Arsenal wakishangilia ushindi wao wa leo dhidi ya Stock City.
Aaron Ramsey akishangilia bao la kwanza aliloifungia Arsenal.
Charlie Adam (kushoto) akishangilia na mwanzake Geoff Cameron aliyeifungia Stock bao la kusawazisha.
Per Mertesacker akiifungia Arsenal bao la pili kwa kichwa.
Bacary Sangna akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la tatu kwa Arsenal.
Arsenal FC leo imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya
kuilaza Stock City mabao 3-1. Kwa ushindi huo, Arsenal wamefikisha
pointi 12 baada ya kucheza mechi tano. Katika mechi ya leo iliyopigwa
Uwanja wa Emirates jijini London, Arsenal wamejipatia mabao yao kupitia
kwa Aaron Ramsey, Per Mertesacker na Bacary Sangna. Stock City wamepata
bao lao kupitia kwa Geoff Cameron.
No comments:
Post a Comment