Friday, March 14, 2014

Weekend hii unaweza kuitumia kwa kuangalia hizi movie kwenye theater tofauti.


movieni300 Rise of an Empire ni movie ambayo inategemewa kuangaliwa sana na watu wengi kuanzia kesho kwenye theaters za hapa Tanzania.
Movie hii ambayo itaonyeshwa kwenye 3D imetoka kwa director wa 300 na Man of Steel. Pamoja na hiyo kuna movie nyingine zitakazoonyeshwa kwenye muda tofauti.
Cheki hizi ratiba na uchagua movie yako ya kwenda kuangalia kuanzia kesho 14/3/2014
1932722_518380071615403_998529629_o
1977464_10152082969808842_1854562348_n
1262536_518379108282166_178997219_o
1921189_518379384948805_551108562_o

Taarifa za Mtumbwi uliozama Mtwara March 13 ukiwa na kina mama wauza samaki..

Screen Shot 2014-03-13 at 10.13.49 PMTaarifa kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi ni kuhusu Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo.
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama 3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na wahusika wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo.

Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo March 14 2014


.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Thursday, March 13, 2014

PICHA SI ZA MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA - MAOFISA WA MALAYSIA

Waziri wa ulinzi Hishammuddin Hussein (katikati) akikanusha madai ya ndege kukaa masaa manne hewani kabla ya kupotea.
Picha za satelite za China.
...Askari maji wa singapore wakiendelea kutafuta ndege hiyo wakiwa umbali wa kilometa 700 kazikazini mwa Singapore na kusini mwa china.
...Nchi mbalimbali zinashiriki katika utafutaji wa ndege hiyo zikiwemo meli 42 pamoja na ndege 39.
Kikosi cha Wanajeshi wa hanga wa China wakiendelea kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines.
Maafisa wa Serikali ya Malaysia waliokuwa wanadadisi picha zilizopigwa na mtambo wa Satelite wa China ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege iliyotoweka, Jumamosi, wamesema kuwa mabaki hayo yalitoweka na huenda sio mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka siku ya jumamosi.

Waziri wa Ulinzi wa Malaysia Hishammuddin Hussein, pia amekanusha madai ya Marekani kwamba ndege hiyo ilipaa kwa masaa mengi kabla ya kutoweka na kupoteza mawasiliano
Amewaambia waandishi wa habari mjini Kuala Lumpar kuwa picha hizo zilizopigwa siku ya Jumapili,saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka na abiria 239 zinadaiwa zilitolewa kimakosa na maafisa wa China.
Aidha tetesi kuwa kifaa cha kupeperusha matangazo cha ndege hiyo kimekuwa kikituma taarifa imesemekana kuwa si ukweli .
Waziri huyo amesema kuwa kupotea kwa ndege hiyo sio kitu kilichotararajiwa.
Picha hizo zilitolewa na idara ya serikali ya China ya sayansi na teknolojia siku ya Jumatano.
Bwana Hussein kadhalika amekanusha ripoti ya jarida la Wall Street kwambandege hiyo ilituma data ya Engine yake kwa karibu saa 4 kabla ya kupoteza mawasiliano na kituo cha trafiki ya ndege.
Amesema kuwa juhudi za kuisaka ndege ghiyo zingali zinaendelea.