JK aweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya
Bagamoyo-Msata
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi
kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata uliofanyika katika kijiji
cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo leo mchana.Wengine katika picha kutoka kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye
pia ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Meck Sadik(Wapili kushoto),Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wanne
kushoto) na kulia ni Waziri wa Mazingira Mhe. Theresa Hoviza.
Ndoto ya miaka mingi
ya kujengwa kwa barabara ya Msata-Bagamoyo kwa kiwango cha lami imetimia leo,
Jumanne, Septemba 18, 2012, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa
barabara hiyo katika sherehe kubwa iliyofanyika eneo la Kiwangwa.
Barabara hiyo ya kilomita 64 inajengwa na mkandarasi wa
ndani ya nchi, Estim Construction, na inagharimiwa asilimia mia na Serikali ya Tanzania bila
msaada kutoka kwa mfadhili yoyote.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania, Injinia Patrick L. Mfugale amesema kuwa barabara hiyo
inayogharimu kiasi cha Sh. bilioni 94, ikiwa ni pamoja na fedha za fidia na
kumlipa mkandarasi mshauri, itakamilika Juni mwakani.
Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais ameweka jiwe la msingi
kwenye barabara hiyo, Injinia Mfugale amesema kuwa mkandarasi wa sasa alianza
ujenzi tokea 2010 baada ya usanifu wa barabara hiyo kukamilika na baada ya
Serikali kumtimua mkandarasi wa mwanzo wa barabara hiyo, TACOPA, Novemba 13,
mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment