Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.
Friday, March 14, 2014
Unaamini huyu mshkaji kafanana na Marehemu Ngwea kwa asilimia 100?
Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.
Picha za Ommy Dimpoz akiwa chini ya ulinzi wa polisi Uingereza.. making the video
Rihanna na Drake tena, hizi ni za jana usiku Manchester.
Ingawa wawili hao waliopachikwa jina la ‘AubRih’ (Kwa maana ya Aubrey na Rihanna) mpaka sasa wamekuwa wakisisitiza bado ni marafiki wa kawaida, headlines zao za hivi karibuni zinaonyesha kuna kitu zaidi ya urafiki kati yao.
Rihanna amekuwa akionekana na Drake wakiongozana kwenye ziara ya kimuziki ya Drake Ulaya ambapo kwa mara ya kwanza walionekana pamoja nchini Ufaransa, kisha Ujerumani na jana usiku walionekana pamoja jijini Manchester – England.
Na hizi ni picha za ushahidi wa wawili hao walivyokuwa wakijiachia kwenye mitaa ya jiji la Manchester usiku jana.
Weekend hii unaweza kuitumia kwa kuangalia hizi movie kwenye theater tofauti.
Movie hii ambayo itaonyeshwa kwenye 3D imetoka kwa director wa 300 na Man of Steel. Pamoja na hiyo kuna movie nyingine zitakazoonyeshwa kwenye muda tofauti.
Cheki hizi ratiba na uchagua movie yako ya kwenda kuangalia kuanzia kesho 14/3/2014
Taarifa za Mtumbwi uliozama Mtwara March 13 ukiwa na kina mama wauza samaki..
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama 3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na wahusika wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo.
Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo March 14 2014
Subscribe to:
Comments (Atom)