Sunday, September 22, 2013

AGUERO, TOURE, NASRI WAPELEKA KILIO MAN UTD

Mfungaji wa mabao mawili mechi ya leo, Sergio Aguero akishangilia moja ya mabao yake.
Yaya Toure baada ya kuifungia Man City bao la pili katika dakika ya 45.
Majanga: Wachezaji wa Manchester United wakiwa hawaamini kilichotokea.
Samir Nasri baada ya kuhitimisha kwa bao la nne.
Wachezaji wa Manchester City Sergio Aguero, Yaya Toure na Samir Nasri leo wamepeleka majonzi kwa Manchester United.  Wachezaji hao wameifungia Manchester City wakati ikiibuka kidedea kwa mabo 4-1 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa Uwanja wa  Etihad, jijini Manchester.
Sergio Aguero ameifungia Man City dakika ya 16 na 47, Yaya Toure akifunga dakika ya 45 kabla ya Samir Nasri kuhitimisha kwa bao la dakika ya 50. Manchester United wamepata bao lao la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Wyne Rooney.
Vikosi vilikuwa hivi:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Jesus Navas (Milner 71), Toure, Fernandinho, Nasri, Aguero (Javi Garcia 86), Negredo (Dzeko 75).
Waliokuwa benchi: Richards, Lescott, Pantilimon, Jovetic.
Manchester United: De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Fellaini, Valencia, Rooney, Young (Cleverley 51), Welbeck.
Waliokuwa benchi: Evans, Hernandez, Nani, Kagawa, Buttner, Amos.

TANZANIA YAZINDUA RASMI SIKU YA TEMBO KITAIFA LEO

 Gari la Maliasili likiwa limebeba Meno ya Tembo, wakati wa kujiandaa na Maandamano kuelekea Mlimani City kwa ajili ya maadhimishoya leo.
 Msanii wa Muziki wa Kitanzania, Mrisho Mpoto akianza kuongoza maandamano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuelekea Ukumbi wa Mlimani City leo.
 Maandamano ya Siku ya Tembo yakiwa yanaendelea kuelekea ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Kongamano hilo.
 Wasanii wa Mrisho Mpoto wakiwa wamebeba chatu katika maadhimisho ya Siku ya Tembo Kitaifa leo.
Mkurugenzi wa wanyamapori  Wizara ya maliasili na utalii Prof. Alexander Songorwa akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na utalii.
 Wadau mbalimbali wa utalii na kupinga mauaji dhidi ya Tembo wakiwa wanafuatilia kwa umakini maadhimisho ya Siku ya Tembo kitaifa.
 Wanafunzi kutoka Shule ya Jitegemee wakiwa wanafuatilia kwa umakini Maadhimisho hayo
Mrisho Mpoto akiwa anatumbuiza katika Maadhimisho hayo ya siku ya Tembo.
Mmoja ya waratibu wa Shuguli za Siku ya Tembo kitaifa Issa Isihaka kushoto akifuatilia kwa umakini siku ya Tembo kitaifa

 Picha ya Pamoja ya Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wadau.

AZAM FC WAIZIMA YANGA

Kipa wa Azam FC, Aishi Manula akiokoa hatari langoni mwake.
Azam FC wakishangilia ushindi wao dhidi ya Yanga leo.
Didier Kavumbagu akimtoka beki wa Azam, Erasto Nyoni (6).
Mashabiki wa Azam FC wakiishangilia timu yao.
Mashabiki wa Yanga.
Mwendesha mitambo wa Azam TV, Maulid Kidabu akiwa kazini.
Kikosi cha Azam FC.
Kikosi cha Yanga SC.
Azam FC leo wameizima Yanga SC baada ya kuilaza kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Mabao ya Azam yamefungwa na John Bocco, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga wakati ya Yanga yakiwekwa kimiani na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza. Kwa matokeo haya, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga SC wanaendelea kusuasua baada ya kutoka sare mbili kwenye mechi zao zilizopita mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City na Prison.
Kipa wa Azam FC, Aishi Manula akiokoa hatari langoni mwake.
Azam FC wakishangilia ushindi wao dhidi ya Yanga leo.
Didier Kavumbagu akimtoka beki wa Azam, Erasto Nyoni (6).
Mashabiki wa Azam FC wakiishangilia timu yao.
Mashabiki wa Yanga.
Mwendesha mitambo wa Azam TV, Maulid Kidabu akiwa kazini.
Kikosi cha Azam FC.
Kikosi cha Yanga SC.
Azam FC leo wameizima Yanga SC baada ya kuilaza kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Mabao ya Azam yamefungwa na John Bocco, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga wakati ya Yanga yakiwekwa kimiani na Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza. Kwa matokeo haya, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga SC wanaendelea kusuasua baada ya kutoka sare mbili kwenye mechi zao zilizopita mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City na Prison.

ARSENAL YAIZIMA STOCK CITY, YAPAA KILELENI EPL

Arsenal wakishangilia ushindi wao wa leo dhidi ya Stock City.
Aaron Ramsey akishangilia bao la kwanza aliloifungia Arsenal.
Charlie Adam (kushoto) akishangilia na mwanzake Geoff Cameron aliyeifungia Stock bao la kusawazisha.
Per Mertesacker akiifungia Arsenal bao la pili kwa kichwa.
Bacary Sangna akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la tatu kwa Arsenal.
Arsenal FC leo imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza Stock City mabao 3-1. Kwa ushindi huo, Arsenal wamefikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi tano. Katika mechi ya leo iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London, Arsenal wamejipatia mabao yao kupitia kwa Aaron Ramsey, Per Mertesacker na Bacary Sangna. Stock City wamepata bao lao kupitia kwa Geoff Cameron.

UPDATES SHAMBULIO LA KIGAIDI NCHINI KENYA: 59 WAMEUAWA, 175 WAKIJERUHIWA

Baadhi ya majeruhi wakitolewa eneo la shambulio na wengine kupatiwa huduma ya kwanza.
Taarifa kutoka serikali ya Kenya ni kwamba mpaka sasa watu 59 wameripotiwa kuuawa na 175 wakijeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate lililopo jijini Nairobi, nchini Kenya.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku.
Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo lililovamiwa ni kati ya 10 na 15.
Shirika la Msalaba Mwekundu awali katika taarifa yake lilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika shambulio hilo.
Mpaka sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi pamoja na vifaru vikiwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ya mateka.
Rais Uhuru Kenyatta katika taarifa yake amesema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake na miongoni mwa waliofariki ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.

VIKOSI VYA YANGA SC NA AZAM FC LEO


OMMY DIMPOZ AWADATISHA MASHABIKI WA MARYLAND NCHINI MAREKANI

Msanii mahiri wa muziki wa Bongo Flava, Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz' akipagawisha wakazi wa Maryland nchini Marekani jana.
Mashabiki waki-show love kwa Ommy Dimpoz.
Mashabiki wakijipa raha wakati wa shoo hiyo.
Ma-DJ kazini.