Sunday, February 16, 2014
Magazetini leo February 16 2014
Kila siku hapa millardayo.com huwa naweka magazeti ya siku husika, kuanzia udaku michezo na hardnews nikiamini kwamba wakati mwingine unaweza kuwa mbali na yanakopatikana au yakawa yanachelewa kukufikia asubuhi.
Lengo la millardayo.com ni kuhakikisha kila Mtanzania anaweza kusoma stori kubwa za Magazeti kabla ya saa mbili kamili asubuhi ambapo kwa mwaka 2014 lengo ni kuhakikisha Magazeti yanakuepo hapa millardayo.com hata kabla ya saa moja asubuhi.
Unaweza kujiunga na familia ya Millard Ayo kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili kuwa karibu zaidi ya habari zote zinazowekwa hapa ambazo huwa link zinawekwa kwenye mitandao hii ya kijamii muda mfupi tu baada ya habari kupandishwa hapa.
Kwa wale walio-miss vitu vya Lil Wayne, hii ni habari nzuri kwenu.
Wakiwa katikati ya show hiyo Drake alitangaza ujio mpya wa album ya Lil Wayne ambayo itakuwa ni ya tano katika mfululizo wa album za Carter.
Tha Carter III ni moja ya album yenye mafanikio makubwa kwenye muziki wa Lil Wayne na Drake amesema May 5 itakuwa siku ya kutoa Tha Carter V.
“If you want to hear Lil Wayne at his best, if you wanna hear Young Money at they best..Carter V, May 5”, alisema Drake akiwa kwenye stage pamoja na Lil Wayne.
Ni kweli Lil Kim ni mjamzito, wengi walitaka kumjua baba… ndio huyu
Jibu ni kwamba rapper Mr. Papers ndio baba wa mtoto huyo ambaye ni wa kwanza kwa Lil Kim na wa pili kwa Mr. Papers kwasababu ana mtoto mmoja ambaye ana miaka 4.
Mr. Papers alisema Kim anategemea kujifungua kwenye mwezi wa tano au wa sita na ni mtoto wa kiume ambae bado hawajachagua jina la kumpa.
Inaaminika Lil Kim atatimiza miaka kati ya 39 au 40 July 11 mwaka huu.
Meno ya Tembo bado ni ishu, haya ni mengine yamekamatwa ya milioni 700.
Unaambiwa mbinu waliyoitumia jamaa ni kukata floor ya chini ya Gari na kutengeneza tank la bandia na kuweka meno hayo kisha kuweka kapeti juu yake chini ya kiti cha kukalia abiria wa nyuma ya dereva, Jeshi la polisi Mtwara linawashikilia watuhumiwa wote watatu.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mtwara.
Kuhusu kunusurika ajali Kala Jeremiah siku ya Valentine.
Saturday, February 1, 2014
Mambo sita usiyoyafahamu kuhusu wimbo wa Msambinungwa wa Tundaman.
Swali la kwanza lilikua ni kujua maana halisi ya Neno Msambinungwa,Tundaman alijibu Msambinungwa ni mtu Fulani hivi asiyeeleweka na hafai katika jamii yaani anaweza kuwa muongo,mtu mbaya mtu mwenye vitendo visivyofaa.
Swali la pili tulitaka kufahamu mpaka sasa wimbo wa Msambinungwa peke yake umemfikisha wapi kwenye hili Tundaman alijibu kwanza anamshukuru Mungu kwa mashabiki wake kwa kuipokea vizur huku akitoa mfano kuwa kuna siku moja hivi alikua anashuka kwenye gari anaenda kwa Maneck akawasikia watoto wanaimba walivyomuona wakaanza kupiga kelele.
Kuhusu jumla ya show alizofanya toka aachie wimbo wa Msambinungwa Tunda anadai amefanya show mbili tu kubwa ya kwanza ilikua ya bungeni na nyingine kwa President’Kikwete’ pale kwenye harusi ya Miraji iliyofanyika Mliman City.
Swali lingine lilikua linahitaji kujua Utofauti kati ya wimbo wa Msambinungwa na nyimbo zake zilizopita kwa hili Tunda alijibu>’Msambinungwa ni usemi ambao nimeuleta kwenye ulimwengu wa muziki maana siku hizi mtaani hata ukizingua kidogo tu unasikia watu wanakuita ‘We Msambinungwa’ usizingue so naona Msambinungwa nimefanya vitu vikubwa sana,ukisikiliza Msambinungwa utagundua’
Kingine ni kuhusu video ya Msambinungwa tunda alijibu>’Video ya Msambinungwa niliambiwa wimbo ni mkubwa so na video inabidi iwe kubwa kwa hiyo nilifikiria maana kuna kampuni niliilipa Kenya nikafikiria kufanya nao lakini nikahisi hawatoiweza wale wakenya nikaona video ya wimbo huu nifanye na Abbykazi,mpaka sasa nishashoot vipande kadhaa nimepanga mwezi wa pili kabla ya Valentine niizindue’
Kwa uchache ufahamu wimbo wa Msambinungwa ulivyokuwa>’Idea ya wimbo huu aliitoa mama yake mzazi na Tundaman na aliomba wimbo huo afanye na Marehemu Dr.Remmy Ongala bahati mbaya Dr.Remmy alifariki,baada ya hapo Tundaman alimtajia wasanii 5 wanaofanya vizuri ndipo mama yake akamwambia afanye na Ally Kiba.
Javier Hernandez Chicharito atakiwa na vilabu sita, lakini anabaki Man United
Wakala wa mchezaji Javier Hernandez amethibitisha kwamba mshambuliaji huyo anaendelea kubakia Old Trafford pamoja na kutakiwa vilabu sita barani ulaya.
Chacharito, 24, amekuwa akihusishwa na suala la kuondoka Manchester United ili kuweza kupata timu atakayokuwa akicheza muda mwingi.
Wakala wake Eduardo Hernandez mapema leo alikaririwa na ESPN Deported akisema: “Nilikuwa na mikutano na vilabu kadhaa, siwezi kuvitaja vyenyewe wala ofa walizotoa, wanavutiwa mno na Chicharito. Moja timu kubwa kabisa iliyopo katika Top 10 ya timu bora duniani ilikuwa moja ya vilabu sita vinavyomtaka Javier.
“Kulikuwa na klabu kutoka Germany, moja kutoka France, mbili kutoka Spain na Italy, kila timu kati ya hizo inamtaka. Lakini, mteja wangu bado yupo kwenye mkataba na Man Utd na ataendelea kuuheshimu mkataba huo.”
Kuhusu kupigana kwa wachezaji wa Yanga Cannavaro na Niyonzima – Yanga wakanusha
Benchi la Ufundi la klabu ya Young Africans limesikitishwa na taarifa zilizoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba wachezaji wa Young Africans kiungo Haruna Niyonzima na nahodha Nadir Haroub “Cannavaro” walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumatano jijini Tanga kuwa hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu taswira ya timu.
Akiongea na mtandao rasmi wa klabu www.youngafricans.co.tz , kocha msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema wao benchi la ufundi wameshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na kuzisoma leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya maslahi yao tu.
Kila mtu alikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nashikwa wasi wasi na waandishi waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika kitu tofauti na walichokiona.
“Sheria za soka zipo wazi, mchezaji au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa kuwapa kadi nyekundu, sasa tumeshangazwa na taarifa hizo zilioripotiwa leo kuwa kuwa kuna wachezaji wetu walipigana ili wachezaji wote walicheza kwa dakika 90 “alisema Mkwasa.
Nadhani imefika wakati tuisaidie jamii kuelewa uhalisia wa jambo husika liliotokea, kwani kuandika tofauti na kilichotokea kunasababisha jamii kuamini/kuelewa jambo ambalo silo lililotokea.
Katika mchezo wowote wachezaji kuelekezana/kukumbushana majukumu ni jambo la kawaida na ndicho kilichotokea katika mchezo dhidi ya Coastal kati ya Cananavaro na Yondani na Niyonzima na Cannavaro na si kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
“Hata mara baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa pamoja na kupeana pole kutokana na ugumu wa mechi, kisha wote kuondoka kuelekea hotelini kupumzika, na sisi kama viongozi hatujaona wachezaji kutofautiana kitu chochote hata kufikia hatua ya kusuruhishwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari “aliongeza Mkwasa .
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd “Chuji” aliyekua amesimamishwa kurejeshwa kundini.
Unataka kujua alichosema Okwi kuhusu Sakata lake lililopo sasa hivi,kipo hapa.
Emanuel Okwi ametoa tamko hilo ikiwa ni siku chache mara baada ya kusimamishwa kwa muda,huku uongozi wa Yanga ukisisitiza kuwa utamtumia mchezaji huyo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro inayotarajiwa kuchezwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda amesema yeye ni mchezaji wa Yanga na mapenzi yake yapo klabu hiyo ndiyo maana hataki kuzungumzia suala la mgogoro wa usajili wake, kwa kuwa hana mpango wa kurudi alipotoka.
Okwi alianza kwa kusema>>’Najua baada ya muda TFF itaniruhusu kucheza,sitaki kurudi nilipotoka kwa kulizungumzia suala la Etoile (du Sahel), pia sitaki kuizungumzia Simba kwa kuwa siyo klabu yangu’
‘Naipenda Yanga na mapenzi yangu yote yapo hapa, ndiyo maana leo hii nipo klabuni nikiwa mchezaji wao. Nilikuwa tayari kuanza kuichezea Yanga katika ligi hii (mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara) na Ligi ya Mabingwa Afrika’.
Kuhusu suala la sakata la kuzuiliwa kucheza Okwi,Katibu Mkuu wa Yanga Beno Njovu amesema kuwa watamtumia Okwi katika mechi dhidi ya Komorozine kwa kuwa wamepata ruhusa ya kumtumia kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).
MZEE GURUMO AFUNGUKIA SKENDO ZA DIAMOND
MSANII mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Muhidini Gurumo ambaye kwa sasa amestaafu, amefungukia skendo ya kuwa na mademu wengi inayomuandama Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni maeneo ya Ilala jijini Dar, Mzee Gurumo alisema: “Diamond ana nidhamu sana ila vile anavyotamba jukwaani na kudatisha mashabiki hapo ndipo balaa linapokuja, watoto wa kike wenyewe wanaanza kujisogeza kwake.
“Pamoja na skendo za mademu zinazomuandama, siwezi kumshusha thamani, ana haki ya kujiopolea mwanamke yeyote anayempenda, yeye kama mwanaume rijali wakati mwingine ni vigumu kujizuia na vishawishi hivyo.”
Subscribe to:
Posts (Atom)