Wednesday, April 10, 2013

lava lava ---- shaa (0fficial video)


EXCLUSIVE PHOTO OF PM ODINGA, MOSES WETANGULA AND KALONZO MUSYOKA IN SOUTH AFRICA

Exclusive photo of the big three from left Moses Wetangula, Raila Odinga and Kalonzo Musyoka at the Sundown Savanna in South Africa.


The CORD Summit of the Rt Hon Raila Odinga, Hon Kalonzo Musyoka and Hon Moses Wetangula share a laugh while on holiday in South Africa after a grueling campaign period.
The Principals are taking a few days off to recharge their batteries before returning to push the Reform agenda for the benefit of all Kenyans regardless of political affiliation.
They remain keen to see the faithful implementation of devolution as prescribed in the Constitution of the Republic and urge Kenyans not to lose sight of this.



SHILOLE ANASWA NA BWANA MZUNGU

SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’ wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.

Shilole akiwa katika pozi na mzungu wake aitwaye George.

Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa

akiwa dukani.

Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).

...Shilole na mzungu wake wakijiachia.


..Wakikatiza mitaani.




HIVI NDIVYO UHURU KENYATA ALIVYOAPISHWA NCHINI KENYA

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiapishwa.

Uhuru Kenyatta (kulia) akisalimiana na rais aliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki.

Uhuru Kenyatta wakati akijiandaa kula kiapo.


 Jaji Mkuu wa Kenya, Willie Mutunga, amtambulisha rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta.

 Rais Uhuru Kenyatta akikabidhiwa upanga na nakala ya katiba ya Kenya kutioka kwa rais mstaafu, Mwai Kibaki ikiwa ni ishara kuwa amekuwa amiri jeshi mkuu wa Kenya.

 Rais Uhuru Kenyatta na 'First lady', Margaret Kenyatta.

 Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake.

 William Ruto makamu wa Rais wa Kenya akisaini.

Kibaki akiwasili.

Rais Mwai Kibaki anayeondoka madarakani akikagua gwaride la heshima.





MWAKA MMOJA KIFO CHA KANUMBA: LULU MACHOZI MPAKA BASI


STADI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) ameibua upya simanzi, machozi na huzuni ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha staa aliyeijengea Tanzania heshima kubwa, Steven Charles Kanumba.STADI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) ameibua upya simanzi, machozi na huzuni ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha staa aliyeijengea Tanzania heshima kubwa, Steven Charles Kanumba.

Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' (katikati) akijiandaa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kanumba, kulia ni mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa na kushoto ni mama yake mzazi, Lucresia Kalugira.

Gazeti lenye hadhi ya nyota tano, Risasi Mchanganyiko lina mkusanyiko wa matukio ya kuhuzunisha kama yalivyonaswa na timu ya mapaparazi wetu, Jumapili Aprili 07, mwaka huu katika siku maalum ya kumkumbuka, iliyopewa jina la Kanumba Day.
Lulu ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Kanumba, yupo nje kwa dhamana akikabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii huyo mwenye mashabiki lukuki ndani na nje ya Bongo.

DAR ES SALAAM
Shughuli hiyo maalum ambayo ililenga kumuombea dua marehemu Kanumba na kumuenzi kwa mema aliyoyafanya iliambatana na uzinduzi wa Filamu ya After Death ambayo inaelezea maisha ya vijana wadogo aliowahi kuigiza nao katika za Sinema za Uncle JJ, This is It na Big Daddy.
Kanumba Day iliandaliwa na staa wa kike wa kiwanda hicho, Jacquline Wolper ambaye pia ndiye muandaaji wa filamu ya After Death.
Katika hafla hiyo, pia ilizinduliwa sinema ya mwisho kutayarishwa na marehemu Kanumba iitwayo Power & Love ambayo iko chini ya Kampuni ya Kanumba The Great.

KWANZA KANISANI
Awali, mishale ya saa 4:00 asubuhi, familia ya marehemu Kanumba, wasanii, ndugu, jamaa na marafiki walijumuika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Temboni katika ibada.
Katikati ya ibada hiyo ya kawaida ya Jumapili usharikani hapo, kulikuwa na sala maalum ya kumuombea marehemu Kanumba.
Utulivu ulikuwa mkubwa kanisani hapo, huku Lulu akiwa katikati ya mama Kanumba, Flora Mtegoa na mama yake mzazi, Lecresia Kalugira wakiwa wamevalia sare ya magauni meupe yenye mchanganyiko kidogo wa rangi na vitambaa vyenye mchanganyiko wa rangi ya pinki na nyeupe vichwani mwao.
Wakati sala ikiendeshwa, Lulu alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi – kazi kubwa kwa wazazi hao ikawa kumtuliza.
Baadhi ya mastaa walionaswa na kamera ya Risasi Mchanganyiko kanisani hapo ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jokate Mwegelo, Irene Uwoya na wengineo.

Wasanii wakiwa katika kaburi la Kanumba.

SAA 6:30 MCHANA
Ibada ilifikia kikomo saa 6:30 mchana ambapo msafara wa kwenda nyumbani kwa mama Kanumba, jirani kidogo na kanisa hilo ulianza.
Utulivu ulikuwa wa hali ya juu nyumbani hapo ambapo wageni wote walipata chakula cha mchana kabla ya safari ya kuelekea katika Makaburi ya Kinondoni....


Saturday, April 6, 2013

KAJALA AANIKA YA JELA


MSANII AFA AKIJIDUNGA

Stori: Denis Mtima
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya aliyetambulika kwa jina moja la Rocky mkazi wa Kawe, Dar amefariki dunia baada ya kujidunga madawa ya kulevya 
   


Ray C
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo na kuomba hifadhi ya jina lake, marehemu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-27, alipatwa na mauti Machi 27, mwaka huu baada kunywa vidonge kumi vya dawa za kulevya aina ya Valium kisha kujidunga sindano tatu za Cocaine.



Langa
Chanzo hicho kilidai, marehemu alikuwa akionywa mara kwa mara na ndugu zake lakini alikuwa akikaidi hali ambayo ilisababisha akamatwe na kuswekwa jela kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiwa.
“Marehemu alitoka Segerea juzi Jumatatu (Machi 25) na Jumanne akaanza kutumia tena dawa za kulevya kama kawaida, akajidunga vidonge kumi kwa mpigo.



Aisha Madinda
“Akaweka kete tatu kwenye bomba la sindano tayari kwa kujidunga ndipo alipozidiwa na kupatwa na umauti akiwa bado hajakamilisha zoezi hilo,’’ kilidai chanzo hicho.
Kabla ya marehemu hajazikwa katika makaburi ya Kawe, askari walifika katika eneo hilo ambapo walibainisha kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutumia madawa ya kulevya katika eneo hilo.




Lord Eyez

“Vijana wengi hapa Kawe wamejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Tunawashauri hasa hawa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao walitangaza kuacha basi waache kweli maana wakirudia basi kifo kinawaita.



Msafiri Diof
“Historia inaonesha kuna wimbi kubwa la wasanii ambao wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya kwa siri kubwa,” alisema afisa mmoja wa polisi aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji.

Thursday, April 4, 2013

SHILOLE, Q-CHILLAH LAIVU!


MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na muimba Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ hivi karibuni waliawaacha midomo wazi wasafiri ndani ya ndege kufuatia tukio lao la kufanya ‘malavidavi’ bila kujali.

Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.

“Tunakubaliana na kazi zao, lakini kusema ule ukweli, sisi abiria wenzao tulishangaa sana, unajua kuonesha vitendo vya mahaba ndani ya ndege si utamaduni wetu Wabongo,” alisema abiria huyo aliyekuwa akienda Mwanza kikazi.
Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana majina makubwa katika burudani za Bongo.
Kufuatia taarifa hizo na kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya ‘pipa’.

Kwa upande wake, Shilole alisema kuwa mabusu ni vitu vya kawaida kwake ikizingatiwa Q-Chillah ni mwanamuziki mwenzake kwa hiyo hakuna tatizo.
“Jamani kwani mabusu yana shida gani, yule (Q-Chillah) ni mwanamuziki mwenzangu na tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si vinginevyo,” alisema Shilole.
Q-Chillah simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokelewa, lakini baadhi ya watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo hana kawaida ya kupokea simu kama namba hazijui.