VITU AMBAVYO WANAUME HAWAPENDI KUTOKA KWA WENZI WAO!!
Haya niliyapata kutoka kwa mshauri wa masuala ya
mahusiano,ndoa na vijana Frederick Kyara.
1.Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao.
mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye
bali fanya kama una mpa ushauri.Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa
kwenye korido maana kuna giza kweli.Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye
korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini?weka balbu
bwana.Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.
2.Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele,mlalamishi.
Yeye ni kulalamika kuanzia jumatatu hadi jumapili.Japo
wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa.Na wenye gubu wanasusa
kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!
3.Wanaume hawapendi mwenzi mchafu.
Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la
kutunza nyumba wanayoishi.Uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.
4.Wanaume hawapendi mwenzi mbishi.
Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi.Utampa
mwanaume ushauri lakini haufanyii kazi
ubishi mwingi.
5.Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao.
No comments:
Post a Comment