Wednesday, January 1, 2014

DINA MARIOS, RUBEN NDEGE, SIYO SIRI TENA

Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’.
Na Mwandishi Wetu
SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.
Kwa muda mrefu Dina na Ruben wamekuwa kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakijitahidi kuuficha usijulikane na watu, lakini hata hivyo watu wa karibu hasa wanaofanya nao kazi, walifahamu juu ya uhusiano huo.
Akizungumza katika Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Radio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita kwa mara ya kwanza Dina alifunguka kuhusu kuwa na uhusiano na Ruben huku akiweka wazi kuwa ana mimba yake.
“Ni kweli baba mtarajiwa wa mtoto wangu ni Ruben Ndege ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Skylight Band. Wengi hapa kazini mnajua kuwa tulianza naye mbali. Kulikuwa na kupanda na kushuka, mara kwa mara lakini nashukuru sasa uhusiano wetu umeimarika,” alisema Dina.
Alisema, katika muda aliokuwa katika uhusiano na Ruben, kuna wakati walikuwa wakiachana na kurudiana lakini anamshukuru Mungu kwa kuwasimamia na kuwafikisha katika hatua hiyo.
Siku hiyo Dina alikuwa akiaga wasikizaji wake, kwa vile atakuwa na likizo ya uzazi ya miezi minne wakati huu akisubiri kujifungua na kumlea kichanga chake.

ANGALIA ALAMA HIZI, ANZA MWAKA NA FIKRA MPYA!

KUNA wakati unafikiria kufanya kitu fulani muhimu kwa ajili ya yule uliyemteua kuwa mwenzi wa maisha yako? Je, huwa unafikiria kama upo katika uhusiano sahihi au unakwenda tu mradi siku zinakwenda?
Wapo watu ambao wako tu kwenye uhusiano kabla ya uchumba lakini matukio kibao yametokea.
Wameshafumaniana, wameshapigana, wameshatoleana maneno machafu, wameshadhalilishana nk. Je, ni sahihi kuendelea katika uhusiano huo? Jibu ni jepesi kabisa, si sahihi.
Ndugu zangu ni vizuri kutafakari. Utakuta mtu yupo kwenye urafiki kwa miaka mitano na mpenzi wake, hajatambulishwa wala hakuna dalili za kufanyika jambo hilo. Siyo sawa. Acha kupoteza muda wako.
Uchumba wa miaka mitano (ikiwa hakuna vikwazo muhimu) si sahihi. Ni muda ambao wenzako tayari wameshakuwa na watoto wawili! Jaribu kutafakari. Usikubali kupoteza muda wako kwa jambo ambalo halina uelekeo.
Wakati unaanza mwaka huu mpya ndugu yangu, pata muda wa kutafakari kuhusu uhusiano wako. Je, kuna matarajio? Je, mwanandoa wenzako analandana sawa na wewe au kuna dalili za kusalitiwa? Kaa utafakari na uchukue hatua.
Anza mwaka huu ukiwa na matumaini mapya, mawazo mapya na fikra mpya kuhusu maisha yako yajayo. Acha kuhesabu namba za siku, wiki, miezi na miaka kila siku ukibaki palepale.
Hapa kwenye All About Love, tutaangalia mambo muhimu ya msingi na kutazama kwa undani uhusiano ulivyo ili uweze kujua upo kwenye kundi gani na kuchukua hatua haraka.
Achana na mazoea, usikubali maumivu katika moyo. Usikubali kuingia mwaka huu ukiwa bado unaburuzwa tu. Tathmini, alikufanyia nini katika kipindi chote cha uhusiano wenu?
Tazama hata katika mwaka huu pekee, amefanya kipi cha kukufanya umuone bado yu bora katika maisha yako? Inawezekana juzi tu kwenye Sikukuu ya Krismasi alikutesa na kukunyanyasa moyo wako, angalia kwa makini.
Lazima awe na umuhimu kwako, awe ameonesha kweli anakupenda na anaweza kuwa nawe katika maisha yako ndipo ukubali kwa moyo wako kuendelea naye katika mwaka huu. Hebu twende tukaone zaidi katika vipengele nilivyowaandalia.
KWENU WANAWAKE
Dada zangu, mnapoangalia mtu muhimu wa kuwa naye katika maisha ni muhimu sana kuangalia tabia zake, fanya tathimini ya jumla, kutafuta kujua kama ni kweli ana sifa za kuwa na wewe.
Kumfanya awe wako, maana yake umempa nafasi kubwa katika moyo wako. Sasa hakuna sababu ya kumpa moyo wako mtu ambaye penzi lake lina mashaka. Hapa nimekuandalia sifa za mwenzi ambaye hafai kuwa wako.
Soma kwa makini, ikiwa katika mapito ya penzi lenu ana nusu ya sifa nitakazotaja hapa, ni bora utulie, ikiwezekana utafakari upya kuanza mwaka mpya ukiwa katika mtazamo wa tofauti.
Hatimizi ahadi...
Mwanaume ambaye ana nia ya kukutumia na kukuacha, unaweza kupima hata maneno yake, mara zote amekuwa mtu wa maneno mengi ambayo hayatekelezeki! Ahadi zake zimekuwa nyingi ambazo baadaye unagundua kwamba ni hewa.
Huyu hana mapenzi ya kweli na nia yake ni kukuchezea na kukuacha na ndiyo maana anaweza kuropoka hata mambo ambayo anajua wazi kwamba hana uwezo wa kuyatekeleza. Mchunguze zaidi mwanaume wa aina hii, kwani ni moja kati ya dalili za mwanaume ambaye hana sifa ya kuwa na wewe.
Hana mipango...
Hataki kabisa kuzungumzia juu ya mustabali wa maisha yenu ya baadaye. Hataki mijadala ya mambo ya ndoa, ukianzisha anakukatisha. Hata mijadala hiyo inapotokea kwenye runinga au redio mkiwa naye, atabadilisha channel ili asisikilize au kuona.
Huyu bado yupoyupo, anapendezwa na uzuri na mwonekano wako ambao kwake ni pambo la muda tu, na siyo la kudumu kama ambavyo wewe unawaza. Hana mpango na wewe.
Uhusiano wa siri...
Hataki uhusiano wenu ujulikane na ndugu zake/zako wa karibu. Hata inapotokea akalazimika kufanya hivyo, hutoa visingizio vingi. Anaogopa kukutambulisha kwa sababu anafahamu wazi kwamba hana nia ya kuishi na wewe hapo baadaye badala yake anakutumia tu!
Huyu hafai kabisa kuwa mwenzi wako na unatakiwa kumfuta katika akili yako.
Bado kuna mengi ya msingi zaidi ya kujifunza, wiki ijayo tuendelea na vipengele vingine, USIKOSE!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vitatu; True Love, All About Love na Let’s Talk About Love vilivyopo mitaani.

JACK PATRICK MATESO SAA 48

JACK PATRICK MATESO SAA 48



Jack Patrick baada ya kukamatwa na dawa za kulevya.
Stori:  Jelard Lucas
HABARI ya kufungia mwaka 2013 na kufungua pazia la mwaka mpya wa 2014 ni madai ya mwanamitindo kiwango Bongo, Jacqueline Patrick kukamatwa katika  Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya aina ya heroin lakini Risasi Mchanganyiko linaangaza mapya zaidi juu ya sakata hilo.
Mwanamitindo Jacqueline Patrick.
Macho na masikio ya Wabongo wengi kwa sasa ni juu ya mwenendo wa madai hayo, wakati gazeti hili likiendelea kupekenyua limenasa mpya kuwa, Jack yupo kwenye mateso makali kutoka kwa askari wapelelezi nchini humo wanaotaka kujua mtandao unaomuunganisha katika mchezo huo.
SAUTI KUTOKA CHINA
Chanzo chetu makini kilichopo China ambacho kinapiga kitabu kilieleza kuwa, katika kufuatilia ishu hiyo, juzi Jumatatu, Desemba 30, 2013, alikutana na kizingiti cha kushindwa kuonana na Jack katika mahabusu aliyowekwa kwa maelezo kwamba, uchunguzi bado unaendelea.
Dawa za kulevya zilizokutwa tumboni mwa Jack.
Raia huyo wa Tanzania aliyedai ana ukaribu na Jack, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, alisema mengi kuhusiana na mateso anayopata mrembo huyo hivi sasa.
“Ni kweli Jack amekamatwa hapa Macau. Hilo halina ubishi kabisa. Sheria za huku zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo. Nilifika mahabusu aliko kwa lengo la kutaka kumwona lakini nilikataliwa. Nimeambiwa hawezi kuonana na mtu yeyote hadi Machi, mwakani (mwaka huu). Bado wanaendelea na uchunguzi kwanza.
Jack akiwa na mwenzake.
“Unajua wanajaribu kufichaficha mambo ili polisi waweze kufanya upelelezi wao vizuri lakini nimepenyezewa taarifa kuwa ataingizwa chumba cha mateso ili abanwe na kutaja mtandao wake. Wanajua yeye wameshamkamata, lakini wanataka kufahamu mzigo alitumwa na nani, ameutoa nchi gani na unakwenda nchi gani?
“Lengo la kufanya hivyo ni kukomesha mtandao mzima wa madawa ya kulevya. Si ajabu akawa kwenye mateso kwa kipindi chote hicho kama hatakuwa mkweli lakini kwa sasa ataingizwa kwenye kikosi cha kwanza.
Jack akiwa chini ya ulinzi.
“Hapo atakalishwa kwenye chumba cha mateso kwa siku mbili mfululizo (akimaanisha saa 48). Ni mateso makali sana. Wataalam wanajua wanafanyaje ili mtuhumiwa aweze kuzungumza ukweli kwa muda mfupi. Sasa hapo ikishindikana ndipo anaweza kuhamishiwa kwenye kikosi kingine,” alipasha mtoa habari wetu na kuongeza:
“Ni kama huko Bongo tu. Unaposikia chumba cha mateso ya wapelelezi maana yake shughuli yake siyo ndogo. Mimi namuonea huruma sana Jack, lakini najiuliza, hivi ni kwa nini huwa hawajifunzi kupitia wenzao?
“Si juzi tu wengine (Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward) wamekamatwa kwa madawa hayohayo na walisota kwa muda mrefu? Kwa nini hawasikii jamani? Namuhurumia sana kwakweli.”

KUMBE DADA YAKE ALIMUONYA
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na dada wa Jack zinasema kuwa, wakati akitaka kusafiri akitokea Bongo, alimweleza dada yake juu ya mpango wake huo, akamuonya lakini modo huyo alikataa.
“Alimfuata dada yake na kumweleza mchongo mzima kuwa alitaka kwenda na mzigo China, dada yake akamwambia aachane na hizo biashara, akakataa. Jack alifikia hatua akamwambia dada yake kuwa hana mtoto, hana mume wala ndugu anayemtegea kwa hiyo yupo tayari kwa lolote kwani hakuwa na cha kupoteza.
“Kama angemsikiliza dada yake (jina linahifadhiwa) haya yote yasingemkuta na asingeingia kwenye mateso ya namna hii,” alisema mtoa habari wetu huku akiendelea kusisitiza jina lake lisionekane mahali popote kwenye ukurasa huu.
ABEBESHWA MZIGO, ALIPWA MALIPO YA AWALI
Ilizidi kusemekana kuwa, alipokaribia kuondoka Bongo, Jack alimwambia dada yake kwamba anakwenda kambini (kituo cha kuingiza mzigo tumboni) ambapo aliporejea kwa dada’ake alimuonesha dola za Kimarekani 21,000 (zaidi ya shilingi milioni 33) ambazo ni malipo ya awali huku akimwambia alishabebeshwa nusu ya mzigo.
Hata hivyo, habari zinasema Jack alimwambia dada yake huyo kuwa hakuwa akijisikia kusafiri lakini kwa kuwa anatafuta maisha aliamua kuondoka baada ya mzigo kukamilika wote siku iliyofuata.
INA MAANISHA NINI?
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Jack aliondoka na unga hapahapa Bongo kwenda Thailand kupitia Nairobi, Kenya na baadaye Macau, China ambako alinaswa.
MASTAA WAFUNGUKA
Watu wamekuwa na mitazamo tofauti kulingana na ishu hiyo lakini Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameeleza maoni yao kuhusiana na sakata hilo la Jack.
Katika mahojiano na waandishi wetu, tulitaka kusikia kutoka kwao namna wanavyolinganisha tabia ya kujihusisha na biashara za kusafirisha madawa ya kulevya na vitendo vya umalaya ambapo wametoa maoni tofauti.

JACQUELINE WOLPER:
“Mh! Mwenzangu, bora uwe na mabuzi (wanaume wenye mkwanja) 40 kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba mastaa wenzangu wasikubali kubebeshwa madawa kwa kudanganywa eti na dola 30,000, kamwe haiwezi kubadili mfumo wa maisha yako.”

REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’:
 “Madawa ya kulevya hayakubaliki, yalinitenda sana haya madude! Kabisa tulinde vizazi vijavyo kwa kupiga vita madawa ya kulevya. Fanya yote lakini siyo madawa ya kulevya.”

SHAMSA FORD:
 “Nasema hivi, bora umalaya japo pia si mzuri kuliko kudili na biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba waachane na vitu hivyo kwani vinatumaliza kisanii... lakini nasisitiza kutulia na bwana mmoja ni vizuri sana kuliko kurukaruka.”

JOKATE MWEGELO:
 “Hakuna aliye mkamilifu lakini kama kitu ni kiovu ni kiovu tu hata kama mimi na wewe tunakifanya, kimsingi hakuna bora na anayesema kuna ubora basi hajitambui. Vyote vinadhalilisha utu na thamani ya mwanamke. Mwili si wa kuchezewa.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’:
“Tukitumia majina yetu vizuri, hakuna atakayejihusisha na yote hayo... tujitume kufanya kazi, umalaya unaweza kuwa bora kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya kama utabanwa kuchagua maovu hayo. Maisha ya Ughaibuni yatatumaliza kwani tunaiga kwa kukurupuka bila kuelewa.”

TUMETOKEA HAPA
Jack anatuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya Desemba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea jijini Bangkok, Thailand akiwa safarini kwenda Guangzhou nchini China.
Ilielezwa kuwa unga aliokutwa nao una uzito wa kilo 1.1  ndani ya kete 57 huku thamani yake ikitajwa kuwa ni  zaidi ya shilingi milioni 223.
Bado yupo mikononi mwa polisi wa China wakati upelelezi wa awali ukiendelea ambao utafikia tamati Machi, mwaka huu kabla ya kuingia hatua inayofuata.

SNURA 'MAMAA MAJANGA' NA KUNDI LAKE WAKIFANYA MAKAMUZI DAR LIVE

SNURA 'MAMAA MAJANGA' NA KUNDI LAKE WAKIFANYA MAKAMUZI DAR LIVE

Snura Mushi na kundi lake wakifanya makamuzi katika usiku wa mwaka mpya 2014 ndani ya Dar Live.
Snura akisema na mashabiki wake.
Wanenguaji wa Snura wakiwa kazini.
Snura na kundi lake wakizidi kupagawisha mashabiki wa Dar Live.

BAADA YA KUKIMBIWA NA MPINZANI WAKE KALAPINA ATANGAZA KUZICHAPA NA KASEBA

BAADA YA KUKIMBIWA NA MPINZANI WAKE KALAPINA ATANGAZA KUZICHAPA NA KASEBA


Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Kalapina akitangazwa kushinda kwenye mpambano wa ngumi usiku wa kuamkia leo,baada ya mpinzani wake Bahati Mwamfiale kutotokea ulingoni ndani ya Ukumbi wa Msasani Club,sasa aomba pambano na Japhet Kaseba na Mchumia Tumbo.
Kalapina akirudi kwenye chumba cha kubadilishia nguo huku akishangiliwa na wapambe wake.
Francis Miyeyusho (kulia), akipambana na Bondia kutoka nchini Kenya Joshua Omukulu, ambaye alimpiga kwenye mzunguko wa pili kwa KO na kudondoka chini.
Bondia Joshua Omukulu akiwa chini baada ya kupelekewa konde la ujazo na mpinzani wake
Kalama Nyilawila (kulia), akipambana na Ibrahim Maokola, ambapo Kalama aliibuka mshindi kwa KO Ndani ya Ukumbi wa Msasani Klabu.

HABARI 10 ZA GPL ZILIZOTIKISA MWAKA 2013

HABARI 10 ZA GPL ZILIZOTIKISA MWAKA 2013

1. MSIBANI KWA BABA WEMA... LULU ATOA MITUSI MIZITO
Stori: Waandishi Wetu
MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao...
2. ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA HUYU HAPA

Stori: Waandishi Wetu
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya. Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya sheria vitazungumza lakini gazeti hili limejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa denti husika ni tapeli na anacheza rafu ili kumharibia Kapuya kwa maslahi yake...
ZAIDI, INGIA HAPA: ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA HUYU HAPA
3.  EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA
Na Sifael Paul
MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili...
ZAIDI, INGIA HAPA: EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA

4. MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY


Stori:  Jelard Lucas
HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo...
ZAIDI, INGIA HAPA: MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY
5. UKWELI KUHUSU ASALI NA MDALASINI KAMA TIBA
WASIOJUA kuhusu uwezo wa asali na mdalasini wanaweza wasiamini wakiambiwa kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu magonjwa hatari yaliyoshindakana hata hospitalini. Asali na mdalasini zimekuwa zikitumika kama tiba tangu enzi na enzi...
ZAIDI, INGIA HAPA: UKWELI KUHUSU ASALI NA MDALASINI KAMA TIBA
6. RAY YAMEMKUTA  
Stori:Haruni Sanchawa
TUKISEMA staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta ni sawa, kisa ni ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele, Risasi Jumamosi lina mkanda wote. Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam...
ZAIDI, INGIA HAPA: RAY YAMEMKUTA
  7. RAY AKONGOROKA 
Stori: Musa Mateja na Imelda Mtema
MWIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ amezua hofu kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake baada ya kukongoroka ghafla akihisiwa anaumwa, Ijumaa Wikienda limemfuatilia hatua kwa hatua...
ZAIDI, INGIA HAPA: RAY AKONGOROKA
8. DENTI ALIYEDAI KUZAA NA DIAMOND... AUMBUKA, ATISHIA KUJIUA
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’. Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond, ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana. Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua...
ZAIDI, INGIA HAPA: DENTI ALIYEDAI KUZAA NA DIAMOND... AUMBUKA, ATISHIA KUJIUA
9. BONGO MUVI WAMSUSIA WEMA MSIBA
Na waandishi wetu
HUKU akiwa na majonzi ya kuondo-kewa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki dunia Jumapili iliyopita kwa ugonjwa wa kisukari, baadhi ya wasanii wanaounda Klabu ya Bongo Movie (muvi) Unity wanadaiwa kumsusia msiba mwingizaji mwenzao, Wema Isaac Sepetu...
ZAIDI, INGIA HAPA: BONGO MUVI WAMSUSIA WEMA MSIBA
10.  ANASWA
Stori: Richard Bukos, Issa Mnally na Imelda Mtema.
MfanyabiAshara ‘alwatani’ Bongo, mkazi wa jijini Dar, Allain Tajiri amekumbwa na skendo nzito baada ya kufumaniwa na mwanafunzi wa sekondari wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu katika chumba namba 107 kwenye gesti iitwayo Jamboz iliyopo Kinondoni jijini Dar...

Saturday, December 21, 2013

DIAMOND,PENNY WAMWAGANA!

Stori: shakoor jongo na mayasa mariwata.
NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana, Risasi Jumamosi limemwagiwa upupu.
Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ wakiwa pamoja katika pozi.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.
                                Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.

RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori!

 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”
                                                                Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”
                                               Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita ‘weee’ mpaka inakatika, inaita ‘weee’ mpaka inakatika.

RAIS KIKWETE AWAVUA VYEO MAWAZIRI WANNE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
RAIS Jakaya Kikwete amekubali kuwavua vyeo vyao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki aliyekuwa tayari ametangaza bungeni kujiuzulu. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni baada ya kueleza kuwa ameongea na Rais na kukubali kuwavua nyadhifa zao kutokana na ripoti ya Operesheni Tokomeza iliyosomwa leo bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.