hivi ndivyo hali ilivyokuwa Mahakama ya Kisutu
jijini Dar jana
Kiongozi wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na
wenzake, kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya
kuahirishwa kwa kesi yao
Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya
pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo
hakimu anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la
Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo
waliharibu na kuiba mali mbali
mbali zenye thamani ya shilingi milioni
59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha.
Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote
isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana
kwa mshtakiwa namba moja.
Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi
kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine,
palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi
wa kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na
askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa
jijini Dar es Salaam.
Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu
kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa
mahakamani ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka
huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata
kwa nyuma hadi eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao
wakatawanyika.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo
taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na
pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya
maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu
itakapotajwa tena
Wafuasi wa Ponda, wanbaoshatakiwa pamoja naye, wakifunguliwa
pingu mahakamani
Mshtakiwa akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka
mahakamani na kupoteza fahamu
Askari wa kutuliza ghasia magerezani, nao walikuwepo
kikamilifu
Askari wa kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo
mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba
1, 2012
Polisi wa Mbwa nao walichukua nafasi yao
Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za
kugundua vitu vya asili ya chuma hapo.
Farasi wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh
Ponda, waliojikusanya nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar
es Salaam Alhamisi Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya
mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 1, 2012
Polisi wa Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi
mbele ya jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa silaha
na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama
Sheikh Ponda na pingu zake mikononi, akirejeshwa rumande.