tarehe 13 / 09 ni siku ya kuzaliwa hitmaker Omari Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, na huu ndio ujumbe wake kwa familia,marafiki na fans wake.

I would like to thank God for the blessings he has showered me with over the years and especially during my professional musical career!! Saying Allah is great it truly an understatement. Next to him is#TeamPozKwaPoz. Mad love to my fans cause truly without you I am Nothing. Fans, family & friends, you are the pillar of my success and you are irreplaceable... Happy Birthday to ME!! And I'm thankful for everything good or bad as they all have shaped me to be the man I am today. Come celebrate life health and music with me tonight at Elements Lounge. My brothers j martins, AY and FA will be there as well making sure it's more than a birthday!! Tupogo, ama nini?!!

Happy Birthday ommy Dimpoz

Unaambiwa huyu ni mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani

4yearold_mayorb.jpgWRobert ‘Bobby’ Tufts hajaanza hata shule ya  Nursery ambayo huku Tanzania tunaifahamu kama chekechea au vidudu lakini tayari ameshajiwekea historia ya kuwa mwanasiasa mwenye umri mdogo kuliko wote duniani .
Dogo huyo ameweza kuwa meya wa mji mmoja huko Minesotta akiwa na umri wa miaka mitatu pekee, unaambiwa ni Meya wa mji mdogo wa Dorset ulioko huko Minesotta Marekani na hii ni mara yake ya pili kuchaguliwa kuwa meya wa mji huo baada ya kupigiwa kura siku ya jumapili ambapo aliweza kushinda kipindi chake cha pili cha uongozi .
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert 'Bobby' Tufts.
Mstahiki Meya wa Mji wa Dorset Robert ‘Bobby’ Tufts.
Mji huo una serikali ndogo inayoongozwa na meya huyo mdogo ambaye anaongoza idadi ya watu 220 ambao ni wakazi wa mji huo ambapo kama ilivyo kwenye manispaa yoyote, meya Bobby anaongoza serikali ambapo hufanya maamuzi yanayohusu bajeti ya matumizi ya mji wa Dorsett pamoja na masuala mengine nyeti kama ya kodi na makusanyo mengine ya mapato.
Mama mzazi wa Meya Robert Tufts, Emma Tufts anasema kuwa moja ya agenda za uongozi wa mwanaye ni kukusanya fedha kwa ajili ya taasisi ya misaada ya Ronald McDonald iliyoko Dorset eneo la Red River Valley Fargo Dakota ya Kaskazini pamoja na ujenzi wa kibao kipya cha kuwakaribisha wageni huko Dorset kwenye barabara zinazopakana na miji mingine.
4yearold_mayorc.jpgWTaarifa za Meya huyo mdogo kuliko wote duniani zimefika mpaka ikulu kwa Barack Obama ambae amempa Robert Tufts mwaliko maalum kwenye ikulu yake na ana mpango wa kumfanya kuwa mshauri wake maalum kwenye mfuko wake unaofahamika kama ObamaCare Foundation.